Tunapoambiwa kuwa Tanzania inakuwa 'Rebranded' ni vyema pia tukaambiwa nani 'aliichafua', lini na kwa manufaa gani

Tunapoambiwa kuwa Tanzania inakuwa 'Rebranded' ni vyema pia tukaambiwa nani 'aliichafua', lini na kwa manufaa gani

Jina la Tanzania lilichafuka. Mwendazake aliifanya Tanzania kuwa na taswira ya kidikteta kama vile Korea Kaskazini.

Ndiyo maana anasema inabidi nchi isafishwe kwa kuwazungusha waandishi wa habari wa kimataifa wajionee wenyewe jinsi Uhuru, haki na furaha vilivyorejea nchini baada ya kwenda jehanamu yule dikteta.

Halafu baada ya hapo hao waandishi watusafishe... rebranding.
Sio tu Tanzania kuchafuka, Tanzania bado na haijawai kutangaza vizuri kwenye channel bora za kimataifa nafasi yake duniani kwenye uzalishaji, bidhaa na utaliii. Hii ndo nafasi ambayo Tanzania imeipata na inatakiwa iitumie vizuri sana!
 
😂😂😂😂😂😂 acha ujinga wa kujifanya unanijua! Narudia tena hao Watalii wanaoingia Tanzania kila mwaka na kuingiza kwa nchi billions of dollars wanaamua vipi kwenda katika nchi isiyofahamika duniani? Acha kuandika upumbavu.
kwa sababu una chat hapa if una hisi wewe ni mjuzi Sana lakini ni kuhakikishia kama umesoma hapa Tanzania na huna exposure wewe bado hujuwi kitu mkuu bado Sana!!
ujanja wako ndio hizo number za watalii ulizo ziona apo sio!! bado sana kama una exposure 0 bado huwezi kuelewa lolote!
 
Tatizo si Tanzania kutojulikana bali ni Infrastructure.
Nazungumza na Watalii ambao huamua kwenda Afrika ya Kusini na si Tanzania na Infrastructure inachangia sana maamuzi yao. Barabara za uhakika, maji na umeme wa uhakika si kama hapa nchini vyote vya kuunga na gundi. Ni mimi nisiye na akili 😂😂😂😂
Unajua kwa mwaka Tanzania inapokea watalii hawa Udi Mil 2??? Na haijawai zidisha zaidi ya hapo???

Unajua South Africa wanapokea watalii si chini ya Mil 5 kwa mwaka??? Unajua ni Kwa nini???

Unajua kuwa Misri wanapokea watalii si chini ya Mil 10 kwa mwaka ??? Unajua ni Kwa nini???

Labda nikusaidie! Hizi nchi sina program za kujitangaza kwenye hizo channel kubwa duniani.

Nilikuwa nakuonaga una akili Ila leo umeniangusha sana
 
Hivi huo uwekezaji tunaousema ndio kwanza unafanyika Tanzania au umewahi kufanyika? Ni aina gani ya uwekezaji anaouleta ambao ni tofauti na wa Mkapa na Kikwete?
Ungekuwa na exposure usingeuliza Hilo swali.

Mleta mada na wewe nyie ndo mapandikizi ya nchi jirani ambao mnajazana kwenye mitandao humu kutengeneza propaganda chafu ili Tanzania isiwe na programu Safi na muhimu za maendeleo.

Duniani kila mtu anazalisha Ila inaitaji kujitangaza sana ili uvutie wawekezaji wengi na wa uhakika. It’s all about competition na survival for thé fittest! Ni lazima tujitangaze na matunda yake tutayaona sana
 
Unajua kwa mwaka Tanzania inapokea watalii hawazidi Mil 2??? Na haijawai zidisha zaidi ya hapo???

Unajua South Africa wanapokea watalii si chini ya Mil 5 kwa mwaka??? Unajua ni Kwa nini???

Unajua kuwa Misri wanapokea watalii si chini ya Mil 10 kwa mwaka ??? Unajua ni Kwa nini???

Labda nikusaidie! Hizi nchi sina program za kujitangaza kwenye hizo channel kubwa duniani.

Nilikuwa nakuonaga una akili Ila leo umeniangusha sana
Me mwenyewe mkuu hakika mshikaji nina muonaga yupo vizuri Sana lakini kani sikitisha Sana Sana!
unavyo muona jamaa ndio hivyo hivyo walivyo baadhi ya viongozi yaani tuna safari ndefu Sana!
 
