Tunaopinga maamuzi ya Rais kuhusu jiji la DSM tulitaka afanyeje?

Tunaopinga maamuzi ya Rais kuhusu jiji la DSM tulitaka afanyeje?

Mimi ni "layman" tu ila nafikiri hivi

1) Hakuna eneo lolote la utawala linaloitwa "Dar es Salaam", as such, Manispaa ya Jiji la Dar es Salaam ilikuwa kama hewa.

2) Vyanzo vya mapato vya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam vilikuwa kama vile vimekwapuliwa kutoka eneo jingine ambako nako kuna Manispaa, na hivyo kuleta mikwaruzano ya chini kwa chini.

3) Kulikuwa na staff wengi ambao wengine labda walikuwa hawaeleweki wanafanya nini haswa. Kulikuwa na watu ambao walikuwa wanashika nafasi mbili unnecessarily (mfano mayor wa Ubungo huyo huyo anakuwa mayor wa Jiji la Dar Es Salaam).

4) Kofia ya Jiji sasa inavaliwa na Ilala. Yaani ilala sasa ni kama kiranja mkuu wa Manispaa za Dar

Ambalo bado silielewi vizuri ni hii ya Manispaa ya Ilala "kupandishwa" hadhi na kuwa Manispaa ya Jiji la Dar es Salaam. Hii maana yake nini? Tunaua "Jiji la Dar" na kuanzisha/kulibadilisha Jina Manispaa ya Ilala kuwa Jiji?

Watu wa Ubungo, Temeke etc maslahi yao kama wakazi wa Dar es Salaam nani atayaangalia? Majukumu ya iliyokuwa Jiji la Dar yanahamia kwa Mkuu wa Mkoa au inakuwaje? Horizon ya Ilala amabayo sasa ni "Jiji" ina expand beyond mipaka ya Ilala, meaning Manispaa ya Ilala ipo ila imemezwa na Jiji kama ilivyo Tanganyika ndani ya Tanzania?
 
Wakuu Mimi chombo changu kikuu na pekeecha habari ni mitandao ya kijamii. Sio gazeti, radio wala TV. Kwa sababu huku napata habari isiyoghoshiwa (Censored) kwa kiasi flani. Sasa nimepotea kidogo tu nakutana na malalamiko mengi sana kuhusu ilala kuwa jiji, kuhusu maamuzi aliyofanya Mkuu wetu...
Sawa tu kilichofanyika.
 
Nilitaka a-deal na hao waliokuwa watendaji wa jiji la Dsm aliosema ni wazembe hawakai ofisini, wanakula pesa za bure, sasa alivyohamishia huko Ilala nao wakiwa wazembe atahamishia hilo jiji Temeke au Kinondoni?

Amekurupuka alitakiwa atulie kidogo kwanza afanye consultation ya kutosha na watendaji wake kabla ya kuja na huu uamuzi, naamini Rais ajaye anaweza kabisa kuu-revoke.
 
Nilichoelewa mimi ni kuwa huyu kaja kuvuruga kila kitu kavuruga mahusiano ya nchi yetu na nchi nyingine ,kavuruga biashara , kavuruga mfumo wa elimu , kavuruga ajira. Na sasa kaamia huku . tuendelee kumuombea tu amalize shughuri yake basi .
 
Wakuu Mimi chombo changu kikuu na pekee cha habari ni mitandao ya kijamii. Sio gazeti, radio wala TV. Kwa sababu huku napata habari isiyoghoshiwa (Censored) kwa kiasi flani. Sasa nimepotea kidogo tu nakutana na malalamiko mengi sana kuhusu Ilala kuwa jiji, kuhusu maamuzi aliyofanya Mkuu wetu..
Kwanza sentensi yako ya mwisho inaonyesha kwamba huhitaji maoni bali unashangaa wanaopinga yanayofanywa na viongozi wa chama chako. Ukihitaji maoni subiri wakupe maoni na siyo kuwaambia kwamba watu wanawapigia makelele viongozi wako.

Kwanza utawala wa kaya hii chini ya chama chako umeharibu kabisa mfumo stahiki wa uongozi wa serikali za mitaa. Ukweli ni kwamba serikali za mitaa ni mamlaka kabisa ndani ya nchi na wizara inayohusika na serikali za mitaa, hapa kwetu TAMISEMI inapaswa iwe chini ya ofisi ya Waziri Mkuu maana ndiye mwenye jukumu la kuzisimamia serikali za mitaa kwa ukaribu na huwa na waziri mwenye dhamana ya kuisimamia wizara hiyo na kutekeleza serikali na kanuni zote zinazoongoza Serikali za mitaa.

