Pre GE2025 Tunapoelekea uchaguzi mkuu 2025, tuepuke wagombea wanaotaka kutugawa kwa misingi ya udini, ukabila, jinsia na ukanda

Pre GE2025 Tunapoelekea uchaguzi mkuu 2025, tuepuke wagombea wanaotaka kutugawa kwa misingi ya udini, ukabila, jinsia na ukanda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CHADEMA badala ya kutuuzia sera zao na jinsi au namna gani inaweza kutatua na kumsaidia Mwananchi anayesumbuka mtaani, wao wamejikita kwenye siasa za utengano, visasi ,vinyongo na misimango.

Tukiacha ya Uchaguzi, ni dhahiri CHADEMA na wanachama wao, wamejikita mitandaoni na sera za Udini, Ukabila na Ukanda.

Mfano, kila Rais SSH anapofanya uteuzi, wao wanalalamika, Rais anateua watu wa Dini yake, sio hivyo tu, tuliwasikia walivyokuwa wakiwasimanga na kuwazodoa kabila la Wasukuma na kushusha Jamii yao na kuliita ni genge!

Isitoshe, CHADEMA imekuwa ikinadi sera za Kikanda, yaani wanataka makabila yaunde Majimbo kitu ambacho ni hatari kwa amani na Usalama wa Taifa.

Piga kura kwa umakini 2025
Stupid
 
Ha ha ha.

Kwamba ukisema hayo ndio utaonekana wewe ndie mwenye akili?
1000000331-jpg.2894540


Nyie CHADEMA ni hasara kwa Taifa hili.
Wewe ndio hasara. Kila kitu unawaza CHADEMA.
 
CHADEMA msubiri uongozi wa kupewa tu ifikapo 2025

Hamchaguliki.

Ulisikia mapovu ya Tundu Lissu juzi kwenye mahojiano na Star T.V

Mbula

Kwa akili zenu za ki CHADEMA mnafikiri anachagulika yule?
Unachagulika wewe.
 
Inapotokea vipindi vya uchaguzi wagombea wakiwa wanatafuta kura, pamoja na sera nzuri za kujiuza wanazokuwa nazo, pia huweza kutumia njia nyingine mbalimbali za kusaka kura. Sababu hizo zinaweza kuwa ukabila, udini, ukanda au jinsia. Wanaweza kutafuta kura kwa kutumia ukabila au kutafuta kura kwa kutumia udini.

Kufatuta uongozi kwa kutumia udini au ukabila unagawa watu. Kazi ya uongozi ni kujenga watu kuwa kitu kimoja ambapo wanaweza kushirikiana kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo bila kuhisi ubaguzi wa namna yoyote.

Kiongozi yeyote anayehubiri ukabila, ukanda au udini ili kupata kura ni mtu hatari sana katika taifa na hapaswi kupewa madaraka yoyote.

Tanzania ina makabila zaidi ya 120, hivyo tunapochagua viongozi tuangalie sera zao kama zinauzika na zinaweza kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Wakati wa uchaguzi, wagombea wengi hasa nafasi za juu huongeza nafasi za kutumia majengo ya dini na kushiriki shughuli nyingi za kidini ili kuweza kujiuza. Tuwe makini na kile wanachokisema na ku-digest yale yote yasiyo na chembe ya ubaguzi.

Kuna wale viongozi wanaohubiri ukanda, kwamba sasa ni zamu ya labda Kaskazini kutoa Rais etc etc. Hawa lengo lao linakuwa si zuri zaidi ya ubaguzi wa kikanda na kugawa wananchi.

Kuna wagombea wanaohubiri JINSIA, kwamba mkimchagua mwanamke hawezi kutimiza majukumu yake ya kiuongozi kutokana na wanawake wengi labda kuwa na majukumu ya kulea familia etc. Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Shinyanga Mjini, Mgombea wa CHADEMA alilalamika kubaguliwa na mgombea wa CCM, Patrobas Katambi kuwa msimchague mwanamke kwasababu anaingia siku zake hivyo hawezi kuleta maendeleo.

Ubaguzi wowote wakati wa uchaguzi ni mwiba mkubwa kwa maendeleo ya demokrasia, huweza kupelekea kutompata kiongozi sahihi na hata kupelekea machafuko kuanzia ngazi ya chini na hata nchi kwa ujumla. Majirani zetu Kenya chaguzi zao tumekuwa tukiona zikiendeshwa kwa misingi ya ukabila, ambapo makabila matatu (Wajaluo, Kikuyu na Kalenjin) ndiyo yenye nguvu.

Ubaguzi ni adui wa utu na unapaswa kupingwa kwa nguvu zote wakati wote na mahala popote

Je, chaguzi ulizoshiriki ni jambo gani mgombea alifanya ukaona ni ubaguzi?
Hebu mtaje mmojawao tuanzia hapo tuliwaweka wazi itakuwa jambo la heri kwa Taifa.
Tumetoka Vatican ujue kuomba baraka.
 

Yani hapo ndipo keyboard warrior wa CHADEMA mlipofikia?

Yaani umezunguka kwenye fuvu lako lote hilo ulilolibeba na yanayo kutoka kinywani ni "Stupid" ?? C'mon you can do better than that.

Jaribu kuwa mbunifu.

Yani unakasirika kusoma ukweli?

Econonist unajitahidi sana, ukizingatia kazi mbili ulizonazo. As a spin doctor and a masseur. Ndio, wewe ni mchua misuli na Mropokaji, vitu viwili tu ambavyo unalipwa na T.L na Mbowe kufanya. Una makasiriko tangi ujiunge na CHADEMA umebaki kuwa ulivyo. Kufanya massage na kutukana.
 
Unachagulika wewe.
Unakimbia hoja, unaleta viroja.

Wapi nimesema natafuta kuchaguliwa.

Mbowe na Lissu kila siku wanajinadi, unafikiri ni kwasababu wanawajali wananchi au ni kwasababu wanataka madaraka?
 
😂😂😂😂😂

Nitaenda kupiga kura nikizingatia haya:👇

1. Sukari kilo moja 5200/=
2. Hospitali hazina madawa ila magari yamefika namba STN 😂
3. Mgao wa umeme umekua sehemu ya maisha
4. Kuna mikoa haijaunganishwa kwa barabara ya lami
5. Bei ya mbolea imepanda kwa zaidi ya 40%
6. Maisha yamezidi kuwa magumu huku wachache wakifaidi keki ya taifa hukooooo
 
Back
Top Bottom