Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili (undergraduate) Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili (MUHAS). Naomba kuwasilisha changamoto zinazotukabili wanafunzi wa programu tofauti na Udaktari wa Binadamu (MD) na Sayansi ya Maabara (BMLS), katika kufanya mitihani ya kozi ya Microbiology.
Kozi hii imekuwa chanzo cha msongo wa mawazo na hofu ya kitaaluma kwa baadhi yetu kutokana na
1. Mitihani kutokuzingatia mahitaji ya programu husika, malalamiko yetu ni mitihani haiendani kikamilifu na yaliyofundishwa na mahitaji mahususi ya programu zetu, Hali hii inasababisha wasiwasi kuhusu haki na usawa katika tathmini ya wanafunzi.
2. Changamoto katika ufaulu wa wanafunzi; Kumekuwa na tatizo la idadi kubwa ya wanafunzi wanaopata mitihani ya marudio (supplementary examinations) kila mwaka. Tunaomba Idara iweke mikakati ya kuboresha ufundishaji ili tuweze kufaulu.
3. Mabadiliko ya Ratiba Nje ya Utaratibu; Idara imekuwa ikibadilisha ratiba za mitihani na kuziendesha nje ya ratiba rasmi ya chuo, jambo linalovuruga maandalizi yetu katika mitihani hiyo.
Tunaiomba Idara ya Microbiology kuangalia upya mfumo wake wa ufundishaji na utungaji wa mitihani kwa kuzingatia mahitaji mahususi ya kila kozi wakati wa kuandaa mitihani, ili itathmini kile kilichofundishwa darasani.
Pia kuheshimu na kufuata ratiba rasmi za chuo ili kutufanya tuwe maandalizi ya kutosha na utulivu wa kiakili