Cha ajabu hapa Tanzania TAMISEMI imepelekwa ofisini kwa Rais ambaye ni msimamizi mkuu wa Serikali Kuu na Ofisi ya Rais ni Serikali kuu. Hapa mgawanyo wa madaraka umevurugwa. Haiwezekani leo Rais wa nchi ambaye ni Muhimili wa Serikali Kuu ndiye anaamua na kushughulikia mambo ya serikali za mitaa. Hiki ni kituko cha Karne. Sasa waziri wa TAMISEMI ana kazi gani? Halmashauri zote za miji na Majiji zinapaswa ziwe chini ya mamalaka ya TAMISEMI na siyo IKULU.

Waziri wa TAMISEMI ndiye alipaswa kufanya hayo yanayofanywa na huyo jamaa.
 
Hii itakuwa na Faida gani ukilinganisha na hicho alichokifanya.

Maana lazima tujue
Swali lako la "angefanyeje tofauti na alivyofanya" halina maana wala mantiki...

Ni sawa na wewe uje kwangu uamue kubadili jina langu kibabe na uamue kunipa jina jipya "Mtunduizi" badala ya "The Palm Tree" kisha wewe huyohuyo watu wakilalamika na kukuuliza mbona unambadili jina huyo? Jibu lako linakuwa rahisi tu, ktk muundo wa swali la "..kwani mngetaka nifanyeje...?"

Jibu hili obviously, hali - make sense kabisa, right..? Ndivyo ulivyo wewe kupitia hoja yako hii uliyoiposti humu na sasa tunajadili...

Hata hivyo, ni vyema ukafahamu jambo hili muhimu sana, kuwa, kutofautiana kimawazo na kimitazamo ktk jambo lolote ni jambo la kawaida kwa binadamu...

Ndo naweza kusema kuwa, wewe unayekubaliana na maamuzi ya Rais Magufuli, tushawishi na sisi wengine kwa kueleza sababu tangible zilizomsukuma Rais kuchukua maamuzi haya....!!
 
Wakuu Mimi chombo changu kikuu na pekee cha habari ni mitandao ya kijamii. Sio gazeti, radio wala TV. Kwa sababu huku napata habari isiyoghoshiwa (Censored) kwa kiasi flani. Sasa nimepotea kidogo tu nakutana na malalamiko mengi sana kuhusu Ilala kuwa jiji, kuhusu maamuzi aliyofanya Mkuu wetu...
Tunauzoefu naye huwa anafanya mambo kwa kukurupuka si umeona mlivyohamia dodoma., kule wenzetu huweka plan kwanza na kuangalia challenges/benefits hapa ni ukiamka tu asubuhi ilala itakuwa jiji kuanzia sasa badala ya manispaa.

Yako mambo mengi ya kudeal na nchi na very sensitive kwa sasa lakini hamjayapa kipaumbele mfano sasaiv corona mumekataa tiba za wataalamu ambayo nchi mbali mbali ulimwenguni wameafiki.

Tumeambiwa nchi ina madaktari bingwa lakini na wao wamekuja na wazo lile lile na kupiga nyungu tu, ukiwauliza nani alipona kwa nyungu hawana data, kila mtu sasa anaishi kivyake, watu hawajui wachukue tahadhari kwa kiwango gani. No updates
 
Nilichoelewa mimi ni kuwa huyu kaja kuvuruga kila kitu kavuruga mahusiano ya nchi yetu na nchi nyingine ,kavuruga biashara , kavuruga mfumo wa elimu , kavuruga ajira. Na sasa kaamia huku . tuendelee kumuombea tu amalize shughuri yake basi .
Kweli huyu ni mvurugaji tu hakuna lingine. Kwanza nashangaa anaingilia mamlaka ya serikali za Mitaa ambayo kwa kweli inapaswa kuwa chini ya TAMISEMI ndani ya ofisi ya waziri Mkuu. Yeye yupo Serikali kuu na ndio Mamlaka yake.

Ni kuvuruga tu na kuwasimanga wafanyakazi kana kwamba hao wafanyakazi wa lililokuwa jiji ndio walileta huo muundo. Kwanza yeye ndio amekuja kuvuruga kila kitu. Hivi nani kamshauri afanye hivyo. Kwani mkoa wa Dar es Salaam umekufa na kuzaliwa mkoa wa Ilala?
 
Nilichoelewa mimi ni kuwa huyu kaja kuvuruga kila kitu kavuruga mahusiano ya nchi yetu na nchi nyingine ,kavuruga biashara , kavuruga mfumo wa elimu , kavuruga ajira. Na sasa kaamia huku . tuendelee kumuombea tu amalize shughuri yake basi .
Kwa lugha rahisi, Jiwe ni Kivuruge.

