Tunamlipa Nini Fiston Mayele Kwa Kuitangaza na Kuifikisha Mbali Ligi KUU Tanzania Bara?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Wengi tumekuwa tukishangilia Fiston Mayele. Pale anapofunga tumekuwa wepesi kuiga namna yake ya kipekee ya ushanhiliaji. Hata wale wa upande wa pili nasikia walikuwa wakitetema kisiri huko faragha.

Wengi tumeinjoy uwepo wake katika Ligi yetu pendwa.

Kama umekuwa mfuatiliaji makini wa LiGI KUU utakubaliana nami kuwa tangu atue Jangwani kuna exposure fulani hivi ambayo imekuwa ikikosekana huko nyuma ila yeye amekuja nayo.

Kwa mfano kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wafuatiliaji wa mpira wa wana michezo nje ya mipaka ya Tanzania.

Pia kuna ongezeko kubwa sana la kundi rika la chini kufuatilia mpira zaidi msimu huu kuliko misimu yote iliyowahi kuwako.

Aidha, Vyombo mbalimbali vya Kimataifa vya Habari na Burudani vimeanza kuiangazia Ligi Yetu ya Tanzania. Kwa mfano mashirika ya mpira wa miguu kutoka barani Ulaya ie LaLIGA.

Pia ongezeko la wachezaji wa kigeni kutoka nje ya mipaka ya Tanzania ni matunda ya Uwepo wa Mayele katika LiGI KUU. Kila mchezaji hivi sasa anatamani kucheza Tanzania ili awe kama Fiston Mayele.

Si Makanisani, Si Misikitiki wala Maofisini Fiston Mayele amekuwa gumzo. Hiyo yote inatokana na jitihada zake za kuosaidia LiGI KUU ya Tanzania kupata recognition kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kwa lengo la kuvutia uwekezaji.

Haya Yote Anafanya FISTON MAYELE. Kwa moyo wake mkunjufu ameamua kuwa mzalendo wa hiari kwa Taifa la Tanzania.

Sio Kwamba angeshindwa kufanya haya kwako lakini amechaguwa kutufanyia hivi watanzania.

Je, TUMEJIANDAA KUMLIPA NINI?

View attachment 2278661
 

Attachments

  • IMG_0330.jpg
    145.8 KB · Views: 7
Kijana uhaba wa team yako pendwa usipitilize hadi ukatengeneza ubaguzi na kuwadhalau wachezaji wa team zingine please relax kijana..... AHSANTE MPOLE
 
Nikusahihishe staili ya mayele na yeye kaiga kwenye season ya sanger. Ni season ya waturuki.
Sasa kaangaalie hiyo season then uje kusema season na mayele stayle ipi imeanza.
 
Wengi!!! wewe na nani?

Uwe specific, maana kutumia neno "wengi wetu" kwa wengine ina sound kama tusi

Tumetifautiana kwasababu sio wote tuliokuwa tunaona ushangiliaji wa aina ile ya kutetema maziwa kwa mwanaume ni ishara nzuri.

Wengine wanasema jamaa alikuwa ana tetema kifua. yes they might be right inatokana na wewe ulivyokuwa unaangalia.

Wengine walikuwa wanaagalia view ya upande wa nyuma, sasa hawa watu wakikuambia walikuwa wanaona mtetemo kwenye makalio usiwabishie hiyo ni view waliyoiona walio kaa nyuma.

But yote kwa yote lazima tumpe pongezi kwa hatua aliyofikia kwa kua mshindi wa pili.

Lakini swala la kutumia wingi bila kuweka mchanganuo wa aina gani ya watu wanohusika na huo wingi katika kuelezea waliopendezewa na aina ile ya ushangiliaji hapo unakuwa unatukosea watu wengi sana.
 
Idadi ya wajinga inaongezeka kwa kasi kubwa sana huko Yanga. Ushamba na ulimbukeni unawasumbua sana
 
Acha ulimbukeni, amka kapambane na maisha wewe
 
Acha ulimbukeni, amka kapambane na maisha wewe

Mm ni mjasiriamali.

Ninaenjoy financial freedom right now.

Sipaswi kuamka asubuhi na kwenda kwenye ofisi ili nikawafanyie kazi wengine. [emoji23]
 

Uwezi ukawa mpenzi wa LIGI KUU na wakati huo huo ukajitenga na ukweli.

Kuna kitu Fiston amekiongeza.
 
Nikusahihishe staili ya mayele na yeye kaiga kwenye season ya sanger. Ni season ya waturuki.
Sasa kaangaalie hiyo season then uje kusema season na mayele stayle ipi imeanza.

Sanger imeanza kuigizwa mwaka 2017

Ikazinduliwa mwaka 2019

Mayele ameanza kutetema kabla ya mwaka 2016.
 
Maelezo meengi! Point hakuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…