Tunamsifu Bernard Morrison, ila kwa 75% hana Msaada kwa Simba SC na ni Mzigo, lakini kwa 25% ndiyo huwa anatusaidia

Kocha wa Madrid ya Bonyokwa hana ubavu wa kumrekebisha au kumpiga benchi kama alivyofanya Prof Nabi kwa Saidoo
 
Sure tena akaandika na kwenye page yake kwamba anajilinda asije kupigwa uviko19 .Kweli alishajiona mess[emoji16]
 
Sure jamaa anapenda Sana kamera anasahau Ana majukumu gan yaliompeleka Simba.
Chenga zipigwe lakin sio kila Mara ili kutaka kuonyesha wewe ndie wewe ,wakina lonardo wanapiga chenga pia wanaibeba timu kwenye nyakat ngumu ,Jana nilikua bandan alivyotoka nikafurah Ila wajinga kibao wakalaum ,baadae wakatoka kwa aibu baada ya kuona changes na kupatikana goli baada ya kuingia shomi.

Jamaa Ni mchezaj mzur Sana sema showoff na ufather mwingi vinamharibu .

Mtu Kama huyu piga benchi mechi za maana na timu itoke na ushindi bila yeye alafu yeye achezeshwe mechi za kawaida Sana za kwenye ligi ,lazima nidhamu itarud tu.
Ntibanzokiza nae alianza ufather huo lakin big up kwa nabi aliamua amuonyeshe kuwa wewe Ni mtu wa kawaida Sana linapokuja swala la nembo ya yanga ,for sure toka hapo kawa na nidhamu balaa .

Kwa hapo watani wametufundisha kitu hata Pablo aige Hilo niamin nidhamu itamrudia tu.

Nashaur hata derby asicheze kabisa maana najua hatafanya chochote .
Wawa ,Morrison ,kanoute ,Bocco kwenye derby watuache kidogo ,Bora tufungwe Ila hao watu wasichezeshwe kabisa .
 
Hata Wanazi wakikushambulia lakini Ukweli Morrison ni mvua ya msimu.
 
Anachonifurahisha zaidi kwenye hizo asilimia 25 ni pale anapoamua matokeo. Atacheza vibaya dk 89 lakini dakika 1 anaweza kubadili Kila kitu.

Ila jamaa wakati mwingine ana maudhi.
 
Si kocha kampa kile cheo cha akina Messi na Ronaldo (free role) kwahiyo mwache avimbe bana
 
Ban yako ilikuwa lifted lini we mbwiga
 
Morrison amejaaliwa kipaji kuliko hata Luis Miquissone. Leo Luis yuko Al Ahly, Morrison kabaki Bongo anaupanda mpira! Masihara mengi yasiyo na msingi.
 

Ndio maana Msimu uliopita Miquissone alikua anamuweka benchi…Konde boy kipaji anacho halafu mtu wa kazi!
Morrison kipaji kingi kichwani sifuri na masihara ya kijinga kila kukicha!
 
Wanadamu kwenye roho za kitu...simba ikishinda tunasahau mapungufu ya wachezaji, tukipoteza tunaanza ku justify MTU mmoja mmoja.

Huu sio ukomavu wa kimpira na uelewa kuhusu mpira wa miguu. IPO hapa ya kuchambua makosa ya timu na mchezaji mmoja mmoja kabla ya mechi, sio baada ya mechi.

Game tactics na approach ya mchezo husika inabadili sura ya timu. Ikiwa Pablo kashasema tushambulie taratibu na sio kwa pupa, Morrison na Dilunga msikabe, wewe shabiki unataka kitu gani?

Timu ilikwenda Zambia kuhitimisha safari ya kwenda hatua ya makundi ni kitu gani kingine mnataka?

Mara nyingi falsafa ya kocha inaathiri malengo ya timu na uongozi kwa ujumla. Mifano hai ni kwa Man City na Chelsea msimu ulioisha. Nani alitarajia kuwa Man city atafungwa fainali mbili zote na timu ile ile tena goli moja tu?

Sent from my Infinix X559 using JamiiForums mobile app
 



Sent from my Infinix X559 using JamiiForums mobile app
 
Umeandika kweli tupu.
Kiukweli pale hamna kitu. Ni hivyo tu Tanzania hakuna wachambuzi kuna wachambaji.
Kwa umri aliokuwa nao bwana yule hawezi kubadilika.
 
Mimi ni mmoja wa watu ambao sifurahishwi na uchezaji wake akiingia team inakosa utulivu kona anataka kupiga yeye faulu yeye anapenda kucheza na majukwaa.
 
Kukumbusha Ni muhimu kuliko kuimba pambio kwenye hakuna ,hata mechi ikimkubali vipi bado anakua na ufather na mbwembwe zisizo na ulazima .

Kuna game unaona kabisa wachezaji wakiacha kucheza na majukwaa na kuwa serious uwezo wa kupata goli 5 na kuendelea Ni kawaida tu ,Sasa ugonjwa huu lazima ukemewe ,Mara nyingi simba ikipata goli 2 au 3 wachezaji wanaanza show off za kipumbavu ,timu lazima iwe na spirit ya kuheshimu mchezo dakika ya kwanza had 90 ,nadhan unafuatilia mpira wa ulaya ,timu ikikuotea inakupiga had 7 wanakua hawana muda wa kupoteza yaan wanakaza mwanzo mwisho.

Tukikaa kimya huu ujinga utaendelea kutucost ,refer mechi dhidi ya wale makiriri ,Simba imetolewa sabab ya huu huu ujinga wa kuamin game imeisha na kuanza kucheza na majukwaa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…