Tatizo si Tanzania kutojulikana bali ni Infrastructure.
Nazungumza na Watalii ambao huamua kwenda Afrika ya Kusini na si Tanzania na Infrastructure inachangia sana maamuzi yao. Barabara za uhakika, maji na umeme wa uhakika si kama hapa nchini vyote vya kuunga na gundi. Ni mimi nisiye na akili 😂😂😂😂
Kwani kwenye mbuga za Africa Kusini na za Tanzania mfano Serengeti kuna tofauti gani ya infrastructures??!

Mie nimefika Kruger national Park iliyopo South Africa na nimefika Pia Serengeti iliyopo Tanzania. Nakuhakikishia Serengeti ni bora zaidi ya Kruger kwa kila kitu, kuanzia wanyama hadi miundombinu Ila Kruger inapokea watalii karibu mara 5 ya serengeti kwa mwaka!

Unajua shida ni nini???? Shida ni matangazo na watu wenye akili Kama zenu mnadhani kujitangaza ni kupoteza muda
 
we jamaa watali hawafuati umeme wala maji Safi wata shangaa nini ebow!
we mwambie mtali unataka kuona sehemu zakutisha au za kufurahisha yani bara bara mbovu mbovu au za lami ata kuambia mbovu mbovu! eti maji wana taka kuona maji machafu kabisa mnayo tumia nyie viumbe wa sayari nyingine!
 
Kuna madhara makubwa pia kuwapa position kubwa "washamba"..

Mshamba ni mtu ambaye hajawa exposed kwenye nyanja, vitu, mahali ila hata bado akitengenezewa mazingira ya kujifunza ila bado atachagua kubaki na ushamba wake...

Jk alikua Mwanajeshi na Amiri Jeshi mkuu sikuwahi kumuona amevaa combat alipokuwa Rais, Sikuwahi kumuona Mwinyi Alhaji Hasaan wala Mkapa hata Mwalimu na Combat...

Jiwe alipigilia hadi combat na sandals unajiuliza huyu mtu alikua sawa kweli or he was a serious bipolar case???

Katiba inaruhusu utoaji maoni ila vyombo vya habari vyote alivitia mfukoni hata tangu kuumwa kwake hadi kifo hakuna chombo cha ndani kiliripoti ni vyombo vya nje hasa Keznya baada ya hapo Kassim aliibuka na kufokea watu msikitini na kuendelea kukumbatia uongo na ufichaji taarifa...na kina Chalamila wanasema wameongea naye yuko fit anachapa kazi

Kwangu mimi Kassim ndio alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kujiuzulu huyu ndio mtendaji mkuu wa serikali wa kila siku iweje asiwe anajua kweli? Makamu wa Rais bongo ni "cheo picha" tu
 
Mama wa Kitasha atakuwa na magroup manne ya watu 25. Wameamua kwenda South Afrika nimejaribu kumshawishi sana waje Tanzania na jibu lake katika hao watu mia kuna baadhi wamewahi kufika Tanzania and they didn’t enjoy the experience of lack of electricity for so many hours also lack of clean water sometimes for days hivyo wameamua kwenda South Afrika. Kwani kufika kwenye mbuga za wanyama huwa wanapaa hata washindwe kuona barabara zilivyo mbovu. Acha KUKURUPUKA!!!!

i know what I am talking about with concrete evidence. There you go!

Kwani kwenye mbuga za Africa Kusini na za Tanzania mfano Serengeti kuna tofauti gani ya infrastructures??!

Mie nimefika Kruger national Park iliyopo South Africa na nimefika Pia Serengeti iliyopo Tanzania. Nakuhakikishia Serengeti ni bora zaidi ya Kruger kwa kila kitu, kuanzia wanyama hadi miundombinu Ila Kruger inapokea watalii karibu mara 5 ya serengeti kwa mwaka!

Unajua shida ni nini???? Shida ni matangazo na watu wenye akili Kama zenu mnadhani kujitangaza ni kupoteza muda
 
Leo GENTAMYCINE natoa angalizo kwa wale ambao huko maofisini au katika maeneo mengine mnapokuwa na vyeo vya manaibu (makamu) wa ubosi mkiona wakubwa zenu wanakosea au wanaharibu muwe mnasema mapema au mnaachia ngazi kuliko kuendelea kuwa nao kiutendaji.

Halafu, ama wakistaafu kazi au wakifa ndiyo mnakuja kutuonyesha 'kimafumbo' kuwa mlikuwa hamkubaliani 'kimaamuzi' kwani wenye akili kubwa tutawatafsiri nyie si tu ni wanafiki bali pia mna 'vielementi' vya uchawi pamoja na vya ufitini pia.

