Tunamlazimisha Babu Seya kurudi kwenye Muziki ila kiukweli amechoka, amezeeka

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Kiukweli huyu mzee tulivipenda vitu vyake ila tusimlazimishe kurudi kwenye Sana'a ya mziki! Huyu mzee kachoka na kazeeka hivyo hata akirudi kwenye muziki performance yake itakuwa poor.

Ingawa kuna wengine wanataka kumtumia kisiasa mi ningeshauri aachwe apumzike
 
Mkuu umetumia vigezo gani kumuona kachoka..!?,
Ni nani anataka kumtumia kisiasa..!?
Mashabiki wake ndio wana uwezo wa kuamua Kama kachoka au la..!
 
Mkuu umetumia vigezo gani kumuona kachoka..!?,
Ni nani anataka kumtumia kisiasa..!?
Mashabiki wake ndio wana uwezo wa kuamua Kama kachoka au la..!
Sina shaka haya maswali ingawa umeuliza nina imani utajijibu mwenyewe tena vizuri kabisa
 
Huyu si alikokoka na akasema hata kama atatoka muziki na yeye basi,

Au kaambiwa “NATAKA UIMBE”?
 
Mkuu umetumia vigezo gani kumuona kachoka..!?,
Ni nani anataka kumtumia kisiasa..!?
Mashabiki wake ndio wana uwezo wa kuamua Kama kachoka au la..!
Labda akimtamzama usoni na vile ameungua kwa mkorogo basi anamuona kachoka..eti USO wake umekua kama chips yai iliokosa mafuta!
 
Babu seya Amechoka kweli Apumzike amuhachie papii kocha.
 
Bado hajachoka. Mwangalie maestro King Kiki kwa mfano, au Said Mabera kwanza kabla hujasema hivyo. Kwenye mziki hakuna cha kuzeeka.
 
Haya bibi Seya tumekuelewa, mzee kachoka.
 
Kila nabii na wakati wake
 
Hata punda afe, lazima mzigo wa bwana ufike.
 
Nahisi haka ni kadalili ka uoga hivi..? Unawezaje kutamka kachoka wakati yeye hajatamka? Kumbuka muziki si kama kuponda zege, muziki ni burudani bhana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…