Tunamtaka Joh Makini wa 'Hao', huyu wa ni-come ndugu zake njooni mumchukue

Tunamtaka Joh Makini wa 'Hao', huyu wa ni-come ndugu zake njooni mumchukue

Alicho jaribu kumentain ni ule mtindo wake wa Kusuka Nywele, nadhani hajabadili Msusi...!

KUHUSU MUZIKI ni Madudu tuu, bora kipindi kile anapigania jina Mfalme, nilikuwa namuelewa vizuri..
 
kuna wimbo wanatikisa kope za macho nayo sijui inaitwa nicome hata siwaelewi kabisa
 
kuna mtoto alishawahi kusema anaskia joh anabebwa mpka anaanza kuhisi ni ukweli
 
Kweli mkuu hata ule wimbo wa kata leta hamna kitu, ni aibu from hero to zero, lakini tatizo lake sasahivi ni nn ?
 
Aisee huyo chalii tangu amehamia dar amekua wakisoroooo kama jamaa wa huko tu.
 
Mimi ni mmoja wa mashabiki wa msanii Joh makini tangu anatoka akitengenezwa kuja kuchuana na msanii mwenye kipaji kuliko wote bongo (Chid benz).

Mwamba wa kaskazini alitikisa anga la mziki na kila mkwaju alioachia ulikuwa wa Moto ndio maana alipojiita Tz Jay z sikumbishia sana.

Nakumbuka ngoma zake kama Mfalme,Hao,muda,sijutii,Stimu zimelipiwa,Show za Joh,Kilimanjaro n.k, collabo alizopiga akangaa kama utaipenda ya Hussein machozi na nyinginezo.

Huyu Joh makini wa Weusi simuelewi kabisa yaan amepwaya katika uandishi kuliko zaman, hatumuoni kama Hip hop icon wa kaskazini yaani anakoelekea haeleweki kabisa.

Chondechonde tunamhitaj Joh Makini wa Hao, huyu wa madaraka,Nicome ndugu zake njooni mumchukue.


tutamchukua ucjal
 
Eti”Nikiona kibinda mi nadinda nakitia mimba”ahahaaahaahhaahahaha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hata kama kubadilika si kwa ujinga huo.Ptuh.
nikiskiaga huo wimbo unapofika kwenye huo ubeti huwa nazima radio
 
Back
Top Bottom