Ninaamini message sent and delivered.
Kuna story moja sijui ina ukweli kiasi gani.

Kruschev alichukua madaraka baada ya Stalin kufariki, siku moja kwenye kikao ndani ya chama, Kruschev akapiga sana madongo kwa Marehemu Stalin. Kuna member mmoja akamwandikia swali Kruschev, "Mbona hukusema haya wakati Stalin yupo madarakani?". Baada ya swali kufika kwa Kruschev, alipolisoma akauliza "ni nani ameandika hili swali nimpe jibu lake?", kila mtu akapiga kimya. Akauliza tena, kila mtu kimya. Akawaambia, natumaini mmepata jibu.

Moral of the story, courage sio kitu chepesi, kwenye hizi nchi zetu zisizojali haki, Mamlaka ni kama bulldozer, na wewe ni papai tu. Watu kama kina Lissu na Mdude ni wachache sana, kwamba unafuatiliwa, unatekwa, unapigwa ,unaumizwa na bado unakuwa mwiba sio kazi ndogo. Kwani Ulimboka yupo wapi?

Unasema ukiona mkubwa anaharibu "sema" au "achia ngazi", yaani unaamini Vice President au Prime Minister anaweza sema dhidi ya mkubwa wake au unadhani anaweza kujiuzuru? Hiyo ni theory, practically that can never happen, labda sio hapa Tanzania. Unamkumbuka yule Katibu Mkuu wa CCM aliyeona mambo yanaharibika "akasema ukweli", aliishia wapi?
 
Mtateseka sana nyie burundi na Rwanda gang. Tumejifunza mapandikizi yote ya nchi zingine msahau tena kukamata uongozi wa nchi hii
Huo ushahidi kwamba sisi ni Burundi Rwanda gang uko wapi? Lord Denning ni mtu sana kisheria huko uk...weka ushahidi
 
Jina lako haliakisi akili yako! Kwa iyo nchi zilizofanya iyo program nazo zilikuwa zinakarabati???

kwanza iyo program unaijua?? Ushawai hata kuangalia vipindi kama Quest means business huko CNN??
Usilete dharau zako za kijima. Wewe ndio mwenye akili sio na kwamba ndiye unayefahamu kila kitu kilichopo Tanzania na nje ya nchi?

Tafadhali tusikoseani adabu, mind your business if you feel you can't swallow the versatile pill. Respect other's opinions as yours do.
 
Leo GENTAMYCINE natoa angalizo kwa wale ambao huko maofisini au katika maeneo mengine mnapokuwa na vyeo vya manaibu (makamu) wa ubosi mkiona wakubwa zenu wanakosea au wanaharibu muwe mnasema mapema au mnaachia ngazi kuliko kuendelea kuwa nao kiutendaji.

Halafu, ama wakistaafu kazi au wakifa ndiyo mnakuja kutuonyesha 'kimafumbo' kuwa mlikuwa hamkubaliani 'kimaamuzi' kwani wenye akili kubwa tutawatafsiri nyie si tu ni wanafiki bali pia mna 'vielementi' vya uchawi pamoja na vya ufitini pia.

Ninaamini message sent and delivered.
You guy! rebranding it self doesnt mean only what you perceive. it goes further as explained in this definition from WIKIPEDIA

Rebranding
is a marketing strategy in which a new name, term, symbol, design, concept or combination thereof is created for an established brand with the intention of developing a new, differentiated identity in the minds of consumers, investors, competitors, and other stakeholders.[1] Often, this involves radical changes to a brand's logo, name, legal names, image, marketing strategy, and advertising themes. Such changes typically aim to reposition the brand/company, occasionally to distance itself from negative connotations of the previous branding, or to move the brand upmarket; they may also communicate a new message a new board of directors wishes to communicate.

Nafaham kabla ya kupost hii thread yako, pengine umepitia maana nyingi, na hivyo ukajikita katika hoja uliyo itolea maelezo.

Ingawa, maelezo yako na maana ya re branding, kidogo vinatofautiana hasa uliposema suala la unafiki.

Asante.
 
Rebranding ina maana pana zaidi ya hulka za makamu kutokuwa muwazi wakati bosi akiwa bado yupo hai.

Aliyekuwa makamu aliona mengi na pengine tuseme alivumilia mengi pia.

Anayo haki ya kuja kivingine kwa maana ya kuboresha zaidi ufanisi wa kile kilichofanywa na mtangulizi.

