Pre GE2025 Tunapata fundisho gani Kwa Trump, Rais wa zamani wa America, kukutwa na hatia Kwa makosa ya jinai?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Fundishonnililolipata ni kuwa huyu wa kwetu anatakowa tumfunge kifungo Cha maisha jela.maana Nchi amaiharibu sana
 
Hukumu ya kihistoria imetolewa katika mahakama za huko America, Kwa Rais mstaafu wa nchi hiyo, Donald Trump, kukutwa na hatia Kwa makosa 34 ya jinai, aliyoshitakiwa nayo.

Hiyo inamfanya Donald Trump, kuwa Rais wa kwanza mstaafu wa America, kukutwa na hatia, Kwa makosa ya jinai tokea Taifa Hilo liundwe.

Kwa nchi yetu najua Hilo haliwezekaniki kutokea, Kwa kuwa Taifa letu, watawala wetu wametengeneza Katiba, inayompa Kinga Rais yeyote anayedumu Kwenye madaraka, kuwa hatashitakiwa Kwa makosa yoyote, anapokuwa madarakani na hata pale anapostaafu!

Ndiyo maana madai yanayotolewa na wananchi walio wengi, pamoja na vyama vya upinzani vya nchi hii ya madai ya kuandikwa upya wa Katiba ya nchi yanakuwa na nguvu sana

Swali hapa ni kuwa kama nchi tunapata fundisho gani Kwa Rais mstaafu wa Taifa kubwa na lenye nguvu kubwa za kiuchumi, kukutwa na hatia Kwa makosa ya jinai aliyoyafanya akiwa madarakani?

Somo pekee tunalopata hapa ni kuwa hakuna Binadamu, aliye juu ya Sheria, hata Rais wa nchi anapaswa kushitakiwa, iwapo atafanya makosa ya jinai.
Somo kuu ni kuwa In America no one is above the law even the President,huku kwetu Rais yuko juu ya sheria,hagusiki
 
Fundisho ni Moja tuu,mtawala Yuko Juu ya chochote hakuna Cha Marekani Wala Katiba Mpya 😁😁
 
Somo kuu ni kuwa In America no one is above the law even the President,huku kwetu Rais yuko juu ya sheria,hagusiki
Absolutely true

Hapa kwetu, wanamlinganisha Rais wetu kuwa sawa na Mungu!😎
 
Fundishonnililolipata ni kuwa huyu wa kwetu anatakowa tumfunge kifungo Cha maisha jela.maana Nchi amaiharibu sana
Suluhisho ni kuunda Katiba ya nchi, ambayo haitamfanya Rais wa nchi awe juu ya Sheria, ambapo hapaswi kufunguliwa mashtaka yoyote ya jinai, anapokuwa madarakani na hata anapostaafu!😎
 
Back
Top Bottom