DOKEZO Responded Tunaohitimu VETA, Kozi ya Forklift Operator tunahitimu hatujui kitu sababu Forklift yenyewe ni mbovu

DOKEZO Responded Tunaohitimu VETA, Kozi ya Forklift Operator tunahitimu hatujui kitu sababu Forklift yenyewe ni mbovu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Forklift .jpeg
Mimi ni muhitimu wa kozi fupi ya Forklift Operator katika Chuo cha Veta Chango’mbe Dar es Salam Mwaka 2025, pale kuna changamoto nyingi zinazosababisha watu wanahitimu wakiwa hawapo fiti, ni kama wanaendaenda tu katika hiyo kozi.

Kwanza kabisa Forklift iliyopo ni mbovu kupitiliza, inazima kila wakati na ni ya kizamani, kwahiyo unaweza kwenda pale kwa siku na usijifunze, ikabatika kuwaka tu.

Wanafunzi wapo wengi so kila mtu anaendesha kama dakika 3 tu, unaenda nyumbani, pili Mwalimu mwenyewe anakuwa na kozi 4 kwa siku anafundisha magari madogo, magari makubwa, magari ya abiria ndiyo anakuja kumalizia na nyie wa Forklift.

Unatoka pale ujui kitu hadi kupata kazi inakuwa changamoto kwasababu Forklift mbovu na hujifunzi kwa usahihi.

Kwahiyo anakuwa kachoka, yaani ni kama mnajifundisha tu halafu vyeti vyenyewe vinachelewa kutoka mpaka usubiri miezi mitatu, unasoma kozi ya mwezi mmoja kisha cheti kukipata inachukua miezi mitatu.

Pia, wanabatia ya kukosea majina ya wanafunzi makusudi ukienda kuchukua cheti jina limekosewa unalipa hela tena ya kubadilisha jina.

Ufafanuzi wa VETA ~ VETA: Forklift iliyopata hitilafu imerekebishwa, ni jambo la kawaida Vyombo vya Moto na mashine kupata hitilafu
 
Matapeli hao, ss mtu hujui kuendasha gari unaenda hapo unakuta hilo li fork haliwaki teena. Si unakuwa hujui kitu kbs jamani.
 
Back
Top Bottom