Tunapoficha makosa ya Diamond kwa kisingizio cha uzalendo

Tunapoficha makosa ya Diamond kwa kisingizio cha uzalendo

Mi hao wamaotukana kiswahili kwenye hizo page Twitter instagram na kwenye hizo blog wananichosha vibaya saana.... muda mwingine huwa naona hadi aibu kusoma waliyoandika

Utashangaa sana na ndio utajuwa mswahili wa Tandale alivyo na mashabiki mapunguwani. Jitolee kuwapa kuwalipia kwa Ras Simba, hii ni aibu tunachoreshana bila sababu.
 
Utashangaa sana na ndio utajuwa mswahili wa Tandale alivyo na mashabiki mapunguwani. Jitolee kuwapa kuwalipia kwa Ras Simba, hii ni aibu tunachoreshana bila sababu.

Mhhh Matola bana....
 
Last edited by a moderator:
kwani mondi yeye kamfanya nini davido??? and big brother amedanganya vipi sasa???

mkuu km umefuatilia hii ishu vizuri nadhani utakuwa unaelewa kuwa tweet ya davido haikuwa personal kwa diamond ila tweet ya diamond ilikuwa personal kwa davido hpo ndyo kuna tofauti na ugomvi ndyo umeanzia hpo
 
mkuu hebu jaribu kusoma between the line na ujiongeze kuelewa sio kukomaa na ligi

acha kukariri misemo, nisome between the line natafuta nini huko??? mi nimemuuliza boniface salim aliesema hata angeshinda mnamibia the tweet would remain the same, kwamba big has cheated again, so what does this mean??? wewe ukasema ujumbe wa davido ulimlenga big ambae bba iliyopita alimpa dilish wa Ethiopia ndio maana amemuambia 'N they cheated again' ndio nikakuuliza they cheated at first kwa kumpa dilish badala ya kumpa nani??? this time big cheated again kwa kumpa idris badala ya kumpa nani????
 
Last edited by a moderator:
Moderator unganisheni hizi thread za diamond za ile "diamond fans' special thread"

asante.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nimekuwa nikifuatilia hili suala la Diamond kuwa na msuguano na Davido tokea ushindi wa Idris Big Brother na nikiri kuwa Diamond hakupaswa kusema aliyosema dhidi ya Davido kwa sake ya urafiki wao!

Kwanini nasema hivyo? coz thamani ya urafiki waliokuwa nayo haiwezi kupotezwa kirahisi hivyo ingawa kuna watu wanafurahia tena kwa sababu za kitoto, kwa wale walioishasoma novel ya godfather nadhani wananielewa ninapozungumzia thamani ya urafiki! Kwani urafiki ni kama kula tunda na ukimaliza kuipanda mbegu yake ili siku utakapohitaji tena tunda uwe na sehem pa kulipata.

Sasa ninachoona ni giza kubwa mbele yetu sie mashabiki wa Diamond hatuoni ukweli tumejikinga kwenye kivuli cha uzalendo, hatutaki kukubali kuwa Davido kasaidia kupush mafanikio ya Diamond kwa kiasi fulani, mara baada ya number one rmx kutoka milango ilianza kufunguka kwa kasi kwa Diamond na hili wengi hatulioni bado tumefunikwa na kivuli cha uzalendo hatusimami kwny fact! ukitaka kuamini hili nenda youtube kaangalie number one rmx imeangaliwa na watu wangapi dhidi ya original version!

Kwa taarifa yako kuna gape la watu zaidi ya million mbili. Ndyo tunakubal Davido siyo mungu so Diamond hana haja ya kumtetemekea lakini kwa hili alipaswa kuonyesha heshima angalau kidogo kwani alichofanya ni ukosefu wa fadhila wa hali ya juu. mwisho na suggest Diamond afanye mpango amalize hili suala hata kama ni kimya kimya ili kuondoa tension iliyopo sasa.

Umeandika maelezo marefu lakini b hujagusa mzizi wa yote hayo hasa. Wakati ukijitahidi kujenga hoja dhaifu ya kuonyesha kuwa diamond kamkosea Davido lakini umeshindwa kabisa kupambanua n kuweza wazi chanzo cha msuguano na neno gani baya ambalo diamond alilolisema au kulifanya dhidi ya davido

Mi binafsi nilichokiona ni maneno ya chuki na kejeli aliyoyatoa davido dhidi ya ushindi wa Idris na Diamond kwani aliposema "they cheated again...." ni wazi alionyesha kutokubaliana na matokeo ya Big brother Africa na matokeo ya Channel O Africa Music Award.

