Tunaopinga maamuzi ya Rais kuhusu jiji la DSM tulitaka afanyeje?

Tunaopinga maamuzi ya Rais kuhusu jiji la DSM tulitaka afanyeje?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Wakuu Mimi chombo changu kikuu na pekee cha habari ni mitandao ya kijamii. Sio gazeti, radio wala TV. Kwa sababu huku napata habari isiyoghoshiwa (Censored) kwa kiasi fulani. Sasa nimepotea kidogo tu nakutana na malalamiko mengi sana kuhusu Ilala kuwa jiji, kuhusu maamuzi aliyofanya Mkuu wetu.

Ila kwa haraka nikatafuta anayetoa mbadala kuwa alipaswa afanye nini ambacho hajafanya kwenye maamuzi hayo sijaona.

Sasa unadhani amekosea nini na alipaswa kufanya nini ili tuungane kupinga na kushangaa maamuzi.

Au ni kelele tu za mitandaoni maana siku hizi ni kama Sifa au ujiko hivi kupinga kila anachofanya Mkuu.
 
Binafsi sijaelewa kilichofanyika. Wataalamu wa TAMISEMI naomba mnifafanulie.


JESUS IS LORD!
 
 
Anajua mwenyewe na uongozi wake, angesema anabomoa majengo ya dsm yote na kuhamishia watu chatto ndo tungepinga ila kama vipo mambo safi tuu
 
Nimeelewa hadi nimesikitika.
Kwa nini hakufanya hivyo 2015.
Au Wapinzani wangetishia kumpeleka ICC hahaha
 
Anajua mwenyewe na uongozi wake, angesema anabomoa majengo ya dsm yote na kuhamishia watu chatto ndo tungepinga ila kama vipo mambo safi tuu
Mambo yako vizuri.
Shortcut ya kumpongeza kama unaona aibu ni kuibua uozo mwingine ili aushughulikie.

Kupinga kwingine hata mapepo yanasikitika, maana yanaona unataka kuyazidi viwango
 
Yeye huyu haelewi nini kinaendelea kiukweli hili suala wengi hawajui nimewasikiliza hata watangazaji wengi kwenye radio wwanaruka ruka tu hakuna anayeelewa
Ndio maana nauliza. Sielewi kabisa Mkuu.
Hongera kwa kunigundua MAPEMA.
Fafanua kwa Faida yangu na wasioelewa wenzangu.
 
Sijui hata wanapinga nini, hii itapunguza msongamano, na kuongeza kipato cha jiji ambayo itapelekea kujengwa kwa miundo mbinu mikubwa yenye kiwango cha kimataifa.
 
Hii ina uhusiano wowote na kuongeza uwigo wa ukusanyaji wa mapato?
 
Kwangu mimi sababu ni Raisi sio unatoa maamuzi tu..., Shirikisha wadau mwisho wa siku maamuzi yawe ya wataalamu / wadau (na yeye akiwa mdau) haya mambo ya kuweka precedent kwamba maamuzi ya mtu mmoja ni sawa kesho keshokutwa atakuja chizi wa kutuamulia vitu vya ajabu ajabu..

Kuamua aamue ila maamuzi yawe shirikishi, yeye kazi kubwa iwe ni kusimamia na kuhakikisha hayo maamuzi shirikishi yanafanyika.
 
Back
Top Bottom