Tunaosubiri namba E tukutane hapa

..mbanga za kimuhemuhee cha number E zimeanza pungua Sasa...halafu ndai zenyewe za kawaida tu kabisa ..
 
Hebu kabla hatujakimbilia kusubiri namba E tuonyeshane screenshot ya account zetu benki kupitia mobile app za benki. Siyo tunakomenti na watu hawana hela wanasubiri namba E. IST tu sasa hivi showroom millioni 18.
 
Habari wakuu,
Kuna hawa waagiza magari wanaitwa HEDGARS MOTORS niliwapatia pesa ya kuniagizia gari tangu Mwezi wa sita, Ilipofika mwezi wa saba mmiliki wa hiyo ofisi (HEDGAR MSUYA) alipotea hewani na kutokupatikana tena na ofisi wakafunga mpaka hivi sasa bila ya kutoa taarifa zozote kuhusu hela zetu alizochukua kutuagizia magari. Naomba msaada kama kuna yeyote aliye na updates zozote za hii ofisi, au mwenye changamoto kama yangu na hii ofisi. Napokea ushauri kuhusu namna ya kufanya kuhusu hii case.
 

Nitoe pole. Matapeli wameshakuwahi subiri waje kukupa mwongozo
 
Mkuu pole sana, ila ukitaka gari agiza mwenyewe online maswala ya kutumia mawakala utapeli ni mwingi.
 
Huu msala ushawahi nitokea kwa jamaa walijiita magari rahisi na sasa wamebadili jina....

Nililala nao mbele wakanirudishia changu bado kiasi kidogo...


Fungueni file polisi hao jamaa wengi ni matapeli. Msikubali kukaa mezani. Na muende central kabsa sio mnaenda vituo vidogo.


Kingine mjue polisi nao watawala hela ila watawasaidia. Msikubali kwenda mahakamani maana kesi za madai huwa ni ufala. Fanyeni ubangidu tu unamtesa mtu mpaka atoe hela....
 
Watanzania bado wana ujinga mwingi ndo maana wanaibiwa. Mtu anatumia muda mwingi JF, Twitter, Insta, FB ila hajui jinsi ya kutafuta gari Befoward na kuuliza jinsi gani afanye aweze lipia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…