Akileta wawekezaji wakubwa wa Kilimo na wakazalisha mazao mengi yakatumia reli ya SGR kutoa Mali bara na kuleta bandarini hapo makamu wa zamani anakuwa kaongeza ubora wa kilichoanzishwa na mtangulizi.

Akileta wawekezaji wakazalisha Mali kule Chato na zikasafirishwa na ndege zitakazotua pale makamu atakuwa kaupa ubora uwanja ule.

Naamini makamu wa zamani ana nia njema na nchi lakini siku zote waharibifu wa nchi ni sisi wenyewe.
Kwanini hakujiuzulu mapema kama aliona mengi na akavumilia ili kujipa heshima zaidi kwa nchi na wananchi?

Kama alichagua kuwa kimya bila kuchukua hatua ya kujiondoa kwenye serikali dhalimu na isiyofuata sheria hata kwa sababu za visingizio tu, huoni kwamba unamwingiza kwenye mtego wa kutuhumiwa?

*It was logically very simple retreatment mindset era to strategically step down and regroup for the brilliant state remedial as opposed to what is revolving around now.
 
Ni rahisi kuhoji kwanini asijiuzulu lakini kila mmoja akiamua kujiuzulu kwa kutoridhishwa na uongozi wa juu yake hizo taasisi kubwa zilizofanikiwa duniani zisingeweza kufika zilipofika.

Cha muhimu ni huyu ambaye hakujiuzulu kufanyia kazi upungufu wote ambao aliuona, pengine ni bahati zaidi kuwa hakujiuzulu ili sasa aje na kitu kizuri zaidi kwa taifa.
 
Nani atathibitisha palikuwa na upungufu wakati aliyekuwepo hayupo kujibu upungufu unaodaiwa? Kumbuka usimhukumu mtu bila ya kumpa nafasi ya kujitetea. Anayetuhumiwa kufanya makosa hapo katangulia mbele za haki (RIP) na hana uwezo wa kujibu kinachodaiwa mapungufu. Mapungufu anayaona binadamu kwa kuwa kila mmoja anautashi wake. Ukiulizwa mapungufu yalisababishwa kwa kutozingatiwa sheria ipi hauwezi kuonesha hapa.

Kujiuzulu ndio kipimo cha thamani zaidi, angalau angetoka hadharani akatuambia umma kwamba nilitaka kujiuzulu lakini nilizuiwa au nilishauriwa na kina fulani nisifanye hivyo kwa sababu moja mbili tatu tungemwelewa vizuri tu sio gia hizi za kumsingizia mtu ambaye hayupo duniani tena akijua hawezi kuamka na kujitetea hii sio haki
 
RAIS MAGUFULI ALIMWEKA "JELA" MAKAMU WAKE SAMIA SULUHU HASSAN

Na Bollen Ngetti

MWANAMUZIKI Ndanda Kosovo aliwahi kuimba, "Jela..jela ni mbaya, jela..jela ni mateso". Ndanda hakukosea. Aliimba uzoefu alioupata jela hapo Ukonga. Ninamuunga mkono Ndanda kwa uzoefu nilioupata nikiwa jela Keko na Segerea. Jela ni mbaya. Ukiwa jela umezungukwa kuta nene ndefu huwezi kuona nje kwa kifupi unakuwa umenyimwa uhuru wako.

Hata hivyo hakuna jela mbaya duniani kuliko hata Gwantanamo kama jela ya fikra. Yani jela ambapo huwezi kutoa mawazo yako hadharani. Hii ni jela mbaya inayojengwa na shetani tu.

Niliwahi kudokezwa huko nyuma lakini sikuandika maana nilikosa ushahidi kwamba kuna wakati Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitaka kujiuzulu nafasi ya Umakamu kujiondoa kwenye gereza la fikra lakini wenye hekma na busara walimshauri asifanye hivyo.

Kwa namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyoongoza nchi hii kwa siku 100 ni dhahiri alikuwa jela la fikra. Ni ukweli kwamba hakukubaliana na mambo mengi ya Rais Magufuli hata kama leo anasema "Mimi na Magufuli ni kitu kimoja" lakini matendo ni tofauti.

Mama Samia hakukubaliana na uendeshaji wa demokrasia nchini. Alikuwa jela na ilimtesa ndio maana amechukua njia tofauti kuendesha dhana nzima ya demokrasia. Hakuwa na jinsi wala namna. Bila shaka alilia kimya kimya gerezani.

