Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapo baadhi yetu ambao wanaamini kuwa "sera za CCM ni nzuri ila zimekosa watekelezaji tu". Wapo wanaoamini kuwa sera hizi ni nzuri sana vitabuni ila hazijapata watu wazuri kuweza kuzifanyia kazi. Wengine wamefikia kuamini kuwa uzuri wa sera hizi unasababisha hata nchi jirani kuzi"copy" na kuzi"paste" kwenye mipango yao. Wale wenye kuamini hivi hatimaye huamini kuwa siku moja CCM itaweza kupata watu wazuri wa kuzitekeleza sera zake - hadi hivi sasa inaonekana watu hao hawapo. Miaka hamsini ya kutawala ati hawajapatikana watu wakuzitekeleza sera hizi vizuri.![]()
Sisi wengine tunasema siyo tu wamekosa watu wa kuzitekeleza bali hata wakipata watu wazuri kiasi gani sera hizo hazitekelezeki. Hazitekelezeki kwa sababu ni sera mbovu zilizoandikwa kwa maneno mazuri. Kwa watu wanaopenda maneno matamu ni rahisi sana kuhadaika na sera hizo.
Mfano mzuri ni hili la Kenya kutuwekea ngumu mabasi yetu ya kubeba watalii (tour buses) kutumia viwanja vyao kwa ajili ya watu wetu kubeba watalii na kuja nao Bongo. Ukiangalia kwa haraka haraka utaona kuwa ni matokeo ya kushindwa kwa sera mbalimbali; kuanzia ya usafiri, uchukuzi, uchumi n.k Sasa watu wengine wanapolalamikia Kenya na kuona kama Wakenya hawaoneshi kujali udugu na ujirani mwema wanasahau kuwa ukipanda mbigili usitegemee kuvuna mpunga! Tunavuna tulichopanda.
Inawezekana vipi katika mipango yetu yote na matumizi yote ya hela kwa miaka hamsini na ushee bado tunategemea huruma na hisani ya majirani zetu kufanikisha mojawapo ya kinachoitwa ni sekta muhimu sana? Hivi kwa muda wote huo watawala wetu walioshindwa wamekuwa wakinufaika kwa sababu ya huruma ya Kenya? Hivi wamesahau kabisa historia? Cha jirani siyo chako; hata kama kakuazima.
Kwamba kisa ni masuala ya sheria ya miaka 30 iliyopita ambayo inaonekana kushindwa kwenda na wakati au mahitaji nalo linathibitisha tu kushindwa kwa viongozi wetu. Hivi hatuwezi kufikiri mbali hadi itokee migogoro? Inawezekana kweli watawala wetu wanaendeshwa na matukio na siyo maono yenye kueleweka? Wengine wanasema na sisi tulipize kisasi; sawa lakini mwisho wake ni nini? Inaonekana kwenye utalii sisi ndio tuko kwenye huruma ya Wakenya.
Angalia kwenye sekta nyingine vile vile utaona tatizo hili la kushindwa kwa sera zao liko wazi japo hatujapata watu wenye kulionesha hili bayana. Miye nimedokeza kitu ambacho kiko dhahiri. Cha kushangaza na kusikitisha kuwa wapo baadhi yetu bado wanafikiria kuwapa tena watu wale wale miaka mingine mitano ya kujaribu sera zile zile ambazo zimethibitika kushindwa huko nyuma ati kwa vile watakuwa na sura tofauti. Kwani tatizo letu sisi sura? Ni sera.
Kama kuna mtu anasema wana sera nzuri; naombeni hata mfano mmoja wa maana wa uzuri wa sera zao.
Tanzania ni failed state. Kila kiongozi ni mwizi na sio muwajibikaji.
Ndugu Mhe prof dkt Kikwete ni rais msanii ambaye historia ya nchi hii itamweka katika kumbukumbu kwa usanii huo. Hakuwahi kuwa na dhamira ya dhati ya kusimamia kupatikana kwa katiba mpya iliyobora. Yeye alikuwa na bado anaendelea kutafuta legacy kwa kudandia kitu ambacho hakiamini, yaani hakikuwahi kuwa moyoni mwake. Matokeo yake ni hili libora katiba unaloona limependekezwa na litapitishwa tupende, tusipende. Hiki ndicho alichokuwa amedhamiria na huo ndio tunauiita usanii. Na historia itamuhukumu yeye na timu yake ya akina 6 na vijisenti!!Mwanakijiji, Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kuweka misingi imara ya kulipeleka taifa mbele, akaona aanze na kuandika katiba mpya kabisa, alichagua team makini ya akina warioba baregu salim. badae akaunda bunge la katiba lililojumuisha kila uwakilishi.
