Tunapoambiwa kuwa Tanzania inakuwa 'Rebranded' ni vyema pia tukaambiwa nani 'aliichafua', lini na kwa manufaa gani

Wanataka kupiga pesa za walipa kodi tu. Eti unafanya rebranding kwa sababu kuna Rais mwanamke!? KWELI? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Toka nje ya Tanzania ndio utajuwa Tanzania haijulikani!!
 
Ni mawazo ya kipumbavu sana kuwahi kuyasikia. Na haya eti ndio maono ya Nchi! Kujulikana Duniani. Kwa hiyo, tukijulikana watoto mashuleni watapata Madawati na Vitabu na wazazi watapata uwezo wa kuwalipia Ada? Niliposema tuna Raisi ambaye hana maono na badala yake tuna Raisi ambaye ameziba pengo la kikatiba sikuwa nimekosea!
 
Wanataka kupiga pesa za walipa kodi tu. Eti unafanya rebranding kwa sababu kuna Rais mwanamke!? KWELI? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Tanzania haijulikani kama unavyo weza jiaminisha kuna mtu unaweza muambia umetokea Tanzania ikachukuwa muda Sana kuelewa adi atizame ramani ni shakutana na wengi Sana !!
Ata wachina karibu ya 60 hawajuwi kama kuna Nchi inaitwa Tanzania!!
 
Hii research yako ulifanya wapi? Hao wageni chungu nzima tunaopata kila mwaka na wanaoingiza $$$ billions kutoka nchi mbali mbali duniani wanafika vipi katika nchi ambayo haifahamiki?

Mawazo ya kijinga sana! North Korea, Afghanstan, Irak na Rwanda nazo hazijulikani? Hivi haya ndio maono ya kuongoza Nchi? Hivi kwa mfano, kungetokea Mchuano ndani ya Chama wa kumtafuta mgombea wa CCM na mama akawa miongoni mwao haya ndo mawazo angeenda nayo kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wampitishe kukiwakilisha Chama?
 
Hii research yako ulifanya wapi? Hao wageni chungu nzima tunaopata kila mwaka na wanaoingiza $$$ billions kutoka nchi mbali mbali duniani wanafika vipi katika nchi ambayo haifahamiki?
Hebu tuwaulize uhusiano kati ya Nchi kujulikana na kuendelea kwa Nchi husika.
 
Ushaambiwa kuna wakati una uvumi ulipita na ukazimwa, kwamba alitaka kubwaga manyanga, yaani alikuwa hakubaliani na sera za mwendazake.
 
Hivi huo uwekezaji tunaousema ndio kwanza unafanyika Tanzania au umewahi kufanyika? Ni aina gani ya uwekezaji anaouleta ambao ni tofauti na wa Mkapa na Kikwete?
Dunia huenda ikibadilika na mahusiano ya watu hubadilika pia.

Tanzania yenye reli na ndege zake ya Samia ni tofauti na ile ya waliomtangulia.

Tanzania yenye watu milioni 60 na kundi kubwa la wasomi uwekezaji wake ni tofauti na ule wa wakati wa Mwinyi wakati idadi ilipokuwa milioni 25.
 
Hii research yako ulifanya wapi? Hao wageni chungu nzima tunaopata kila mwaka na wanaoingiza $$$ billions kutoka nchi mbali mbali duniani wanafika vipi katika nchi ambayo haifahamiki?
mkuu umesafiri Nchi ngapi apa ulimwenguni?
nina hakika ata 2 huja safiri ungekuwa umesafiri usinge bisha kabisa!
Bora useme umetokea Kenya kidogo Sana ina fahamika!
kama South Korea Thailand ndio kabisa china yenyewe nina kuhakikishia karibia ya 60% au zaidi hawajuwi Tanzania!
urusi hivyo hivyo! licha unaona watali wao wamekuja wengi mwaka huu ni corona imewafanya wakaitambua Tanzania! na warusi na marekani ndio wanaongoza kwa matumizi ya pesa starehe!
 
Ushaambiwa kuna wakati una uvumi ulipita na ukazimwa, kwamba alitaka kubwaga manyanga, yaani alikuwa hakubaliani na sera za mwendazake.
Kazi ya urais na umakamu ni ngumu zina changamoto zake nyingi na binadamu wakiwa pamoja lazima siku moja moja wapishane kauli.
 
Akiboresha Burigi pia ndege zitatua Chato Airport.
 
Mkuu una juwa watu wengi Sana kama wewe kama umekulia hapa hapa Tanzania na hujawahi kutoka unaweza hisi ni mwazo ya kijinga kama unavyo hisi!!
kuna siku utajiona bado wewe mwazo yako ni madogo Sana Sana kuliko ulivyo tegemea! kama hao Afghanistan nina marafiki zaidi ya 3 hakuna ata mmoja anaye ijuwa Tanzania!
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ acha ujinga wa kujifanya unanijua! Narudia tena hao Watalii wanaoingia Tanzania kila mwaka na kuingiza kwa nchi billions of dollars wanaamua vipi kwenda katika nchi isiyofahamika duniani? Acha kuandika upumbavu.
 
Jina lako haliakisi akili yako! Kwa iyo nchi zilizofanya iyo program nazo zilikuwa zinakarabati???

kwanza iyo program unaijua?? Ushawai hata kuangalia vipindi kama Quest means business huko CNN??
 
Mkuu kumbuka kuwa JPM miaka mitano yake kajenga mazingira ya uwekezaji wa ndani na nje. Sioni dhambi kwa awamu ya sita kujikita katika kuhakikisha miundo mbinu hiyo inaanza kuleta tija kwa taifa.

Kagame alikwenda kuwekeza Arsenal ili jina la nchi yake lionekane juu ya jezi ya timu hiyo, hakuwa mjinga hata kidogo.

Sisi wenye serengeti na mikumi na Tanzanite itakuwa aibu kama tunaishia kujitangaza kiuoga kimataifa.
 
Aisee nimeipenda hoja yako
 
Unajua kwa mwaka Tanzania inapokea watalii hawazidi Mil 2??? Na haijawai zidisha zaidi ya hapo???

Unajua South Africa wanapokea watalii si chini ya Mil 5 kwa mwaka??? Unajua ni Kwa nini???

Unajua kuwa Misri wanapokea watalii si chini ya Mil 10 kwa mwaka ??? Unajua ni Kwa nini???

Labda nikusaidie! Hizi nchi sina program za kujitangaza kwenye hizo channel kubwa duniani.

Nilikuwa nakuonaga una akili Ila leo umeniangusha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…