Tunapoelekea ajira itakuwa ndoto kupata kwa watoto wa maskini na kama huna connection

Tunapoelekea ajira itakuwa ndoto kupata kwa watoto wa maskini na kama huna connection

Waache wakae kimya,kuja siku wasiokua na ajira watachoka.
 
Kama una ndugu yako amefanikiwa ni vizuri kumuomba akusaidie kupata mtaji ili na wewe ujipatie kipato. Ukisubiri ajira siku hizi unaweza kuchanganyikiwa, kuwa mlevi, mvuta shisha au changudoa
 
Binafsi, nilitambulishwa kwa mke wa Mheshimiwa fulani. Nikaona niwe na mawasiliano naye mara kwa mara kama dada yangu. Hivi majuzi, aliniuliza kama nilikuwa tayari nimepata ajira. Nilipomwambia kwamba bado sijapata, aliniambia atanisaidia kwa kuzungumza na mume wake ili aone namna gani anaweza kunisaidia.

Sasa hapa najiuliza, baada ya yeye kuzungumza na mume wake, ikitokea nikaombwa kutoa pesa, basi nitakuwa katika matatizo. Nimeamua niwe nafanya juhudi za kukusanya mtaji mwenyewe na kusahau kuhusu ajira ya Tamisemi.
Nilishaandika Tanzania haina tatizo la ajira kuna Tatizo la vipaumbele cya Nchi yetu hasa kwa viongozi!!

Ajira zipo nyingi na mahitaji yapo sana lakini serikali inagoma kuathiri ilu wapate posho na anasa za kuwalipia viongozi!!!

Ajira zipo kibao!!
 
Back
Top Bottom