tunanaomba msaada/ushauri....

tunanaomba msaada/ushauri....

The Kop

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2010
Posts
209
Reaction score
93
sisi ni vijana wasomi wa shahada kutoka chuo cha mipango ya maendeleo vijijini Dodoma. tumeunda kikundi cha wajasiriamali kinachoitwa Poverty Eradication Through Agriculture (PETA). kikundi kina jumla ya watu saba,mwenye elimuya chini miongoni mwetu ni kidato cha 4. kwa ujumla tunajishughulisha na kilimo cha umwagiliaji na tuna matarajio ya kufuga kuku wa asili kwa njia za kisasa. hadi sasa tumeandaa shamba la ekari 6 ambazo tunatarajia kulima mpunga, Tuliamua kulima mpunga, japo halikuwa wazo letu, baada ya kuwepo tishio la mvua nyingiambazo zingetuingiza hasara endapo tungelima zao lingine, ukizingatia mtaji ulikuwa wa kuunga unga(tuliweka kiasi cha boom tulichokuwa tunapata). Vile vile tumeweza kuchimba mtaro wa mita 300 kutoka na kituo cha maji (water point) ya ft6*6

tunataka kupanua kilimo chetu,kwani tuna shamba la eka 50, ambazo tumepewa na mlezi wetu wa kikundi. Shamba hilo bado bikra kabisa kwani tumefyeka pori ambalo lilikuwa halijalimwa kwa muda mrefu sana, na udongo wake ni wa mfinyazi mweusi tii. Kwa ujumla udongo huu unakubali kila aina ya mzazao.

Tumejaribu kwenda Halmashauri ya wilaya ya bunda.tukiwa na mchanganuo wa japo tukopeshwe kutoka mfuko wa maendeleo ya jimbo au kupitia mfuko wa vijana lakini wanadai hakuna pesa,tumejaribu kwenda bank,anadai hatukopesheki, hatu secutity. Tunaomba wadau, kama tuna weza kusaidika namna yoyote ile,hususan kukopeshwa, tusaidiwe, ili tukabiliane na changamoto za kukosa ajira.

MAKADIRIO YA KUANDAA EKARI 20 ZA MPUNGA
Kufyeka miti na kuondoa visiki 50,000@eka
50,000*20= 1,000,000/=
kulima kwa mara ya kwanza 50,000/= kwa eka
50,000*20= 1,000,000/=
kulima kwa mara ya pili
40,000/=@eka
40,000*20=800,000/=
kulainisha(leveling) 30,000/=@eka
30,000/=*20=600,000/=
kuweka makinga maji 30,000/@eka
30,000/=*20=6,000,000/=
JUMLA NDOGO 4,000,000/=

Mipira ya kummwagilia,( tayari tuna mita 200 na mashine tunayo)
mita 500@100=150,000/=*5=750,000/=
Petroli lita 200@2500=500,000/=
JUMLA NDOGO=1,250,000/=

JUMLA KUU 5,250,000/=

MAKADIRIO YA MAPATO
Wastani ekari moja inatoa gunia 40-45, ukipanda mbegu za kitaalamu na kulima kitaalam
40*20=800
wastani wa bei ya ginia la mpunga= 100,000
100,000*800= 80,000,000/=
80,000,000/= toa matumizi, tuseme mil 10
faida mil 70.
NB Kuna NGO inaitwa THIRD MILLENIUM PEACE INITIATIVE FOUNDATION, BUNDA, wameahidi kutupatia pembejeo na utaalamu wa kilimo bure. Huo ukokotoaji ni kwa mujibu wa wataalamu wao.
kwa mawasiliano namba za m/kiti wa kikundi 0768092016
naomba kuwasilisha.
 
Haya ndiyo mawazo tunayotaka vijana wetu wawe nayo. Big up.
Naomba niwashauri katika mahesabu ya faida mzingatie riba kwa maana pesa hiyo mtaikopa hivyo haiwezi kutolewa bila riba.
kila la kheri.
 
