Uchaguzi 2020 Tunaoona mbali tulionya jambo hili halina siha kwa ustawi wa Taifa

Jiwe kapanic hovyo hovyooo.Anamlazimisha mama janeth kuomba kura.Mama wa watu hata hajui kuongea
 

Ule mpango haukuwa na faida kwa CCM ni kweli, Jee ulikuwa na faida kwetu Chadema? kama haukuwa na faida kwa CCM na ulileta hasara kwa Chadema.

Basi moja kwa moja CCM walifaidika kwa kuleta Udhaifu wa kimapato kwa Chadema kwa sababu RUZUKU inategemea sana idadi ya wabunge ulio nao.
 
  1. Je, umerahisisha kampeni?
  2. Tuliowanunua watarudi?
  3. Tumependwa zaidi?
Kwanza ulifanya utia nia kuwa mgumu zaidi maana wana-ccm wengi walikuja kwa hasira zaidi. Pili, mliowanunua sio lazima kurudi maana hawana chao. Tatu, idadi ya waliowachukia ccm imeongezeka maradufu. Kazi kwenu.
 
Wagombea uraisi wawili waliyoitikisa CCM ambao ni Lowasa na Slaa ambao ndiyo ilikuwa tegemeo la cdm walinunuliwa kwa kupewa kazi na kupewa ahadi ya kulindiwa mali zao. Hivyo hiyo ilitoa taswila sahihi ya cdm kuwa shida yao ni pesa na si vinginevyo
Shida ya Chadema ni pesa ? CCM shida yao ni mawe ? Bumbaaav
 

Hii kauli ya kukua kwa upinzani, naomba uirudie baada ya tarehe 29th October, 2020.
 

hakuna maneno ya cdm yanayoaminika katika hii nchi, kama wapinzani walinunuliwa basi ina maana chama chenu ni kibovu sasa hamna watu wenye msimamo, unfortunately ndo economics ya dunia ilivo, any super nation wanatumia pesa kuwadanganya maraisi wa afrika then watu wanakubali sasa kwa kua na nyie mmeshaonyesha kwa vitendo then probably you cant rule because pesa inawanunua, ingawa hakuna sehem mtu amenunuliwa but kutumia mfano wako then chama chenu ni cha kipumbavu sana kwenye pesa

mara hatutaki ndege alafu aliesema nae anapanda ndege! WTF
 
Huo ulikuwa mnada wa watumwa katika karne hii.
Umetia dosari chama cha mapinduzi kufanya biashara haramu ya binadamu,nje ya utaratibu wetu wa kuchagua wawakilishi wetu kwa nguvu ya hoja kila miaka 5,labda kifo,incapacitated, au kukiuka sheria za Jamhuri.

Hata wajumbe wafia chama wamehoji kwenye Halmashauri Kuu mantiki ya kuleta malaya wa kisiasa na athari zake.

Lakini navyo vyama vya upinzani vimekaa kimya au kutoa majibu mepesi,bila kuwachukulia hatua ya kisheria viongozi wa CCM kwa kula njama za kuwarubuni na kununua viongozi wapinzani.

Wapinzani wanao ushahidi wa maneno ya Humphrey Polepole akihamazisha manunuzi ya wabunge,madiwani wa upinzani,akiwafananisha dirisha dogo la usajiri.

Ndio sababu wapiga kura watasita kupigia kura upinzani kwa kutokuwa na uhakika ya huyo mbunge au diwani kukimbia chama baada ya kuchaguliwa.
 
Wakudadavua na TandaleOne njooni huku mjibu
 
Mission imefeli vibaya mnoo ..na kati ya vitu ccm wanajutia ni huu ununuzi wa madiwani na wabunge kutoka upinzani ..umefeli kwa [emoji817]%
Kila biashara ina faida na hasara.

Muhimu tu wale madiwani wamepiga pesa za bure.
 
Mimi Nina lugha moja rahisi Dana.Hao walimshauri vibaya m.kiti wajipange,kwani haha ni matokeo ya ushauri wao mbaya.
 
Mkuu utaumiza ubongo wako bure kujibizana na mazezeta ya Lumumba. Mada inaongelea kingine lenyewe linakuja kuharibu kabisa.
 
upinzani ndo kwanza umepakwa mafuta. Nilishasemaga humu kuwa upinzani sio Mbowe, Lissu wala Zitto. Hata ukiwaua wote hao upinzani utakuwa palepale. maana upinzani uko kwenye nyoyo za watu. Kila mtu anaepata riziki yake kwa taabu sana ni mpinzani, kila mtu asiyekuwa na ajira ni mpinzani, kila mtu aliyeonewa na chombo cha serikali ni mpinzani, kila mtu asiyekuwa na chakula, maji, umeme, shamba, ajira ni mpinzani.
 
Walifungia vyama pinzani visifanye siasa wakidhani wameua upinzani kumbe ndo wametia petrol kwenye tanulu la moto. Tulieni tuwafurushe Ikulu
 
Kama kuna mpango uliopangwa kindezi huu ulikuwa mmojawapo na hasara zake zitazidi kuonekana siku za usoni.
Bado na matokeo ya kura za maoni nayo yatazidisha upana wa kovu na kutia ndimu kwenye donda!!
 
Mna gubu nyie loh

Kisa ni hasira za kutoungwa mkono na wananchi huko kwenye kampeni zenu
 
Jiwe kapanic hovyo hovyooo.Anamlazimisha mama janeth kuomba kura.Mama wa watu hata hajui kuongea
Mama Janet Aliitwa Aonekane...
Mama Janet Aliitwa ASALIMIE...

Hakuambiwa aombe KURA....Bali alimuombea kura.....
 
Hahaha mimi kinachonifurahisha Rais Magufuli alipiga kampeni tangu 2015 hadi leo 2020 hajamaliza , sijui apewe muda gani ili wananchi wamuelewe!?
 

Hiyo leseni ya kuuza nchi inakatwa wapi ili tukawakatie CDM nao waiuze nchi? Acheni ubinafsi wa kuiuza nchi peke yenu. Tuko kwenye ulimwengu wa biashara huria kila mtu anaruhusiwa kuiuza nchi yake. Last time niliangalia serikali ya CCM mlishaiuza nchi kwa kuingia katika mikataba ya miaka 100 ya unyonyaji wa madini. Teh teh!
 

Mmiliki wa huo mpango ni yeye mwenyewe Rais, turejee alipoingia tu madarakani akawatoa awatoako Dr.Bashiru na Polepole na kuwaleta kwenye chama na kuwapa uongozi wa juu kabisa kwenye chama, hawa hawajawahi kuwa wana CCM iweje waletwe tu na kupewa uongozi hapo hapo?

Huo wa kununua wapinzani ni mwendelezo alioufanya toka mwanzo ndani ya chama, akiamini anafagia masalia ya wana CCM wa zamani na kujenga chama chake ndani ya CCM, hii yote ni kujitengenezea uhakika wa kutokupingwa. Binafsi huwa najiuliza na sipati majibu kwanini huyu mtu anaogopa sana kupingwa, hajawahi kuwa muumini wa siasa za ushindani, ndio maana kwa kununua wabunge na madiwani wa upinzani alijua uchaguzi huu hakutakuwa na mpinzani hata mmoja, Meza imepinduka hehe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…