Alihakikisha watu makini wanapewa kutengeneza kanuni zitakazoongoza uendeshaji wa bunge la katiba, kazi hiyo akapewa mzee wetu Tundu Lissu, cha kushangaza akatunga kanuni mbovu na za hovyo kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akashindwa kuzitumia, na baada ya kuona hilo basi akae kupambana angalau tuokoe chochote akabeba virago akatimua akabaki kununua viandishi vya habari vya kipuuzi na kumwandika kila gazeti.
Tunaweza inyoshea vidole ccm, tuseme ukweli miaka yote report ya CAG ilikuwa haiendi bungeni JK akaamuru ipelekwe bungeni na ijadiliwe kwa uwazi na wahusika wawajibike, badala yake tunageuza report zile kuwa sehemu ya kupigia fitina, sote tunajua biashara ya iptl ilikuwa ya nani lakini tukamshupalia muhongo kipumbavu tu, haya tunaondoa muhongo tunamweka simbachawene halafu tunajiona washindi "hovyo kabisa"
Nashindwa kuelewa tunamwondoa balozi kagasheki tunaweka nyalandu hivi kichwani zinatutosha kweli? haya mambo hayaendi na hatuna mtu wa kutukwamua gharasha tumelamba wenyewe tunafungwa sasa, inakuwaje?
Mifano mizuri; lakini si unaona hata watu makini wanavyotumia muda kuwapa legitimacy na relevance wanaotangaza nia ndani ya CCM kana kwamba tumeshakubali Rais ajaye lazima atoke CCM?
Wapo baadhi yetu ambao wanaamini kuwa "sera za CCM ni nzuri ila zimekosa watekelezaji tu". Wapo wanaoamini kuwa sera hizi ni nzuri sana vitabuni ila hazijapata watu wazuri kuweza kuzifanyia kazi. Wengine wamefikia kuamini kuwa uzuri wa sera hizi unasababisha hata nchi jirani kuzi"copy" na kuzi"paste" kwenye mipango yao. Wale wenye kuamini hivi hatimaye huamini kuwa siku moja CCM itaweza kupata watu wazuri wa kuzitekeleza sera zake - hadi hivi sasa inaonekana watu hao hawapo. Miaka hamsini ya kutawala ati hawajapatikana watu wakuzitekeleza sera hizi vizuri.![]()
Sisi wengine tunasema siyo tu wamekosa watu wa kuzitekeleza bali hata wakipata watu wazuri kiasi gani sera hizo hazitekelezeki. Hazitekelezeki kwa sababu ni sera mbovu zilizoandikwa kwa maneno mazuri. Kwa watu wanaopenda maneno matamu ni rahisi sana kuhadaika na sera hizo.
Mfano mzuri ni hili la Kenya kutuwekea ngumu mabasi yetu ya kubeba watalii (tour buses) kutumia viwanja vyao kwa ajili ya watu wetu kubeba watalii na kuja nao Bongo. Ukiangalia kwa haraka haraka utaona kuwa ni matokeo ya kushindwa kwa sera mbalimbali; kuanzia ya usafiri, uchukuzi, uchumi n.k Sasa watu wengine wanapolalamikia Kenya na kuona kama Wakenya hawaoneshi kujali udugu na ujirani mwema wanasahau kuwa ukipanda mbigili usitegemee kuvuna mpunga! Tunavuna tulichopanda.
Inawezekana vipi katika mipango yetu yote na matumizi yote ya hela kwa miaka hamsini na ushee bado tunategemea huruma na hisani ya majirani zetu kufanikisha mojawapo ya kinachoitwa ni sekta muhimu sana? Hivi kwa muda wote huo watawala wetu walioshindwa wamekuwa wakinufaika kwa sababu ya huruma ya Kenya? Hivi wamesahau kabisa historia? Cha jirani siyo chako; hata kama kakuazima.
