Tunaojiandaa kuishangilia Kesho Simba SC ikicheza na Singida United tujiandae Kisaikolojia

Tunaojiandaa kuishangilia Kesho Simba SC ikicheza na Singida United tujiandae Kisaikolojia

TABIRI ZISIZO ZA KISAYANSI, HUHUSISHA SANA, WATU WASHIRIKINA.
 
Kutabir si kazi ya binadamu, mungu ndiye hutabiri, hivo ni rahis kujua kama kwako yupo au VIP
 
Ukisikia kwenda chaka ndo uku a level tulkua tuna sema jomba kaenda OP
 
Kweli nimeamini kuna Watu ni Mangumbaru / Wajinga sana na hii thread pia imenisaidia kuwajua. Katika sentensi yangu tu ya mwanzo nimesema na kuweka tahadhari mapema mno kwamba hata hivyo Mimi nimetabiri tu / nimefanya nujum yangu ila mwenye kujua kama Simba SC leo ingeshinda ni Maulana / Mwenyezi Mungu peke yake na bahati nzuri Simba SC imeibuka na ushindi tayari ' Mijitu ' imekurupuka huko ilikotoka na kuanza kunilaumu huku ikisahau kwamba Mimi nimetabiri tu na sijasema nina uhakika na matokeo hayo kwa 100%.

Najua kuna ' Mijitu ' mingine ' mipuuzi ' ambayo sasa hivi inajifanya kunichukia kwa huu uzi wangu kwasababu tu iliamini kuwa ndivyo itakuwa na ' ikabeti ' na sasa ' mikeka ' yao imechanika ndiyo hasira zao zote inajifanya kuhamishia Kwangu. Sikumlazimisha Mtu aamini nilichokisema / kukitabiri na kama kuna ambao mnadhani huwa nabahatisha tu jaribuni kutafuta humu humu uzi wa mechi ya Simba na Yanga ya mwaka jana ambayo nilitabiri hivi hivi na katika mechi ile 99% ya nilichokitabiri kilitokea na Watu wengi humu walinipongeza pia.

Kama kweli mnajua kubisha au mlikuwa mna uhakika kwamba ' nujum / tabiri ' yangu ilikuwa ' magumashi ' mbona hamkujitokeza mapema kunikatalia na kunidhihaki lakini mlivyo ' Minafiki ' mmesubiria hadi mechi imeisha Simba SC imeshinda ndiyo mnajifanya kuleta ' mipua ' yenu na kujifanya kunilaumu / kunidhihaki.

Hopeless wakubwa!

Cc: moyes, Jmujun, Nahonyo, sikonjose, Bwana Mapesa, ijoz, kelao, King Ngwaba
 
Ila mimi hata hiyo mwakajana Sijakupongeza, Kwa Sababu siamini katika tabiri za Kienyeji. Nitakuunga mkono baadhi ya Maeneo sio katika tabili zako, Ingawa wewe ni ndugu yangu wa Karibu tu.
 
Mengineyo namuachia Mwenyezi Mungu kwani Yeye ndiye kila kitu hivyo kama akiamua Simba SC tutashinda sawa itakuwa hivyo lakini kutokana na ' nujum ' zangu ( namaanisha tabiri zangu ) za hadi muda huu natiririka na naserereka na huu uzi ni kwamba matokeo ya Kesho ya mechi ya Simba SC na Singida United ni kama yafuatayo:

Simba SC 0 - Singida United 0


au


Simba SC 1 - Singida United 1


au


Simba SC 0 - Singida United 1


au


Simba SC 1 - Singida United 2

Na kama haitoshi kutakuwa pia na Kadi Nyekundu katika moja ya Timu.

Wana Simba SC wenzangu chonde chonde Kesho tuanze kujiandaa Kisaikolojia na msije kusema sikuwatahadharisheni mapema kisha baada ya mechi tukasikia tena kuna Wapenzi / Mashabiki wa Simba SC wamefariki dunia kwa ' mshtuko ' wa matokeo.

Tuonane Kesho Saa 11 na dakika 55 au Saa 12 Kamili jioni ili tuulizane zaidi juu ya ' nujum ' zangu hizo hapo juu.

Kila la kheri.

Nawasilisha.
Next time jikaze wewe !!
 
Back
Top Bottom