Tunaosubiri namba E tukutane hapa

Tunaosubiri namba E tukutane hapa

Naona watu wanapiga mahesabu ili wajue namba E inatoka lini kwa mashaka kwamba gari za D zitashuka bei. Namba zitakuja zitaondoka gari zitabaki, sasa mtu anaogopa kununua gari kisa namba? Yani ukae bila gari na una matumizi nayo kisa unasubiri namba kweli?
Mahesabu yao si sahii yani gari ishuke thamani zaidi ya nusu kisa kubadilika namba? Hapana kwa kweli hawapo sawa. Kuna gari namba C na inauzwa bei zaidi ya D. Gari unakuta imetunzwa ipo kinanda then uuze bei rahisi kisa unasubiria E.

Mwingine anakuambia sinunui gari mpaka E ifike.... Yani nikae na hela kisa E huyo atakua hana mpango wa kununua gari ila mbwembwe za mitandaoni....
 
Kwani wasiwasi wenu wa D ni nini? Gari hazishuki bei kwa sababu ya namba wakuu, mtu gari yake DYZ kanunua millioni 17 auze kwa millioni 6 kisha kuna namba EAA? Biashara haiko hivyo hata siku moja. Ukiona gari zinauzwa bei hizo ujue zilinunuliwa bei za chini enzi za namba C.
Wewe jidanganye tu na hio Dualis yako DYZ!
Hata ukiifungia kabatini usitembelee mpaka wa number E akisajili jua tu hutauza bei sawa na wa E!

Atakaesajili Dualis kwa namba EAB akiiweka sokoni tu na wewe ukaweka DYZ yako sokoni at the same week kama bei ya EAB itakuwa 17M wewe wa DYZ lazma utauza chini tu tena unaweza shangaa wewe ikakata hata million 4-5 toka kwenye bei ya mpya. Ukashangaa yako unauza 13M ila ina upya ule ule wa EAB.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mahesabu yao si sahii yani gari ishuke thamani zaidi ya nusu kisa kubadilika namba? Hapana kwa kweli hawapo sawa. Kuna gari namba C na inauzwa bei zaidi ya D. Gari unakuta imetunzwa ipo kinanda then uuze bei rahisi kisa unasubiria E.

Mwingine anakuambia sinunui gari mpaka E ifike.... Yani nikae na hela kisa E huyo atakua hana mpango wa kununua gari ila mbwembwe za mitandaoni....
Gari ambayo ni namba C na inauzwa ghali kuliko D lazma iwe gari ya bei ghali na practical sana kama Land Cruiser labda!

Tena hio ni ile ambayo ina matunzo mazuri mno.
 
Aisee kuna siku niliona RAV 4 namba A ni mpya, nikajiuliza au namba wamebandika????

Yes gari nyingi kubwa zinadumu sana. Maana huwa imara. Range rover namba A unakuta si sawa na IST namba DC utakuta ile range bado mpya...
 
Naona GSM kailimbiza namba DY kaingiza gari kama 100 na ushekhe na akiweka na tela zake ina maana anadouble namba...
 
Aisee kuna siku niliona RAV 4 namba A ni mpya, nikajiuliza au namba wamebandika????

Yes gari nyingi kubwa zinadumu sana. Maana huwa imara. Range rover namba A unakuta si sawa na IST namba DC utakuta ile range bado mpya...
Zile gari zina ground clearance nzuri mno
 
Mimi natafuta 2M mniuzie IST D niwe naenda nayo kubebea radiator
 
Umeangalia wapi Mkuu?

Kama hizi hesabu zako zingekuwa sahihi maana yake mpaka sasa tungekuwa DXL au DXK yaani hata DYA ingekuwa bado sana.

2021
Sept-Oct.....DXE-DXF.
Nov-Dec......DXG-DXH.

2022
Jan-Feb.....DXI-DXJ.
Mar-Apr.....DXK-DXL.

UHALISIA:
Toka September 2021 mpaka March 2022.(Na hapa March ndiyo imeanza tu)

DXE..
(F,G,H,I,J,K,L,M,N,O,P,Q,R,S,T,U,V,W,X,Y,Z)

DYA...B,C,D,E,F,G,H,I,J,K,L,M,N,O,P,Q,R)

Yaani kwa miezi 7 (Sept 2021-Marc 2022) tumeenda herufi 40.(March ikiwa siku 4 tu)

Kwa mwezi ni herufi (40/7)=5.7.

Mkuu,Mimi natumia DXE kama benchmark sababu nina uhakika nayo (ndiyo namba yangu) halafu nyie mnaangalia sehemu,unaona tofauti.[emoji16][emoji16].

Kama mwezi tunasajili herufi 5.7 maana yake DZA-DZZ (herufi 26) itatuchukua miezi (26/5.7)=4.6

Hii wala siyo PROBABILITY bali ni ACTUALITY

Toa I na O mzeee hazitumiki
 
Wewe jidanganye tu na hio Dualis yako DYZ!
Hata ukiifungia kabatini usitembelee mpaka wa number E akisajili jua tu hutauza bei sawa na wa E!

Atakaesajili Dualis kwa namba EAB akiiweka sokoni tu na wewe ukaweka DYZ yako sokoni at the same week kama bei ya EAB itakuwa 17M wewe wa DYZ lazma utauza chini tu tena unaweza shangaa wewe ikakata hata million 4-5 toka kwenye bei ya mpya. Ukashangaa yako unauza 13M ila ina upya ule ule wa EAB.
Kwani unanunua gari uuze au hitaji lako la kwanza ni kukusaidia ktk mizunguko yako!?
 
Huo ni mfano tu mkuu na kama wewe unatembelea gari moja hadi ufanane nayo kuna watu wananunua magari na kuyauza mda mfupi baada ya kuyasajili kwa watu watakaoyapenda.
 
Ila waTZ wakiamua jambo lao hawashindwi. Ile speed ya watu kununua magari Oct-Dec 2021 si tunaikumbuka lakini?

Hata hivyo hiyo miezi hata Japan gari hushuka bei, ndio muda muafaka kama umezishanga kuagiza gari
 
Kuna meli inaitwa TRANQUIL ACE inaingia March 15. Hii ndio meli kubwa kuwahi kuja TZ. Mara ya kwanza ilikuja 2021 August ilishusha magari 3700+

Ngoja tuone

Kuna gari za kwenda Malawi, Zambia n.k
 
Wewe jidanganye tu na hio Dualis yako DYZ!
Hata ukiifungia kabatini usitembelee mpaka wa number E akisajili jua tu hutauza bei sawa na wa E!

Atakaesajili Dualis kwa namba EAB akiiweka sokoni tu na wewe ukaweka DYZ yako sokoni at the same week kama bei ya EAB itakuwa 17M wewe wa DYZ lazma utauza chini tu tena unaweza shangaa wewe ikakata hata million 4-5 toka kwenye bei ya mpya. Ukashangaa yako unauza 13M ila ina upya ule ule wa EAB.
Tatizo watanzania ni washamba sana.
 
Back
Top Bottom