Tunaosubiri namba E tukutane hapa

Hoja ya meli kuja dar ni hoja dhaifu sana , meli haibebi magari ya kusajiliwa Tanzania pekee, inabeba gari za nchi nyingi, unaeza kuta hizo gari 3000 plus zinazoshuka tunazajili 500,tu , zingine zikasafirishwa au zinanunuliwa na dealers sometimes bond kwa usajili wa baadaye
 
Hivi magari yanayoshuswa dar ila yanaenda nje ya nchi huwa yanaifadisha vipi serikali kimapato?
1 gari yoyote lazima ilipe port chages , serikali inakunja mkwanja
2 Wharfages, bandari lazima ikunje pesa yake
3 Roadtoll hapa tanroad wanakula chao mapema
4, Agency fees , watanzania wenzetu wanapata ajira

So on and so, kiufupi hata meli ije na gari za nje tupu bado serkali inapata mpunga ,
 
July EAA [emoji736]
Bado sana , twaeza fika november , E ni herufi ya tano tu kati ya 24 zinazotumika,( I na O hazitumiki)
Kila herufi inasajili magari 900, kama Tra wanasajili gari 3000 kwa mwezi , maana yake kwa mwezi hardly tunatumia herudi nne, kutoka E hadi Z manaake kuna heerufi 18 , ukigawanya kwa 4 maana yake tutatumia miezi 4 kutoka sasa kufika DZX , na bado tutatumia nusu mwezi kumalizia DYZ na DZZ, hii ni kadirio la chini kabisa na kama kasi hiyo ya kusajili itaendelea , ikitokea imeshuka tunamaliza mwaka huu na D
 
Jamaa akiona meli imeshusha anajua ndinga zote zinaingia barabarani bongo ASAP....
 
Hivi magari yanayoshuswa dar ila yanaenda nje ya nchi huwa yanaifadisha vipi serikali kimapato?
Mkuu...port charges,wharfage etc. Magari 4000 yatahitaji madereva wa kupeleka yanapoenda(short term ajira), huwa wanayafanyia service hapa hapa kabla hayajaondoka, wanananunua triangle,fire extinguishers etc, wataweka mafuta, yaani kuna faida nyingi direct and indirect.
 
Kwa mwezi Tz tunasajili magari kama 3,000 tu bado tuko nyuma sana.
 
Asante kwa majibu.

Pia hata ajira za vijana kuyasafirisha kuyapeleka huko.

Basi tupambane hata magari ya EAC na SADC yote yapitie Dar.
 
Asante mkuu kwa majibu.

Nilikuwa nafahamu port charges na hizo nyingine.

Hiyo ya wharfage ndo nilikuwa sifahamu.
 
Mwaka huu unaweza isha na D.
 
Asante kwa majibu.

Pia hata ajira za vijana kuyasafirisha kuyapeleka huko.

Basi tupambane hata magari ya EAC na SADC yote yapitie Dar.
Ni swala la muda tu , yatapita. Beira ilikuwa inakuja kuipiku Dar port, ila Mozambique wana kiranga ncha machafuko plus language barrier, hata hao wakongo walioanza kuitumia wameingiwa na uoga sasa wamerudi Dar,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…