Tunaobeza harakati za Mbowe na wenzake

Mzizi wa hoja ni kuwa baadhi yetu tunashajiisha VIOLENCE APPROACH....

Nimepokea masahihisho...
Kama hiyo violence approach inaweza kuondoa ccm madarakani , chama kilicholeta kila aina ya dhiki nchini Tanzania , basi tutaitumia , hii ni kwa sababu lengo letu ni kuokoa nchi na wananchi , ngoja tuone haya majadiliano kama yataleta Katiba mpya na Tume huru .

Chadema haitakuwa na shida ikiwa itashindwa kwenye uchaguzi huru na haki , lakini hatutakuwa na Mswalie Mtume ikiwa tutashindwa kwa Hila za Dr Mahera na Mamluki wenzake wa ccm , hata kama wameshika bunduki .

Nakili hii post yangu .

HAKI HUINUA TAIFA
 
Mzizi wa hoja ni kuwa baadhi yetu tunashajiisha VIOLENCE APPROACH....

Nimepokea masahihisho...

..hivi kati ya Ccm na wapinzani ni upande gani uko more violent than the other?

..tuwakemee wale wanaoumiza, na kutesa wenzao, badala ya kulaumu wanyonge wanaoteswa na kudhulumiwa kwasababu ya mitizamo yao ya kisiasa.
 
'…Wanataka tufanye nao mazungumzo ya maridhiano …maridhiano na mtu ambae hajakiri makosa yake, mtu ambae hajakiri alikosea wapi?…over my dead body…'


Walisikika Makamanda hapo zamani za kale wiki chache zilizopita


sasa hivi hata Zitto akipost anacheza Mziki anavamiwa na Matusi kuwa anawacheka wao

Hasira za Lema zinamuishia Zitto hadi kasingizia ndio yupo Nyuma ya Mgogoro wa NCCR wakati tunajua alie katika kati ya Mgogoro ni Mbunge wao wa zamani wa Rombo Bw.Selasini


mjifunze kupunguza mihemko na ushabiki lila sehemu


Freeman Mbowe ni Mjanja sana na anajua kucheza game za kisiasa kibongo bongo


kawastua kidogo na uamuzi wa kuwatimua kina Halima hapo hapo akaingia kwny Mazungumzo kwa lugha rahisi kauma akapuliza akalamba asali
 
Kuna mijitu mijinga kama Martini ambayo wala kwenye chama hawajulikani ila ndo leo kupitia mitandao wanataka kushika ajenda za chadema. Uhuni mtupu
 
Kuna mijitu mijinga kama Martini ambayo wala kwenye chama hawajulikani ila ndo leo kupitia mitandao wanataka kushika ajenda za chadema. Uhuni mtupu
Majadiliano yanajenga zaidi na naamini yataza matunda
 
Naomba mfano wa hivi karibuni wa NCHI ILIYOTUMIA VIOLENCE APPROACH wakashika dola na nchi ikakaa SAWA!!!!

Ukisharuhusu VIOLENCE ndiyo wakati wa Mabepari kuwaweka watakaokidhi matakwa yao na WAO KUCHUKUA RASILIMALI ZA NCHI BILA HATA HIYO MIKATABA YA KINYONYAJI...

Sana watasaidia lila upande ili kukoleza Moto vizuri.... Tutapewa silaha ili tuuane vizuri.... HAPO NDIYO ITAKUWA "LAITI TUNGE......"

Tusapoti nia MHE. RAIS NA MWENYEKITI MBOWE....... Mama ni msikivu, tumuunge mkono atatuvusha SALAMA!!!!

Kikao cha Jana IKULU ni mwanzo Mzuri.....
 
Tuwaunge mkono ni mwanzo mzuri na unaweza kufungua njia!!!
 

Hii porojo ni kama porojo nyingine tu, na hazijaanza leo…. hamjawahi kushindwa uchaguzi huru na kwa haki.

Hamtoshi kushika dola japo huwa mnajiapiza kuiondoa CCM madarakani kwa namna yoyote, ila hamna maandalizi toshelevu…. hakuna wananchi wataounga mkono hiyo unayoita violence approach.
 
Zote hizi ni juhudi za kurejesha amani na kujenga utulivu wa nchi ambao uliharibiwa na taira wa chato.

Huyu Mama anakazi kubwa Sana kurejesha mahusiano na nchi nyingine sio Jambo dogo maana tulikua tumejitebga kabisa, Tanzania tulianza kubaguana kivyama na hii sumu ilimea haswa kwa akili ya kawaida ilikua inatufikisha wapi Kama sio kuanza kuuana.

So kwa huyu Mama haya alio yafanya ni makubwa mno zaidi.

Watanzania Tumshukuru Sana Mwenyezi Mungu kwa kutuondolea yule mzee.
 