Mama yetu Samia hakupenda uminyaji wa Uhuru wa Habari. Ilimtesa ndio maana "Fundi" alipomwondoa duniani Pombe naye kuchukua hatamu waandishi wa habari wakashangweka. Akaruhusu Uhuru wa Habari na dunia imeshuhudia maana enzi hizo za jela hata andiko hili lisingetoka maana ningekwenda jela la majengo.

Mama Samia hakufurahishwa na kesi za kubumba. Ilimtesa, ilikuwa ni jela kwake ndio maana alipoingia madarakani akafyatua kesi 147 zilizobumbwa na TAKUKURU. Hali hii ilimtesa. Lakini kuachiwa kwa viongozi wa dini wa Uamsho waliosota kwa miaka 9 jela nayo ilimweka jela kisaikolojia Samia. Hakupenda uonevu.

Huyu mama ni swala 5. Ni Muislamu Safi. Hapendi mali za dhulma iwe ni kwa mtu binafsi au Serikali. Hakupenda fedha za dhulma zilizotokana na kesi za kubumba za uhujumu uchumi na ML ndio maana tunaendelea kushuhudia watuhumiwa wakichomolewa magerezani kwa makundi. Lilimuumiza lakini hakuwa na lakufanya maana hakuwa Mkuu wa Maamuzi, Rais. Kitendo cha Mahakama Kuu kuamuru Serikali kurudisha fedha za dhulma kwa kina Mbowe ni ishara nyingine ya kuwa mama yetu aliumia sana kwa matendo hayo. Alikuwa jela.

Makamu wa Rais Samia (sasa Rais) hakupenda watu kuishi kwa hofu na woga. Alitamani watu wawe huru ndani ya nchi yao ila waheshimu Sheria za nchi. Ndio maana leo hata mama lishe, bodaboda nakadhalika wanakwambia, "nchi inafunguka". Wanahisi uhuru walioukosa miaka 5 tuliyoipa kisogo.

Kumbe hata mradi wa Bandari ya Bagamoyo (BEZ) iliyopigwa vita na Pombe ilimkera. Ilimweka jela la kifikra. Hakupenda lakini leo ameamua tufanye mazungumzo mradi ufanyike.

Ndugu zangu, tumuunge mkono Samia kuondokana na gereza la kifikra ili tulisongeshe mbele gurudumu la maendeleo ya nchi.

Binafsi nimejitoa sadaka kumlinda na kumtetea Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan. Mniunge mkono.

Bollen@2021
#MguseMamaNinuke
 
Kwanini hakujiuzulu mapema kama aliona mengi na akavumilia ili kujipa heshima zaidi kwa nchi na wananchi?

Kama alichagua kuwa kimya bila kuchukua hatua ya kujiondoa kwenye serikali dhalimu na isiyofuata sheria hata kwa sababu za visingizio tu, huoni kwamba unamwingiza kwenye mtego wa kutuhumiwa?

*It was logically very simple retreatment mindset era to strategically step down and regroup for the brilliant state remedial as opposed to what is revolving around now.

Nani atathibitisha palikuwa na upungufu wakati aliyekuwepo hayupo kujibu upungufu unaodaiwa? Kumbuka usimhukumu mtu bila ya kumpa nafasi ya kujitetea. Anayetuhumiwa kufanya makosa hapo katangulia mbele za haki (RIP) na hana uwezo wa kujibu kinachodaiwa mapungufu. Mapungufu anayaona binadamu kwa kuwa kila mmoja anautashi wake. Ukiulizwa mapungufu yalisababishwa kwa kutozingatiwa sheria ipi hauwezi kuonesha hapa.

Kujiuzulu ndio kipimo cha thamani zaidi, angalau angetoka hadharani akatuambia umma kwamba nilitaka kujiuzulu lakini nilizuiwa au nilishauriwa na kina fulani nisifanye hivyo kwa sababu moja mbili tatu tungemwelewa vizuri tu sio gia hizi za kumsingizia mtu ambaye hayupo duniani tena akijua hawezi kuamka na kujitetea hii sio haki
Aliyejiuzulu katangulia mbele za haki lakini kaacha mambo mengi yanayoongea kwa niaba yake na ndiyo watu wanayoyatumia kumjadili.

Kama makamu alikuwa msaidizi tu ingawa aliona na alibariki kila kitu kwa usaidizi.

Kufanya uchaguzi baada ya rais kutangulia ingekuwa ngumu sana kumbuka gharama za uchaguzi mkuu kwa nchi moja ya afrika.
Katiba imempa yeye nafasi ya urais na limekuwa jambo lilotupitisha vyema kipindi kile kigumu.
 
Back
Top Bottom