KERO Tunaomba Halotel iboreshe huduma ya mtandao Zanzibar, imekuwa ni changamoto sana

KERO Tunaomba Halotel iboreshe huduma ya mtandao Zanzibar, imekuwa ni changamoto sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mohamedi24

Member
Joined
Dec 3, 2024
Posts
5
Reaction score
2
Mimi ni mdau wa JamiiForums ninayeishi Zanzibar, Mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Magharibi B. Nimekuwa mtumiaji wa mtandao wa Halotel kwa takribani miaka minane sasa, lakini kwa muda mrefu nimekuwa nikikumbana na changamoto ya upatikanaji wa huduma katika baadhi ya maeneo.

Nikitoka Mkoa wa Mjini Magharibi kuelekea Mkoa wa Kaskazini, mtandao wa Halotel mara nyingi haupatikani kabisa. Nilipowasiliana na huduma kwa wateja, niliambiwa huenda tatizo likawa kwenye simu yangu. Nilibadilisha simu na kununua mpya, lakini tatizo bado limeendelea.

Leo, nimetoka eneo ninapoishi na kusafiri takribani kilomita 20 tu, lakini huduma ya Halotel haikupatikana.

Tunaomba Halotel iboreshe miundombinu na huduma zake ili mtandao upatikane kwa uhakika katika maeneo yote ya Zanzibar na nchini kwa ujumla. Changamoto hii inatukwaza sana sisi wateja ambao tumekuwa tukiamini na kutumia huduma zenu kwa muda mrefu.

Tunaomba mtuchukulie hatua na kuboresha huduma zenu. Tumechoka kukosa mtandao katika maeneo mbalimbali.

markup_1000315656.png
markup_1000315673.png
 
Back
Top Bottom