Tunaombeni mrudisheni fast Jet ya kipato rafiki kwa Mtanzania, Air Tanzania sio huduma ya kijamii ni huduma ya Watanzania wachache matawi ya juu

Tunaombeni mrudisheni fast Jet ya kipato rafiki kwa Mtanzania, Air Tanzania sio huduma ya kijamii ni huduma ya Watanzania wachache matawi ya juu

Kama walikuwa nafuu kiasi hicho, kwa nini haikwenda Kenya au Uganda au Rwanda hata Burundi basi. Tuna umbumbumbu Watanzania
Fastjet Haikuondoka Tanzania Kwakupenda Ila Mzilankende Aliwaagiza Tanzania Aviation Authority
Kitowaongezea Muda Wa Vibari Ya Kufanya Kazi Hapa Nchini
Lengo Hasa Likiwa Wanataka Kupanda Ndege Wapande Air Tanzania

Tena Maelekezo Yalitoka Wazi Kiongozi Wa Serikali Akipanda Fastjet Achukuliwe Hatua Chap


Kwahiyo Fastjet Wakakosa Kibari Cha Miruko Hapa Tanzania Ikawa Ni Lazima Waondoke
Ndiyo Wakaenda Nchi Zingine, Laurence Masha Anawatazama Tu
 
Then walikuwa kwa vipofu. Iweje washindwe kwenda huko kwingine kama issue ni unafuu wa tiketi? Haya masoko ya watu masikini tofauti yao nini?
Fafanua hoja yako.

Kwamba Kampuni imeona soko lipo Tanzania, inapofukuzwa unataka iende Kenya au Uganda ambako tangu Mwanzo haikuona kama kuna soko!!!???ikuwa kwa bipifu
 
Kenya sio Tz kuna competition kali sana makampuni ni mengi, muda huo Jumbo jet ndio ilikuwa imekamata zaidi Kenya.

Strategy ya fastjet ilikuwa kutengeneza himaya kwenye nchi zenye huduma mbovu za ndege, enzi hizo kabla hajafika air Tanzania kulikuwa na kero kibao akaona aje hapa kutake advantage

Rwanda na Burundi nchi ndogo hizo zinakaribiana na mkoa wa Mwanza, safari nyingi kwa basi unafika kwa muda

Fast jet waliweza kwenda Zimbabwe pia
Vipi Nigeria? Kenya Jambojet hakuweza kuwa low cost hata robo!
 
Then walikuwa kwa vipofu. Iweje washindwe kwenda huko kwingine kama issue ni unafuu wa tiketi? Haya masoko ya watu masikini tofauti yao nini?
Soko hutawaliwa na mambo mengi. hapa ni machache ya kuangalia.

1. Bidhaa unayouza huko unakotaka kwenda kuipeleka sokoni hakuna bidhaa kama hiyo?

2. Washindani wako kwenye soko wana nguvu kiasi gani. unaweza kuwapiku?

3. Kipindi cha mpito tangu kuanzisha biashara mpaka kufanikiwa unao mtaji wa kutosha?

4. Sheria za biashara kwenye eneo unalotaka kuwekeza zikoje. Ni rafiki?

5. Idadi ya wateja itaifanya biashara yako iwe endelevu?

Sasa mimi siyo mtaalam wa biashara ya mambo ya Anga (Aviation business) kwa ivo kujua mazingira ya biashara Kenya na Uganda yalikuwaje wakati Fast Jet wanaondoka Tanzania siwezi kujua.
 
Ile ilikuwa budget airline, hivyo hata kama bei ingepanda bado ingekuwa nafuu yani isingeweza kulingana na atcl
Ndege za ATC zilinunuliwa kwa "Cash Payment in full" kwa ivo mzigo wa kurudisha gharama za ununuzi ulikuwa mkubwa sana.

Fast Jet zilikuwa ndege zilizokodiwa, wanalipana kwa kadri ya biashara kutokana na mapatano yao. Sasa lazima moja bei iwe imechangamka kidogo.
 
Ndege za ATC zilinunuliwa kwa "Cash Payment in full" kwa ivo mzigo wa kurudisha gharama za ununuzi ulikuwa mkubwa sana.

Fast Jet zilikuwa ndege zilizokodiwa, wanalipana kwa kadri ya biashara kutokana na mapatano yao. Sasa lazima moja bei iwe imechangamka kidogo.
Hatujakataa swala la wao kununua kwa cash inabidi warudishe faida, ila walitakiwa waziache fastjet ziendelee na biashara ili kila mtu achague kupanda anayopenda

Nchi ina watu zaidi ya mil 65 hao Atcl watawamaliza wote?? Pia huduma zao haziridhishi huenda wangebadilika kama wangekuwa na mpinzani thabiti
 
Hatujakataa swala la wao kununua kwa cash inabidi warudishe faida, ila walitakiwa waziache fastjet ziendelee na biashara ili kila mtu achague kupanda anayopenda

