Tunamshukuru vipi Mzee Mkapa katika ulimwengu wa utandawazi?

Tunamshukuru vipi Mzee Mkapa katika ulimwengu wa utandawazi?

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Nakumbuka nilirudi likizo Mwaka 1999 Nikakuta mzee anayo simu ya Motorola kubwa nikashindwa kuitofautisha na radio call aliyokuwa anatumia na simu ya motorola aliyokuwa nayo na kipindi hicho ndio huduma za simu zimeanza kutolewa kwenye vibanda vya wafanyabiashara. Cha kushangaza ilikuwa huduma ya kubeep (kama walivyokuwa wanaita kubeep)' ilikuwa nı Tshs 500.

Kwa kweli sikuweza kuamini. Kulikuwa na huduma pia ya kutuma 'meseji' na kupigiwa. Yani unampa mtu namba ya simu ya mwenye kibanda, anapga na wewe pia unamlipa mwenye kibanda kupokea simu yako. Kijiji kizima tulikuwa tunajuana..so simu ikipgwa toka kwa ndugu yako mjini utatafutwa mpaka upatikane.

Sikumbuki tulilipia sh ngapi kutuma msg na kujibiwa kutumia simu ya mwenye kibanda. Kiukwelia tumetoka mbali. leo hii kuna mijitu inalinga na simu SMARTPHONE ikikosoa baadhi ya mambo ya Mzee Mkapa hapa JF ,nyie watu nyie no body perfect.
 
Mtu anapoomba kwa hiari kupewa dhamana halafu akapewa, lazima awajibike. Tuache kmsifu bure kama vile alipewa bure. Mzee Mkapa alijitahidi kutimiza wajibu wake, kadri ya uweza aliokuwa nao.

Ila tukumbuke alikuwa anapenda sana watu wanaitwa wawekezaji toka nje, na rangi zingine zingine. Hata kama gharama yake ilikuwa kutufanya wote sisi tukawa bure na si kitu
 
Mtu anapoomba kwa hiari kupewa dhamana halafu akapewa, lazima awajibike. Tuache kmsifu bure kama vile alipewa bure.
Mzee Mkapa alijitahidi kutimiza wajibu wake, kadri ya uweza aliokuwa nao. Ila tukumbuke alikuwa anapenda sana watu wanaitwa wawekezaji toka nje, na rangi zingine zingine. Hata kama gharama yake ilikuwa kutufanya wote sisi tukawa bure na si kitu
Ndugu yangu,si dhambi kumsifu mtu akifanya jambo jema, ni uungwana na unyenyekevu kumsifu mtu aliyetimiza wajibu wake vizuri hata km aliomba mwenyewe nafasi hiyo.

Halafu lazima ujue kuwa binadamu tuna mapungufu yetu pia, hivyo kuteleza ni sehemu ya maisha.Hata wewe ukitimiza wajibu wako vizuri bila kujali kasoro zako tutakupongeza na kukusindikiza kwa sifa kede kede siku ya msiba wako.
 
Sijui kwa nini nimekumbuka ile skandal aliyoiibua mrema kupindi bado ana akili.
 
Ndugu yangu,si dhambi kumsifu mtu akifanya jambo jema,ni uungwana na unyenyekevu kumsifu mtu aliyetimiza wajibu wake vizuri hata km aliomba mwenyewe nafasi hiyo.Halafu lazima ujue kuwa binadamu tuna mapungufu yetu pia,hivyo kuteleza ni sehemu ya maisha.Hata wewe ukitimiza wajibu wako vizuri bila kujali kasoro zako tutakupongeza na kukusindikiza kwa sifa kede kede siku ya msiba wako.

Ndio maana tumueleze jinsi alivyo. Ubaya na wema wake.
 
Sawa hivyo ni vitu vidogo hata asingekuwa yeye vingekuja tu. Ni swala la nahitaji ya nyakati

Mkapa alifukia wachimbaji wakiwa hai bulyankhulu
Mengine nitayataja baadaye
 
Ndio maana tumueleze jinsi alivyo. Ubaya na wema wake.
Uzuri ni kwamba alikiri makosa ktk Kitabu chake,sasa Mungu husamehe wakosefu wanaokiri madhaifu yao,sasa wewe ni nani wa kuhukumu?.Vipi siku ukifa ukaona Mkapa yupo Mbinguni utajisikiaje?,au utafanyaje?.
 
Back
Top Bottom