Linapokuja swala la kuugua mtu, hata kama una uadui naye, jambo jema sana kwako ni kumsaidia kwa hali na mali ili kuonyesha kuwa sote hapa duniani tunategemeana, na hakika baada ya kupona mtakuwa marafiki wa kweli kabisa. Hivyo kumwombea na kumsaidia ni jambo jema sana (unajiwekea hazina) kuliko kuendeleza bifu na chuki bila kujua leo kwake kesho kwako.