Tunaomba Wanasheria wa kututetea wananchi wa Kata ya Nyatwali wanaohamishwa kwa malipo kiduchu

Tunaomba Wanasheria wa kututetea wananchi wa Kata ya Nyatwali wanaohamishwa kwa malipo kiduchu

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Serikali imeamua kuwahamisha wananchi wa Vijiji vya Kata ya Nyatwali ili kuongeza ukubwa Hifadhi ya Wanyama - Serengeti.

Wakati wa uhai wa Mhe. Magufuli pendekezo hili alilikataa kata kata na sisi wananchi tulifurahi na kumshukuru Mungu.

Ilipoingia utawala wa Awamu ya Sita jambo hilil lilianzishwa upya kwa kasi kubwa na uamuzi ukafikiwa kuwa wananchi wahame.

Uhakiki wa mali zote katika eneo hilo umefanyika ikiwa ni pamoja na kila mwananchi kuelezwa kiasi cha mali zake na kutakiwa kuweka sahihi.

Tatizo limekuja pale wananchi wanapopunjwa malipo yao. Mfano ekari moja ya ardhi mwananchi analipwa Tshs.2,000,000 kinyume na makubaliano ya hapo awali ya Tshs.4,000,000.

Unapoenda kuweka sahihi unashurutishwa kusaini na kutishwa kuwa hata ukikataa utafanya nini mbele ya Serikali.

Tunawaomba Wanasheria wapenda haki wajitokeze kututetea kwa uonevu unaotakiwa kufanywa na Serikali. Mhe. Tundu Lissu, Wakili msomi Kibatala, Wakili msomi Mallya, Wakili msomi Mtobesya mko wapi njooni mtutetee sisi wananchi wanyonge.
 
Pisheni pori tengefu, Heche hatowasaidia lolote.
 
Write your reply...BORA NYIE SISI TUNATOLEWA BILA FIDIA NA KESI IKO MAHAKAMANI NA WALA SERIKALI HAIJALI.
 
Back
Top Bottom