Mr Equalizer
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 611
- 727
Wana jamvi kwanza nawapongeza kwa kumaliza vizuri mwezi wa ramadhani.Lakini kwa baadhi yatu sisi Walimu sikukuu hii imekuwa si ya furaha kwani mpaka sasa hivi hatujapata mishahara yetu, wakati wenzetu wamepata tangu tarehe 25. Kwa kweli tumesikitika sana ukizingatia tunaishi mazingira magumu sana huku vijijini ambako serikali imejenga shule za Kata. Huku hatuna maji, umeme, hata net work ya kutuwezesha kuwasiliana na ndugu zetu haipo .Tukiwauliza watendaji wa halmashari nao wanasema hawajui kilichotokea hatuna mtu wa kutusaidia. Serikali kuu iko mbali sana na sisi.Tunapenda sana kuitumikia serikali lakini hii imetukatisha tamaa kabisa.