Tunaosubiri namba E tukutane hapa

Namba D is here to stay kwa kweli. Natabiri inaweza kufika 2023 na bado DZ inawa mezani [emoji1]
DY bado magari kama elfu 20 hivi hadi iishe na ushuru umekuwa mkubwa na russia kakiwakisha itachelewa. DZ yenyewe ina magari 23,400 hadi iishe ndo ije namba E. Dawa ni kununua namba binafsi weka jina lako then ikitoka E hamia.
 
Sasa awekese 22m aje apate faida ya 3m mmmmh huoni hapo faida kidogo Ila anategemea mzunguko
 
DY bado magari kama elfu 20 hivi hadi iishe na ushuru umekuwa mkubwa na russia kakiwakisha itachelewa. DZ yenyewe ina magari 23,400 hadi iishe ndo ije namba E. Dawa ni kununua namba binafsi weka jina lako then ikitoka E hamia.
Hata unapoweka no binafs bado no ya kawaida inakuwepo mdau. Sema unabadilishiwa plate no tu
 
Japokuwa hujaniuliza mimi ila nakwambia ukweli registration series ya magari ni factor kubwa katika kuporomoka kwa bei ya gari husika. Tulio kwenye industry tunajua
Haelewi huyo!

Ngoja wazee wa Mlimani city waingie mchezoni mwa namba β€œE” ukipeleka gari hata iwe bado kinanda utaskia hii gari tatizo β€œD” number mkuu! Hii tukupe million 7 tu!

Yani hamna mtu atakuwa na interest na gari yenye namba β€œD” tena. Zitaporomoka bei vibaya mno hasa β€œD” za mwanzo zile! Bora hawa wa DZ wanaweza kuuza uza maana E ikishika kasi watu β€œD” watakuwa hawaitaki tena. Wateja wa magari bongo wako interested na number plate zaidi sio ubora wa gari!
 
Inaanza DYA 101, DYA 102, hadi ifike DYA 999
Then ije DYB 101 had DYB 999
Halafu DYC 101 hadi DYC 999
Kwa mlolongo huo paka uje
Upate namba ya mwisho ya DYZ 999
Ndo uanza na DZA 101
Mkuu kwa taarifa tu tunamaliza DYQ ndani ya siku chache! Kila herufi ni wastani wa week 2 na siku inakuwa ishakata.

Zinafata R,S,T,U,V,W,X,Y,Z maximum projection ukifika mwezi wa 6 namba E itakuwa ishaanza kutembea barabarani!

Kumbuka gari kuna mabasi, Coaster na malori ambayo matajiri hawaagizagi moja moja. Hayo yanakujaga kwa makumi na mamia. Achilia gari binafsi ambazo watu huingiza na kusajili daily.
 
Sasa awekese 22m aje apate faida ya 3m mmmmh huoni hapo faida kidogo Ila anategemea mzunguko
We unafikiri zile gari wanapata faida ya 50/50 mkuu? Una idea kweli na biashara ya magari mkuu?

Ngoja nikupe tip.
Madalali tu wenyewe target huwa ni 300K mpaka 1M akipiga sana ila wengi huishia 500k.

Wenye yards faida yao ni 2M mpaka 3M standard! Mfano IST akiagiza ikamfikia kwa 12M basi yeye atauza 14-15M kwa jinsi gari ilivyo.

Dalali akiingia hapo ndio ataweka 500K yake iwe15.5M ila wengi hawazipendagi gari za hivi sababu hazina faida ya haraka kama used.
 
Mkuu, DZA hadi DZZ umeziacha wapi? Au hiyo utazinunua wewe?
 
Tukubaliane kwanza hizi zinazotajwa hapa (D, E) ni herufi na sio number, kisha tuendelee na mjadala
 
Tukubaliane kwanza hizi zinazotajwa hapa (D, E) ni herufi na sio number, kisha tuendelee na mjadala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…