Unajuwa ubongo wa binadamu una maajabu yake. Ukiona demu anapenda shopping basi "somo la kwanza" lazima lianzie kutoka kwa wakorinto (Mlimani city) vingenvyo facult ya ubongo wake itakataa. Ukiona demu ni mpenda movie basi ili akusikie lazima uanze na mambo ya Kanumba, vinginevyo rejeta itachemsha. Ukiona demu ni mtu wa high tech basi lazima uanze na mambo ya iPod, iPhone, kabla hujaingiza mambo ya i-Fak vinginevyo hilo la mwisho (baada ya iPhone) hataweza kukuelewa mana haliko kwenye facult ya ubongo wake. Sambamba na hilo binadamu anasikia kwa urahisi kitu anachotegemea au anachotaka kukisikia. Mfano nilikuwa na demu wangu ambaye wakati mwingine nikikohoa anazani nimemwambia "I love you" na anaitikia akisema "I love you too". Nikipiga chafya anazani namwita aje (jina lake lina sound kama sauti ya chafya) na akija anakumbana na harufu ya chafya!!
Hivyo basi kwa kujua jinsi binadamu anavyopenda kusikia kile anachotarajia watu tumekuwa tukisema vitu visivyotoka moyoni, maana ndivyo vinavyotakiwa na kupokelewa kwa urahisi. Demu akijuwa kwamba kwa kukuambia hakupendi utakwenda kujitundika au utamtundika anamua "asiuwe" kwa usalama wako na wake pia. Ebu fikiria demu kila kukicha simu yake unamjazia vocha, account yake unaipendezesha kila ikisinyaa, unampa kila kitu anachohitaji, na anajuwa unafanya hivi kwa mapenzi. Unadhani atakuwa mjinga akuite na kukuambia kwamba kapata jibaba linalomtusua na kwamba hajisikii nawe tena? Akifanya hivyo atakuwa irrational.
Bottom line!! Atakueleza kile ambacho anazani upo tayari kukipokea, huku akipunguza penzi taratibu hadi uzoee uhusiano mpya anaotaka uwe nao...wanaita "piece meal." Wito wangu ni kwamba kamwe husimwonyeshe mpenzi wako (gf au bf) penzi 100% na wala husimpende 100%, maana penzi halina bima. Husipomwonyesha penzi 100% utamfanya akueleze kile kilocho moyoni bila hofu na wewe utajiweka tayari kupokea chochote atakachokueleza bila kuathirika sana, mana hukuwa in full gear.