Wakuu Hongera sana kwa jitihada zenu za hali na Mali,

Kwa sasa ishu ya Mikopo ni Nhumu sana na hata pesa zilizopo Halimashauri zinaliwa tu na mwisho wa siku utakuja kusikia riport ya halimashauri wanasema walikopesha vijana kama 50 hivi kumbe ni hakuna,

Kama Mikipo itashindikana ni bora nyie msonge mbele tu, make kwa taasisi nyingi kwa sasa kukopesa kilimo sio rahisi, na Benki ya TIB ni usanii full, unaweza omba mkipo leo ukatoka baada ya miaka miwili,

So songeni mbele na mlichio nacho, kama ni kulima anzeni hata kwa Jembe wakuu inawezekana, au anzeni kidogo na kile mnacho ona k=hakitatumia pesa nyingi, mfano kufuga hao kuku manweza Komaa na ufugaji wa Kuku na baada ya mwakna Na nusu mnaweza kuwa na pesa ya Kutosha kufadhili kilimo chenu, au basi kwenye hayo mashamba muone kama mnaweza lima mazao ya muda mfupi kama Nyanya na kazalika ili mtengeneze mtaji wa kulima Mpunga,

Kwa ishu ya Mikopo kwa kweli tatizo ila haliwezi kuwa ndo sababu ya kuto kusonga Mbele, nendeni na kile mlicho nacho, mko wa tano limeni hata kwa jembe la mkono hata kama mtalima Robe heka au nusu heka bado ni hatua kubwa sana,

Na kama mna hadi Mashine na baadhi ya Mipira anzeni na mlicho nacho na hiyo mikopo inaweza kuwakuta tiyali msha anza safari na mko Robo, kwa sababu mikopo ki kitu kinachukua Process ndefu sana teana mikopo ya kilimo ndo kabisa,

Mmesema mko Bunda? Naomba Connection kati ya Halimashauri ya wilaya ya Bunda na Dodoma vijijini, make mmesema mko Dodoma na mkopo mmeomba Bunda ambao ni mkoa wa Mara.

Nashani hawa ni wanachuo wa chuo cha MIPANGO - MWANZA BRANCH kama sijakosea na wala sio DODOMA - IRDP.

Nawapongeza sana wadogo zangu kwa initiative mlizo nazo, big up.

Cha kufanya,
Mnaweza kwenda kwa mkurugenzi wa wilaya ili awasaidie akikataa kuwaweka kwenye budget basi mwandikie barua mkuu wa mkoa na mumpe kopy mkuu wa wilaya na mkurugenzi wake, mkishindwa nendeni mbele mpaka wizarani na kumbukeni kuandika barua na kuwapa kopy hao ambao walishindwa kuwasaidia, ili badae msije mkalaumiwa. wizara ikishindwa nendeni ikulu kabisa mkapige kambi pale kwa JK atawasikiliza tu, maana kuna vijana niliona kawasaidia ma-trekta na baadhi ya pembejeo.

Hakuna linaloshindikana if u decide to dare.

Big up vijana wadogo zangu hii ni changamoto kwa vijana wa vyuo vingine
 
wakuu, aksanten sana kwa ushaurini wenu na kututia moyo....hakika tutaufanyia kazi, wakati mwingine msaada wa hali huwa ni mzuri kuliko wa mali.....kuhusu chuo, sisi tulisoma chuo cha mipango ya maendeleo vijijini, dodoma, campus ya miyuji...ila wilaya ya bunda, jimbo la mwibara ndilo eneo letu la uwekezaji...
 
Mwibara si ndo kwa Yule mheshimiwa wa Magamba ambaye alisaini form za Zito za kumtimua Pinda? Ok nikija Serengeti nitajitahidi nije huko kuwaona na tunaweza Ongea something
 
Back
Top Bottom