KERO Tunaomba Chuo cha IFM kusikia kilio chetu kuhusu baadhi ya Walimu wanavyokosa huruma kwa Wanafunzi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), nikiwa katika mwaka wa pili wa masomo. Naomba kutoa malalamiko yangu kuhusu mwenendo wa mmoja wa wahadhiri wetu, ambaye kwa mtazamo wangu amekuwa akituletea changamoto kubwa sisi wanafunzi, hasa katika masuala ya ufundishaji na tathmini.

Kwa heshima, naomba mhadhiri huyu apunguze ukali na namna ya kushughulika na wanafunzi. Wapo wanafunzi ambao wamekuwa wakihisi kutotendewa kwa haki wanapokataa baadhi ya matakwa binafsi ya mhadhiri, na baadhi yao wanaona hali hiyo inaweza kuathiri namna wanavyopata alama au kufanya vizuri katika masomo.

Jambo hili limekuwa likileta hofu na kukosekana kwa amani miongoni mwa wanafunzi, kwa sababu nafasi aliyonayo mhadhiri inafanya baadhi ya wanafunzi kushindwa kuzungumza kwa uhuru au kulalamika wanapohisi kuna changamoto.

Kwa upande wa wanafunzi wa kike, kuna malalamiko kwamba baadhi yao wamewahi kukutana na mazingira yasiyowafanya wajisikie salama au huru katika mahusiano yao ya kitaaluma na mhadhiri huyo. Hili ni jambo linalohitaji kuchunguzwa kwa umakini na mamlaka husika ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayenyanyaswa, kutishwa au kuathiriwa kitaaluma kwa sababu ya kukataa jambo lisilohusiana na masomo.

Mwaka huu wa pili, hususan katika muhula wa kwanza, tumepitia changamoto ambazo zimetuumiza sana kama wanafunzi. Tunaomba uongozi wa chuo usikilize malalamiko haya, uwape wanafunzi nafasi salama ya kueleza uzoefu wao na, inapobidi, ufanye uchunguzi wa haki na wa siri kuhusu tuhuma zinazotolewa.

Hatupingi mhadhiri kuwa na mamlaka darasani, lakini tunasisitiza kuwa mamlaka hayo yatumiwe kwa weledi, haki na heshima kwa wanafunzi. Cheo au nafasi ya kazi isiwe sababu ya mwanafunzi kuogopa kutoa malalamiko au kudai haki yake ya kitaaluma.

Naomba suala hili lifanyiwe kazi kwa busara na kwa wakati, kwa lengo la kulinda ustawi wa wanafunzi na kuhakikisha mazingira ya chuo yanakuwa salama, yenye haki na rafiki kwa kila mwanafunzi.

Tunaomba uongozi usikie kilio cha wanafunzi na uchukue hatua stahiki.
 
Mbona umeaema kama chuo kina muhadhiri mmoja tu ambaye ni yy?

1. Taja anafundisha somo gani?
2. Taja somo analofundisha
3. Taja jinsia yake
4. Ainusha ukali au mambo binafsi anayohitaj i.e rushwa ya pesa au ngono.... etc
 
Kibacha madogo piga shule sasa ingekuwa enzi zetu za LUTASHOBYA UDSM SI MGEKIMBIA ?
 
Back
Top Bottom