Tunapofungua au kufunguliwa soda, mbona tunafuta kwa kidole ‘mdomo’ wa chupa?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Umuofia kwenu!

Niwarejeshe kwenye mada, inaeleweka bila mbwembwe, labda kama ni mimi tu.

Ni pale tukifungua soda kuondoa kizibo, wengi wetu hufanya kupitisha kiganja au kidole ili kufuta ‘kimdomo’ cha chupa, hii huwa na maana gani hasa?

Na sababu kama zipo, faida zake?

Picha.? Binafsi sina, labda atokee muungwana.

Maisha ni kuyafurahia, karibuni.
 
Nasubiri majibu..maana nafutaga alafu sijui kwanini nafutaga.😎
 
Kuna wakati ukifungua soda ukitazama kwa umakini kunakuwa na kitu kama kutu kuzunguka kwenye mdomo wa chupa na kisoda pia, wakati mwingine ufunguaji mbaya wa chupa unaweza sababisha mipasuko inayoleta particles ndogo ndogo za chupa kwenye mdomo wa chupa ambazo zinaweza kuwa hatari kwa mnywaji.

Unapofuta kwa tissue unajaribu kuondoa hayo niliyoyaorozesha juu.
 

Cheers [emoji1635]
 
Si ilirudi kiwandani kujazwa upya.? [emoji3][emoji3][emoji3]
Yeah ilijazwa but hatuna uhakika kama kwenye mdomo palioshwa vizuri..
Soda ya chupa hadi nifute na tissue ndio ntakunywa, kama tissue haipo hata leso ntafutia bt lazima nifute.
 
Binasi huwa nafuta kwa sababu 2:
1. Kile kifuniko ambacho kimetengenezwa kwa bati huwa kina kawaida ya kufanya kutu (rust) maeneo ya kwenye mdomo wa chupa.
2. Chupa zenyewe huwa zina kawaida ya kumenyuka na kuacha vipande vidogo vidogo ambavyo visipokata maeneo ya mdomo wa mtu basi vinaweza kuingia ndani ya mwili wa mtu na kusababisha madhara zaidi.

Ifike kipindi sasa haya makampuni ya vinywaji baridi watumie tu chupa za plastiki zenye mifuko ya plastiki ili kuwaepushia madhara wateja wao, ili pia kulinda afya zao.
 
Careem
Soda za ‘plastic’ zipo mkuu, lakini ladha yake ni tofauti kabisa aisee... yaani ni ya hovyo.

Kuhusu sababu ya kutu na chupa kumeguka ina-make sense, nakubali.
 
Careem
Soda za ‘plastic’ zipo mkuu, lakini ladha yake ni tofauti kabisa aisee... yaani ni ya hovyo.

Kuhusu sababu ya kutu na chupa kumeguka ina-make sense, nakubali.
Sio soda za plastiki mkuu, namaanisha chupa iwe ya kigae kama kawaida ila ufuniko uwe wa plastiki, ule ufuniko wa bati unaweka rust.
Kuhusu soda za kwenye chupa za plastiki kuwa na ladha tofauti, kumbuka soda soda zote zinazotengenezwa hapa nchini zina ufake flani hivi. "Umeshawahi kutumia soda za kopo kutoka nchi za nje?" Yaani ukinywa siku moja tu, hizi za nchini zote utaona takataka.
 
sababu ni hii

ili kuondoa zile chenga chenga au chambechembe za chupa. Maan la chupa huwa inapofungwa kunga grip force ambayo husababisha chupa kuchubuka hvyo kizibo pamoja na mdomo kuwa na hizo chengaa
 
Binafsi huwa nafanya vile lakini sio kwa lengo la kufuta isipokuwa huwa nahakikisha kama mdomo wa chupa upo salama au una krek na nikikuta kuna vimapengo yaani umepasuka hata kidogo huwa sinywi bali nalipia na kuimwaga
 
Sifutagi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…