Kwa sasa Tz haiwezi kufanikiwa katika lolote. Tatizo kubwa ni ubaguzi wa imani za kisiasa.
Nina hakika kwenye haya mashindano, hata kama mchezaji atakuwa mzuri namna gani lakini ikafahamika kuwa ni mwanachama au shabiki ya chama cha upinzani, watamwondoa.
Mfano mzuri ni Timu ya Taifa ya soka ambapo Makonda alithubutu hata kutamka kuwa ipo kwaajili ya kutekekeza sera za CCM. Kumbuka kichapo tulichokipata.
Hata kwenye teuzi mbalimbali za kazi za kitaalam, unatazamwa uanachama au ukada. Wakati ukweli unajulikana kuwa watu wengi walio na uwezo, akili kubwa na upeo mkubwa hawapo CCM au siyo mashabiki wa CCM (ripoti ya TWAWEZA - CCM inapendwa zaidi na watu wajinga na baadhi ya wazee).