Pohamba, si vema kufikia uamuzi huo. Wote hatujui contents za vikao hadi sasa. Huenda moja ya contents ni kuwa taka wakiri na Kuja public kuomba msamaha. Kwa hiyo tuwape muda. Subira yavuta heri japo vijana nyie ni maji ya moto. Sema pia uongozi wa Chadema usichukue muda sana angalau kurudi ku formalize haya majadiliano kichama na kutoa roadmap yake ieleweke kuzuia taharuki inayojijenga Sasa
 
Wanaobeza ni wale waliokuwa wanafaidika na siasa za chuki zilizoanzishwa na mwendakuzimu
 
Upo sahihi,ila kuhusu Mh.Lissu,Lema& wengine walioikimbia nchi siyo wa kuwalaumu kwa wanayoyafanya kuendeleza struggle,wasingekimbia tusingekuwa nao leo(It was very dangerous for them) na kauli zao afterwards zimesaidia sana katika kuwezesha uwepo wa mazungumzo yanayoendelea.Hoja zao zimewasaidia Watanzania wengi kufahamu mengi(Awareness to the public) na watawala wameanza kukutana na pumzi ya moto wa madai ya Katiba Mpya.
 

..machafuko yote hutokea kwasababu ya ukandamizaji wa vyama tawala dhidi ya vyama mbadala.


..hakuna hata nchi.moja ambako vyama mbadala vili-resort to violence bila kuwa vimejaribu siasa za amani na ikashindikana.

..machafuko na mauaji ya kimbari ya Rwanda yalifanywa na vijana wa chama tawala. Na chanzo chake ni chama tawala kukataa kuweka usawa kati yake na wapinzani / minorities.

..Genocide ya Wayahudi wa Ulaya iliongozwa na kuasisiwa na chama tawala cha Ujerumani. Ubabe wa chama hicho ulipelekea mpaka kutokea kwa vita kuu ya pili ya dunia.

..Libya nako hadithi ni.ileile. Muamar Gaddafi alimpindua Mfalme, lakini baada ya miaka kadhaa madarakani akajigeuza Mfalme wa Libya. Gaddafi aliua wanasiasa wengi akiwemo mtu wake wa karibu kabisa Major.Jaloud.

..Matokeo ya ukandamizaji wa Gaddafi ni vita iliyoisambaratisha Libya. Gaddafi alipaswa kuwa mwerevu kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi ili kuwezesha mabadilko ya serikali kupitia sanduku la kura.

..Kwa hapa Tanzania Ccm.kuna matukio mengi ya ukatili yaliyoelekezwa kwa vyama mbadala. Ni.muhimu kuyalaani matendo hayo. Pia ni.muhimu waliohusika wachukuliwe hatua.

..Maridhiano yanakwenda sambamba na kuambizana ukweli wa jinsi tulivyokoseana na kuumizana.
 

Umesema vizuri LAKINI KUNA KITU UNAKOSEA.. Huwezi kulinganisha kilichofuatia baada ya utawala wa Gaddafi na maisha baada ya hilo VUGUVUGU HILO....

Kuna msingi Mkuu wa kufanya MAAMUZI hasa kwenye mambo ya Kijamii; FAIDA NA HASARA AMBAZO JAMII ITAPATA KUTOKANA NA MAAMUZI HAYO...

Wanasiasa wengi huangalia fursa ya kwenda IKULU na sii faida au HASARA ambayo jamii kwa ujumla ITAPATA....

BINAFSI siungi mkono kabisa VIOLENCE kwa sababu inawezekana ukamtoa ambaye unaamini ni CHUI ikulu UKAMWINGIZA simba....

Tupiganie DIALOGUE na daima TUPINGE kila anayeshajiisha VURUGU...

KUSEMA NINKWEPESI SANA.... inawezekana kabisa HISTORIA ikamwandika vizuri GADAFFI kwa siku zijazo kuliko WALIOASISI HAYO MAANDAMANO LIBYA
 

..tunakosea.

..chanzo cha machafuko ni wale walioko ktk ikulu zetu na wenye miliki ya vyombo vya dola na mahakama.

..hawa ndio huanza kutumia mabavu dhidi ya vyama mbadala au wale wenye mitizamo tofauti.

..matokeo yake ni jamii kukosa imani na njia za amani kuleta mabadiliko na hivyo kuiga ukatili wa watawala na walioko ikulu.

..hapa Tanzania Ccm tumeshaona muelekeo mbaya wa kikatili wa Ccm dhidi ya vyama vya upinzani.

..Tunatakiwa tuwakemee Ccm kwani wao ndio wenye mamlaka na silaha and have a record of acting violent and irresponsible.

..Tunatakiwa tuwatambue na kuwalaani wote waliohusika na ukatili dhidi ya wapinzani.

..Tukifanya hivyo tutakuwa tumechora mstari kwamba dhuluma na ukatili havina nafasi ktk siasa za Tanzania.

..Tuwatambue na kuwaunga mkono wote walio ktk harakati za kutetea haki, usawa, na demokrasia, ktk nchi yetu.

..Ni lazima tujenge utamaduni wa kuheshimu utu, haki, usawa, demokrasia. Tukifanya hivyo tutakuwa tumejihakikishia amani na maendeleo.

NB:

..Chanzo na mzizi wa machafuko ya Libya ni ukatili na udhalimu wa Muamar Gaddafi.

..Kwa upande wetu Watz, sisi wenye umri mkubwa tunamkumbuka Gaddafi jinsi alivyoungana na Iddi Amin kutupiga vita.
 
Werevu wametoka CHADEMA wamebaki wajinga wajinga tu na werevu wachache waliomua kukaa kimya.
 
Naomba kuwasilisha wanajamvi... critical arguments zinajenga na kuonesha ukomavu wa kifikra zaidi kuliko mapovu, matusi na kejeli ambazo mara nyingi huoneshi ukosefu wa uzoefu au muono hafifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…