Tunapitia mengi katika kutafuta. Tusikate tamaa (Kutoka kuwa walimu wa nursery hadi mkufunzi wa elimu ya juu)

AHSANTE SANA NDUGU PIA HONGERA SANA. NAAMINI IPO SIKU NA MIMI NITAANDIKA UZI KAMA WEWE, NINA IMAN NIMEFANYA INTERVIEW NASUBIRI MAJIBU. STORY INAFUNZA
 
AHSANTE SANA NDUGU PIA HONGERA SANA. NAAMINI IPO SIKU NA MIMI NITAANDIKA UZI KAMA WEWE, NINA IMAN NIMEFANYA INTERVIEW NASUBIRI MAJIBU. STORY INAFUNZA
Kila la heri kiongozi, Mungu awe nawe
 
Hongera sana mkuu.
 
Unafurahi kuajiliwa
Umekubali kuishi maisha ya utumwa mpaka unakufa.

Sisi vijana tunataka historia za kujiajili sio kuajiliwa.

Maisha Yako yatakuwa kula kuoga kuvaa nguo kuwahi kufundisha mpaka unakufa

Acha nipumzike
Si wote wenye uwezo wa kujiajiri instantly baada ya ku-graduate...na haitawezekana wote tufanye biashara, Mungu akivyotuumba ametugawia vipawa tofautitofauti...Mpongeze mwenzako acha ngebe bhana mbona watanzania hatuna tabia ya kupendana?
 
Asikutishe Mkuu kila mtu afanye kile roho yake inapenda. Haya ni maisha tunapaswa kufurahia wewe furahia maisha bhana. Endelea kulamba asali.
 
Unalipwa Sh ngapi hapo?
 
Hongera mkuu tupe hints za interview inakuwaje
 
Tsh. 1,451,000
Kibunda kinene kabisa hiki.

Nafikiri sasahivi ushaanza kuwa Kigogo[emoji2][emoji2][emoji2]

Umeadimika sana humu, bila shaka unalisongesha vizuri Gurudumu la Utumishi wa Umma
 
Hivi MTU akiwa na GPA 3.4 KUshuka chini,anaweza pata nafas za kufundisha hata vyuo vya kati?Naona Vyuo vikuu wanaanziaga 3.5+
 
Kibunda kinene kabisa hiki.

Nafikiri sasahivi ushaanza kuwa Kigogo[emoji2][emoji2][emoji2]

Umeadimika sana humu, bila shaka unalisongesha vizuri Gurudumu la Utumishi wa Umma
Hahaha kaka nipo sana humu ila sichangii mada sana, ila nishakuwa addicted na jf
 
Hivi MTU akiwa na GPA 3.4 KUshuka chini,anaweza pata nafas za kufundisha hata vyuo vya kati?Naona Vyuo vikuu wanaanziaga 3.5+
Kwa vyuo ambavyo si vya juu unaweza kupata, kama vile vya maendeleo ya jamii.

Ila Kwa hivi vya elimu ya juu muongozo unataka uwe na 3.5 au 3.8 kulingana na hadhi ya chuo husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…