Tunaoingia kazini zamu za usiku tupeane uzoefu na vioja tunavyopitia

Tunaoingia kazini zamu za usiku tupeane uzoefu na vioja tunavyopitia

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Sikuwahi kuwa interested na kazi za usiku ni vile tu upepo wa maisha ndo umenifanya nijikute nipo huku na kadri siku zinavyoenda najikuta naanza kuenjoy kufanya kazi usiku na yote haya ni kwa sababu.

1. Napata muda wa kutosha kupumzika na kufanya mishe zangu.

2. Nature ya kazi zetu kama una mpango wa kando kazini lazima uone usiku mfupi.

3. Mara nyingi usiku panakuwa hamna kazi nzito ni kama kwenda tu kuonekana eneo la kazi.

4. Kuna Uhuru mkubwa kutokana na mabosi wengi hawana tamaduni za kuja usiku kazini

5. Mishe haramu za usiku zinazokufanya urudi na chochote kwa mama watoto.

Changamoto.

1. Usingizi ni changamoto kubwa maana kampuni nyingine ni kosa linaloweza kupelekea kusimamishwa kazi.

2. Kumuacha wife peke yake geto maana kuna mabazazi utumia hiyo kama fursa.

3. Wizi

4. Baridi Kali na sehemu ya kutulia Mimi eneo langu la kazi ni mapori kila sehemu utakayogusa ni umande.

5. Kujaribiwa kichawi.

Ila yote kwa yote nipende kutoa shukrani kwa mwenyezi mungu kwa kunipatia kazi maana na Mimi nakatwa na NSSF Kikotoo kinanihusu uzeeni.
 
Changamoto zipo nyingi kulingana na kazi yako kwa mfano askari kulinda usiku ukiwa na silaha kwanza unakuwa na hofu hata mwenzio humwamini hata ukienda chooni unaingia naisilaha lako alafu mbu wanang'ata sana unaogopa hata kusinzia alafu kama umepangwa lindo la ofisi kuu kuna viroja usiku wakati mwingine unaona kabisa taa inawaka na kuzimwa kama kuna mtu kumbe laa ni mizimu tuu
 
wa stendi,
Mbu ni baraa lingine kama kipindi cha mvua ni challenge kubwa kimsingi tunaofanya kazi usiku tunastahili pongezi nyingi sema waajiri wengine wanachukulia poa kiasi kwamba ikitokea hitilafu yoyote kimbilio lao ni kukupeleka kituoni.
 
Hicho kituo cha kazi..kama indicator vile [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kweli kabisa na kuandikishwa maelezo[emoji2][emoji2]
Mbu ni baraa lingine kama kipindi cha mvua ni challenge kubwa kimsingi tunaofanya kazi usiku tunastahili pongezi nyingi sema waajiri wengine wanachukulia poa kiasi kwamba ikitokea hitilafu yoyote kimbilio lao ni kukupeleka kituoni.
 
Kazi za usiku changamoto Sana aise, mbu, usingizi, mvua, walozi, na vifaa !!

Nilipo huku daah tunapiga kazi at least group la watu 12 Hadi 22 Sasa mgawanyiko unapotokea hapo Ni kufata ishara na maelekezo tu Maana unaweza jikuta matatizoni !!

Mvua nayo tabu, afu Ni lazima uwe makini muda wowote chochote kinatokea, kosa moja linaweza gharimu maisha au ikawa kirema
 
Madaktari, wauguzi, wafamasia, wataalamu wa maabara wa hospitali ni kitu cha kawaida sana kuingia shift za usiku

Unforgetable
Kweli ila hao wana ufadhali sababu wanawekewa walinzi na kama hospital kuna vitanda na net kwa kifupi ni kuwa hawana cha kupoteza mziki unakuja kwa sisi walinzi.
 
Back
Top Bottom