Ana roho mbovu ya Uharibifu, hajawahi kugusa sehemu halafu ISIHARIBIKE.
 
Ndio maana nauliza. Sielewi kabisa Mkuu.
Hongera kwa kunigundua MAPEMA.
Fafanua kwa Faida yangu na wasioelewa wenzangu.
Hata mie bandugu sielewi kitu. Sielewi faida na hasara ya hatua hii. Kuvunja H/mashauri ya jiji na kuunda H/mashauri ya Ilala.
 
Ni vyema tukubaliane kutokukubaliana, hii ndio demokrasia. Ila mie nakubaliana na Raisi wangu kwa 100% japo kishingo upande.
 
Mimi ni "layman" tu ila nafikiri hivi

1) Hakuna eneo lolote la utawala linaloitwa "Dar es Salaam", as such, Manispaa ya Jiji la Dar es Salaam ilikuwa kama hewa...
Vuruuuuuuuu. It leaves much to be desired and very many unanswered questions.
 
Mzee katwambia Madiwani wa Dar es Salaam wanakula fedha za bure kabisa wakati hawakuchaguliwa na watu. Twambieni hawa madiwani ambao miongoni mwao ndio mameya walichaguliwa na nani?
 
Huku kwenye mitandao hata kama ni muelewa ni sifa kujitoa ufahamu na kulaumu tu!
Wakuu Mimi chombo changu kikuu na pekee cha habari ni mitandao ya kijamii. Sio gazeti, radio wala TV. Kwa sababu huku napata habari isiyoghoshiwa (Censored) kwa kiasi flani. Sasa nimepotea kidogo tu nakutana na malalamiko mengi sana kuhusu Ilala kuwa jiji, kuhusu maamuzi aliyofanya Mkuu wetu....
 
Wakuu Mimi chombo changu kikuu na pekee cha habari ni mitandao ya kijamii. Sio gazeti, radio wala TV. Kwa sababu huku napata habari isiyoghoshiwa (Censored) kwa kiasi flani. Sasa nimepotea kidogo tu nakutana na malalamiko mengi sana kuhusu Ilala kuwa jiji, kuhusu maamuzi aliyofanya Mkuu wetu...
Kwa kuwa tatizo la Meko ni gharama za Jiji la DAR ambalo halina ardhi, miradi wala mapato, napendekeza angefanya yafuatayo:

1. Angeacha set up iliyopo ya manispaa iendelee na pengine wazidi kuongeza manispaa zingine kama Mbagala, Pugu, Bunju. Hapa hata ile principle ya D by D (Development by Devolution) ingezidi kuwa practical.

2. Wale Mameya wa Manispaa hizo ndiyo wainde Baraza la Jiji. Kama watakuwa watano Kama zilivyo Manispaa za sasa sawa. Halafu watamchagua Mayor miongini mwao

3. Watakuwa na Sekretariati ya watu wasiozidi 5 (Katibu, Afisa Mipango, Mjasibu, Dreva, Katibu Muhtasi) ambao ndiyo watafanya kazi za uratibu

4. Concept ya wilaya ingefutwa tusiwe na ma DC kwa kuwa zile shughuli za DCs ziunganishwe kwa DEDs tu.

5. Gharama za kuendesha Sekretariati ya Jiji zitachangiwa kwa njia ya asilimia au kwa rotation ya Halmashauri moja kwa mzunguko wa mwaka mmoja mmoja

6. Ma Mayor wa kila Manispaa kupitia ma DED wao watatengeneza mipango yao na kuipitisha kwenye Halmashauri zao na Kisha zitapata endorsement ya Baraza la Jiji.

NB:
Hii ndiyo setup ya South Africa ambapo Manispaa za Soweto, Hilbrough, Kempton Park, Sandton, Randeburg, Rodeport zinasababisha JIJI moja maarufu kabisa duniani la Johannesburg

Faida za Approach Hii:
1. Ile concept ya Development by Devolution (DbD) itatekelezwa vizuri

2. Jiji la Dar es Salaam halitapoteza muendelezo wake na historia yake

3. Kutakuwa hakuna kupishana kwa mipango na maenseleo ya JIJI la Dar kwa vile mipango ya manispaa zote inaratibiwa sehemu moja

4. Kwa sasa tuna population ikadiriwayo 6 Milion. Hivyo basi tukifika mwaka 2030 Ni rahisi kuwa Mega City kwa vile population ya Jiji itafika 10 Milion
.
 
Back
Top Bottom