Tunamsaidiaje Irene? Kanyimwa talaka na mumewe, kesi Jumatatu mahakamani

Umenena vyema mkuu ndoa hailazimishwi lakini ni kosa kumpa mimba mke halali wa mtu kwa maana ya kuwa bado hajapewa talaka rasmi na mumewe wa ndoa. Hapo mwanamke ni mzinzi mbele ya sheria na mbingu. Alitakiwa aende mahakani kudai talaka kwa lazima kabla hajashiriki tendo la ndoa na mtu mwingine.
 
Hapana, ingawa ndoa ni fungamano la hiyari na hujengwa ktk upendo miongoni mwa waliomo ndoani, ila kuibatilisha kwa talaka lazima awasilishe vigezo muhimu mahakani.

Mfano, vipigo vinavyopitiliza,magonjwa ya kuambukiza, vifungo virefu nk. Awafuate tu wanasheria wamsaidie, si kuchokana tu.
 
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa mwaka 1971 hakuna hata sababu moja ya mahakama hapo kuvunja ndoa.
 
Hapo hamna sababu za msingi za kuvunja ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa.

Lakini pia Irene amekosea kuzaa kabla ya talaka rasmi.

Hakika analo la kujibu mbele ya mahakama!!
 
Hapo hakuna cha rushwa wala nini.. Sheria iko wazi...Irene ana hatia..period!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…