Watu 50 ni wengi sana.
Kama utakumbuka CC wakati wa uchaguzi wa 2015 ilikuwa na wajumbe 32.
Mkiti JK akaja na majina matano, BKM, JYM, JPM, ARM na ASA
Wajumbe watatu wa CC (Nchimbi, Kimbisa na Sofia Simba) walimgomea mkiti kwanini aje na majina 5 badala ya wote waliochukua fomu wajadiliwe.
Bila shaka kuna watu wachache sana ambao wana nguvu kubwa ya ushawishi na muono wa mambo yaendeje. Wengine wanawaita "deeo state" who knows.
Cha msingi tuombe Mungu kuwe na utulivu, kama watu wanabishana kwa hoja basi maisha yaendelee, isifikie ile hali ambayo JK alisema sio rahisi watu kuachiana glass za vinywaji.
Nadhani mijadala ya tukope au tusikope, na kama tunakopa tunawekeza kwenye nini ili tupige hatua haraka kama nchi, hii mijadala ina tija kwa kupanua ufahamu, tumejua ni kiasi gani tunadaiwa na debt threshold ikoje kwetu (Tanzania).
Tutakiane heri za Mwaka mpya 2022, tuishi kwa ku-debate ila tubaki tukiheshimiana pasi kutwezana au kuwabagaza wale ambao tunatofautiana kwa hoja.