tunaomba serikali ilipe mishahara ya walimu wote mwezi huu

tunaomba serikali ilipe mishahara ya walimu wote mwezi huu

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Wana jamvi kwanza nawapongeza kwa kumaliza vizuri mwezi wa ramadhani.Lakini kwa baadhi yatu sisi Walimu sikukuu hii imekuwa si ya furaha kwani mpaka sasa hivi hatujapata mishahara yetu, wakati wenzetu wamepata tangu tarehe 25. Kwa kweli tumesikitika sana ukizingatia tunaishi mazingira magumu sana huku vijijini ambako serikali imejenga shule za Kata. Huku hatuna maji, umeme, hata net work ya kutuwezesha kuwasiliana na ndugu zetu haipo .Tukiwauliza watendaji wa halmashari nao wanasema hawajui kilichotokea hatuna mtu wa kutusaidia. Serikali kuu iko mbali sana na sisi.Tunapenda sana kuitumikia serikali lakini hii imetukatisha tamaa kabisa.
 
Pole sana ndugu hii ndiyo CCM,wanajenga shule kisiasa alafu wanashindwa kuwalipa walimu stahiki zao.
 
POLE SANA Mkuu!
Dah, ila kweli JF ni noma, inapatikana bila hata ya network!!!!!!
 
Uko benki gani Mwalimu?Nmb toka Jmosi niliona misururu mirefu
 
Kwanza kabisa pole na pili mimi ni mhanga wa hili jambo kama ww ila sisi wenzenu ktk halmashauri yetu jana tulijiorganize na tumefika halmashauri tukaambiwa kulikua na tatizo la acount number za bnk na cheque imetumwa toka hazina tukahakiki pale tunangoja sikukuu ipite tuwekewe chetu watendaji wa halmashauri lazma wana majibu labda hamjawa serious
 
Ubabaishaji unamwisho, walimu badilikeni mkasirike kiakili... or else utawala dhalimu wa chama x utawauwa!
 
Back
Top Bottom