Nchi ina watu zaidi ya mil 65 hao Atcl watawamaliza wote?? Pia huduma zao haziridhishi huenda wangebadilika kama wangekuwa na mpinzani thabiti
Fastjet angekuwa na mafanikio asingwachia madeni makubwa watoa huduma na wafanyakazi wake. Low cost au operating on forward sales haiwezi kuwa endelevu kwenye soko lenye gharama za uendeshaji kubwa kama Afrika. Ndege ya kukodi haina utani na malipo ya mkopo! Nigeria ina uchumi mkubwa hapa Afrika na population ya kutosha, mbona hakuenda huko? Download financial statements zake uone hali aliyokuwa nayo
 
Fast jet niliipanda dar mwanza kuwahi Dem wangu aliyekuwa amechumbiwa na tajiri wa madini wa Kahama.

Nilipofika saa6 mchana nikamwambia Dem anisubirie nimalizie chuo nimuoe. Nikaenda kumjaza kwanza na saa 12 jioni akanisindikiza airport mwanza nikareje mzizima Kwa nauli ya 96,000/= nilikata wiki tatu kabla.

Nikatibua ndoa ya watu. Huyo nesi Hadi siku ya kiama akienda kumlai bwana atanikumbuka kama nipo kuume Kwa baba. Kuna kipindi nilimpandisha mwewe huo wa jet Kwa sh 43,000 akaenda fildi huko mwanza.


RIP my mchumba JG na mwanetu uliyeenda nae tumboni.
Bodaboda hazifai.
 
S
Fafanua hoja yako.

Kwamba Kampuni imeona soko lipo Tanzania, inapofukuzwa unataka iende Kenya au Uganda ambako tangu Mwanzo haikuona kama kuna soko!!!???
Wanaweka Siasa ndn ya biashara. Wenyewe hawakua wakipata asara, mnawakimbiza, mnaanzisha zenu za gharama ghali lkn mnaishia kututangazia mabilioni ya hasara halafu tuchekelee kw kua ni letu!? Itachukua muda kupata maendeleo ...dah!
 

Kwa furaha kubwa sana kipindi cha Uncle Magu niliipongeza serikali kwa kuanza kuleta ndege mpya za air Tanzania nikiamini ya kwamba ushindani dhidi ya fastjet utaongezeka nasi abiria tunufaike zaidi.

sikumbuki vizuri kilichotokea lakini fastjet waliondoka akabaki air Tanzania peke yake kama ndege kuu, hata hivyo sikufa moyo nilidhani tutaendelea kupanda air Tanzania kwa nauli kama za fastjet ama pungufu zaidi, kinyume na nilichofikiria mambo yakawa tofauti kabisa mpaka leo, kupanda air Tanzania ni ghali hata kwa watanzania middle class,

Fastjet tuliweza kupanda kwa elf 70 mpaka laki Dsm kwenda Kia (Moshi / Arusha), iliweza kupata sifa ya kuwa huduma ya kijamii, tuliweza kujionea hata safari za Dsm Mbeya zinajaa

Enzi hizo hata ushamba wa ndege watu wengi waliutoa, Nauli Mbeya hadi Dar kwa basi elf 40, fastjet elf 70 unaona heri uongeze miekundu mitatu upande mwewe

Air Taanzania wanaoweza ku afford ni matawi ya juu wale kina upper middle class na kuendelea, wengine wakipanda labda iwe emergency
Na bado hamjasema. Tuliwaambia Dikteta amekurupuka mkasema bi mbeba maono.

Maono ya kipumbavu ndiyo haya. Yeye amekufa na mliobaki hamuwezi ku afford airticket ya Dar- KIA.

Hakuna national airlines zinazopata faida kwa Africa labda Ethiopian Airlines pekee. Hawa KQ na SAA wamekuwa wakiripoti hasara for the last 3 years.

Kutegemea kuwa utapata mapato kutoka ATCL ambayo utayaelekeza kwenye ujenzi wa shule na mabarabara sahau kabisa.

Ni sekta binafsi tu ndiyo zinafanikiwa kufanya biashara ya ndege au sekta mchanganyiko wa Serikali kidogo na Binafsi sehemu kubwa

Ila Magufuli alifanikiwa kuwa BRAINWASH Watanzania, pamoja na kuwaingiza mkenge bado mnamuita shujaa.
 
Ilikuwa roho mbaya tu kuondolewa

Alitegemea Air Tz itafanya vizuri badala yake ikawa kila hasara tunaambiwa inaleta faida

Ila bora wangerudishwa tu

Au kwani hao wanaoiba mabilioni si waanzishe shirika lao tu
Mnasema ilikuwa roho mbaya. Hao waliopo sasa wenye roho nzuri mbona hawajairudisha?
 
Kama walikuwa nafuu kiasi hicho, kwa nini haikwenda Kenya au Uganda au Rwanda hata Burundi basi. Tuna umbumbumbu Watanzania
Wapo Zimbabwe 🇿🇼 wana chapa kazi, Ebu wafatilie huko utupe mrejesho
 
Back
Top Bottom