Tunaofunga Kwaresma hii tukutane hapa

Niwatakie Kwaresima njema wote tutaonana after Easter.

Muombe Mungu ufunge kwa maombi hata kama ni kushukuru tu sio lazma iwe shida au Tatizo.

Punguza matumiz ya ile anasa unayoipenda sana ikiwezekana iache kabisa...

Jitahid kuweza kutofautisha ushindaji na njaa na kufunga, Pia usigeuze kwaresima kama diet plan yako hilo halitakua lengo la kwaresima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi sijaungama dhambi miaka saba iliyopita, kesho naanza kujiungamisha mwenyewe na mpaka Kwaresma inaisha nitakuwa nimeiepuka Jehanam. Halafu naangalia kanisa lenye kabati nzuri ya kuungamia nimalize mchezo.
 
Itabidi nifunge kwaresma mwaka huu

Nitaanza siku ya kwanza mpaka mwisho

ugumu ni uzi wa kula tunda kimasihara je nitaweza kuupotezea?
[emoji3][emoji3]utaeza tu..na njaa yote iyo utawaza sa ngapi tunda
 
Sante sana, ubarikiwe
 
Kufunga sio lazima kuacha kula wandugu, unaweza kufunga kwa kuacha kufanya chochote ulichokizoea na unakipenda sana ambacho unajua hakimpendezi Mungu wetu (hope mnamjua).

Na hali hii ngumu mtu asijeamua kubana matumizi ya msosi kwa kisingizio cha kufunga, hiyo haitakuwa kwaresma, kufunga kwa mkristu sio kufunga kwa mazoea, unafunga kula tu, NO. Funga kwa kuacha kile unachokipenda sana na kitakutoa jasho kweli kukiacha, huo ndio mfungo.

Vitu kama kubeti, kutoa lugha za hovyo kwa wengine (matusi), kusengenya/ umbea, kuna vitu vingi km hivyo ambavyo tumevizoea sana ndio vyakuacha.

Kwaresma ni kubadilika mpaka jirani yako aone mfano toka kwako, sio kuacha kula mchana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mbona Kama unataka ligi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kasema hapa mambo ya kuacha kula?
 
Kipindi hichi cha mfungo kwaresma ukiwa kwenye ibada hii ya mfungo je unaruhusiwa kuwasilana na mpenzi wako? Mimi ni muislam lakini nina mpenzi kesho anategemea kufunga nataka nifahamu mipaka yangu kwake yeye kwa kipindi hichi chote akiwa kwenye mfungo
 
Asante mkuu maana kuna shughuli zitanibana mitaa hiyo hadi saa 10 hivyo itabidi nisali hapo nashukuru.
Pamoja sana mkuu! Utakuwa muda mwafaka sana ukimaliza hiyo saa 10 unaunga moja kwa moja kwenda kanisani. Inaonesha ni jinsi gani ulivyo Mkatoliki halisi, ubarikiwe sana na uwe na mfungo mwema!
 
Kwaresma ni kipindi cha kutafakari zaidi juu ya maisha yetu na uhusiano wetu na Mungu. Tujitahid tufanye toba na tuwe watu wa sala ili tuwe chumvi kwa wenzetu[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie watu wa Mungu ambae kesho mnategemea kufunga nimewauliza swali hapo juu lakini mpo kimya acheni uchoyo wa kuto kutoa elimu huo ni ubaguzi
 
Aaaah, mkuu Kumbe ni wewe ndiye unatugegedea dada zetu? Ndiyo maana hata Mimi niliwagongea Swalhina wenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…