Tukirudi katika swala la Big Brother tunajiuliza maswali mengi. Je Davido alikuwa ni mshiriki wa Big Brother? Je kuna cheating yeyote aliyoishuhudia? Na kwakuwa yeye sio mshiriki wa big brother kwanini akasirike kwa ushindi wa Idriss?

Nilichokiona hapo ni kuwa Davido ameweka UNigeria mbele kwanza kwakuwa ni Taifa lake na pia Diamond ameweka UTanzania mbele kwakuwa ni nchi yake au wewe ulitaka Diamond auuze Utanzania wake kwa urafiki mfupi tu wa Davido? kumbuka pia kwa maneno yale ya Davido ameukejeli hata ushindi wa Diamond alioupata CHOAMWA kuwa nayo ilikuwa ni cheating? Sasa wewe ulitaka Diamond akubali kutukanwa na kudharauliwa na mtu naye amnyenyekee tu kisa Davido ni rafiki yake? Tueleze zaidi ya kufanya Collaboration katika wimbo wa M Number 1 remix Diamond na Davido wana urafiki gani tena? Kuwa mzalendo wa Tanzania yako usiwe mtumwa wa kimawazo kuwa bila ya Nigeria wasanii wetu hawawezi kusonga mbele. Ukishaanza kujidharau mwenyewe ni nani atakayekuthamini?
 
WaTZ bana! Kwa hali hii CCM itaendelea kuongoza miaka milioni ijayo...

Kwa vile huyo Idrissa kashinda, basi sasa anaonekana alikuwa akipeperusha bendera ya TZ.

Nakumbuka serikali iliwahi kukana kutowatambua washiriki wa huo mchezo. WaTZ wakaungana na serikali yao kuyaponda mashindano; wakisema hayana maadili ya kitanzania n.k.

Sasa jamaa kashinda kitita, kila mtu (sijafahamu serikali kupitia wizara husika imesemaje juu ya ushindi huo) anasema Idrissa alikuwa akituwakilisha waTZ.

Pheeewww.

Tumia akili katika hoja zako wewe. Hakuna mtu yeyote aliyosema kuwa Idris alikwenda kuiwakilisha serikali au kuiwakilisha CCM bali ukweli n kwamba alikwenda kuiwakilisha Tanzania.

Naimani utakuwa unajua kuwa i uweze kushiriki ni lazima uteuliwe kutoka katika nchi yako na wakupendekeze uende kuwakilisha Taifa fulani. Na ndiyo maana licha ya majina yao washiriki pia hutambulika kwa utaifa wao. Hivyo bila kujali msimamo wa serikali ukweli ni kwamba Idriss alikuwa ni muwakilishi wa Tanzania
 
Labda kama alikwenda kukuwakilisha wewe na Familia yako sawa hamna maneno ila mimi sijawakilishwa na namtambuwa Idrisa kama mshiriki kutoka Tanzania.

Upumbavu wa watu mmoja mmoja msiliingize Taifa, Leo umwambie Mufti au Askofu eti aliwakilishwa na Idrisa kwenda kwenye ushetani wa BBA si unatafuta mshikemshike?
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Tumia akili katika hoja zako wewe. Hakuna mtu yeyote aliyosema kuwa Idris alikwenda kuiwakilisha serikali au kuiwakilisha CCM bali ukweli n kwamba alikwenda kuiwakilisha Tanzania.

Naimani utakuwa unajua kuwa i uweze kushiriki ni lazima uteuliwe kutoka katika nchi yako na wakupendekeze uende kuwakilisha Taifa fulani. Na ndiyo maana licha ya majina yao washiriki pia hutambulika kwa utaifa wao. Hivyo bila kujali msimamo wa serikali ukweli ni kwamba Idriss alikuwa ni muwakilishi wa Tanzania

Kweli wewe chura...unarukaruka tu hata pasipostahili kuruka.

Rudia tena kusoma post yangu..pengine utaelewa..
 
Ipo siku utatoa uzi hapa kutuambia tuinamishwe kwa wanaotusaidia
 
Davido ana madharau tena ukichanganya ufupi wake na jeuri ya pesa za kwake na za kwao basi ndo unakua shida kabisa...
 
Back
Top Bottom