Tunaokula ugoro tukutane hapa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Wale wana JF tunaotupia dawa(kamchongo) tujuane haPa.huu hapa Kuna jamaa yangu kanikeletea kutoka kigamboni Ni mkali balaa.napenda kaudongo kale ambacho kana moisture kwa mbali sio Kama huu wa Masai wa buguruni mkavu Sana halafu hauna vibe ukiuweka unaanza kusambaa mdomoni... hii kitu ikikunasa Ni noma unaweza kujikuta unaumwa kumbe kisa umekosa hii kitu ya kwa bibi sometimes huwa nashikwa arosto kinyama so nikiamka tu asubuhi break ya kwanza kwa Masai.nilianza kula ugoro baada ya kugundua unakata hamu ya kuvuta sigara na pia unaleta njaa halafu mi kipindi Hiko nilikuwa Sina appetite kabisa ilinibist nianze kutumia.sasa hivi nimeshakuwa addicted nao.
 

Hivi polisi akikukamata na hii kitu anakusweka lupango au hii sio kesi kama ilivyo bhange na miraa mkuu...?
 
Hivi polisi akikukamata na hii kitu anakusweka lupango au hii sio kesi kama ilivyo bhange na miraa mkuu...?
Wanakataza lakini Sasa polisi wengi na wenyewe wanatupia hii kitu so akikukamata anakuomba anakuchukulia kidogo anakwambia fureshi tembea
 
Wanakataza lakini Sasa polisi wengi na wenyewe wanatupia hii kitu so akikukamata anakuomba anakuchukulia kidogo anakwambia fureshi tembea

Unamaanisha polisi akiwa anatumia bhange akikukuta na bhange ndo atakuacha mkuu...?

Hawa jamaa sio wa kuwaamini kihivyo, ukikutana na asiyetumia ugolo na akakukuta nao inakuaje...?
 
Nakumbuka kipindi hicho 1998 nikiwa mdogo Nilichukua kikopo cha Bibi (babycare)cha kuhifadhia hili zaga.nikaanza kupikapika Kama ugali huku nikichanganyia na udongo,ebanaeeeeh,alinikamata akanilisha Kama vidole 3,kilochotokea!!!πŸ™ƒπŸ™ƒπŸ™ƒπŸ’€πŸ’€πŸ’€πŸ’€
 
ugoro ulinikataa kabisa...
~hasa pale kutematema mate kama nyoka
~kunuka ugoro full time
~mkojo mwekundu na unanuka kinyama
~kuumwa kifua
~hasira hasira yaani ilitawala
~kula kwa kujificha,tofauti hata na bhaghe
~macho kuwa mekundu
~mwili kukosa nguvu na kuwa mchovu mchovu zaidi
~nguo na shuka zakulalia na kushindia kunuka goro
~na stimu yake inakufanya nzutu
~kuumwa kichwa haswaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…