KERO Tunaomba mfumo wa NACTVET ufunguliwe, Wanafunzi wengi Chuo cha Mipango Mwanza tumeshindwa kukamilisha usajili

KERO Tunaomba mfumo wa NACTVET ufunguliwe, Wanafunzi wengi Chuo cha Mipango Mwanza tumeshindwa kukamilisha usajili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wanafunzi wengi katika Chuo cha Mipango, Kanda ya Ziwa, tumeshindwa kukamilisha usajili wa kuendelea na masomo kutokana na changamoto zinazosababishwa na mfumo wa NACTVET.

Tunaomba Serikali na mamlaka husika kuingilia kati na kufungua tena mfumo huo kwa angalau wiki moja, ili tuweze kukamilisha usajili wetu. Tuna hofu kuwa kundi kubwa la wanafunzi litakosa fursa ya kuendelea na masomo kutokana na changamoto hiyo.

Tunaomba mamlaka husika zisikilize kilio hiki na kutafuta suluhisho la haraka, kwani kuchelewa kwa usajili kunahatarisha ndoto na malengo ya wanafunzi wengi ya kupata elimu. Tunaiomba Serikali itusaidie ili tusipoteze fursa ya kuendelea na masomo kutokana na changamoto hii ya kimfumo.
 
Back
Top Bottom