Kwamba kisa ni masuala ya sheria ya miaka 30 iliyopita ambayo inaonekana kushindwa kwenda na wakati au mahitaji nalo linathibitisha tu kushindwa kwa viongozi wetu. Hivi hatuwezi kufikiri mbali hadi itokee migogoro? Inawezekana kweli watawala wetu wanaendeshwa na matukio na siyo maono yenye kueleweka? Wengine wanasema na sisi tulipize kisasi; sawa lakini mwisho wake ni nini? Inaonekana kwenye utalii sisi ndio tuko kwenye huruma ya Wakenya.
Angalia kwenye sekta nyingine vile vile utaona tatizo hili la kushindwa kwa sera zao liko wazi japo hatujapata watu wenye kulionesha hili bayana. Miye nimedokeza kitu ambacho kiko dhahiri. Cha kushangaza na kusikitisha kuwa wapo baadhi yetu bado wanafikiria kuwapa tena watu wale wale miaka mingine mitano ya kujaribu sera zile zile ambazo zimethibitika kushindwa huko nyuma ati kwa vile watakuwa na sura tofauti. Kwani tatizo letu sisi sura? Ni sera.
Kama kuna mtu anasema wana sera nzuri; naombeni hata mfano mmoja wa maana wa uzuri wa sera zao.
Ripoti ya CAG peke yake ingekuwa inatosha kuwafanya Watanzania waamue kuwaondoa watawala wao wa sasa. Tangu 2006 ripoti hiyo imekuwa ikitolewa hadharani na miye nilishaacha kuifuatilia hasa baada ya kuona kina Utouh wanarudia mambo yale yale katika mapendekezo yao miaka nenda miaka rudi huku kila wakienda kukagua wanakutana na madudu yale yale.
Hivi unajua ni mara ngapi CAG kapendekeza wabunge wasiteuliwe kuwa wajumbe wa bodi za Mashirika ya Umma? kwani wameachwa?
Mkuu POMPO statement yako inanishawishi kwa kiwango kikubwa. Katika miaka 9.6 ya JK sikumbuki kama aliwahi kuitisha mhadhara au kuasisi mjadala na kukubali kuwa challenged. Mara zote utasikia anaongea na wazee wa Dar es Salaam ili kutoa maelezo juu ya tukio lililo hot kwa wakati huo. …yaani kujibu matukio. Kwa ufupi hakuna maono bali kusikilizia matukio!Mkuu nakuna maono yoyote wala.mipango yoyote kwenye serikali hii ya kikwete.
Kwa hiyo unashauri nini hasa kwenye hili la watalii kupitia Kenya? Na pili unataka tutoe CCM tulete nani? Na huyo unayetaka tumlete kwa kigezo gani, mimi kama mpiga kura nina uhakika gani kama ni bora klk huyu CCM? Ni kwa sababu tu ya maneno ya mtu na kukosoa ndiyo inatosha kunishawishi kwamba yeye ni bora?
Hua spendi sana kuchangia maada zako cause hua nahisi nitaharibu utamu wenyewe but anyway kaka mkubwa; hao unaowaona wanasifia ccm either humu jamvini au popote basi ujue ni kwasababu ya matumbo yao tu, wamewekeza akili zao kwa jambo la leo na sio kwa ajili ya watoto wao na watoto wa watoto wao, hili nalo ndio lile lile na kukosa vision, hatuwezi ku-plan mambo ya mbeleni zaidi ya miaka walau hata 10 tu, yoyote unaemwona anasifia hicho chama is either fisadi au anafaidika na mfumo huo wa kifisadi na au vinginevyo mtu huyo ujinga ndio unaomsumbua; nilichojifunza humu jamvini ni hiki, kuna ujinga mkubwa sana unaoendelea kwasasa, nao ni hu; mtu atachaguliwa tu eti kwasababu ya kua dini 1 nae au kabila moja nae, hivyo ni baadhi ya vitu vinavyosababisha ccm kuendelea kuwepo madarakani.Mifano mizuri; lakini si unaona hata watu makini wanavyotumia muda kuwapa legitimacy na relevance wanaotangaza nia ndani ya CCM kana kwamba tumeshakubali Rais ajaye lazima atoke CCM?
Kuanzia leo nitakua ninakuita kwa jina hili; "Mhe. Mkata tama" na watu wa jinsi hi tukiwa nao walau 10,000 tu basi kuumaliza umasikini utahitajika muujiza wa Mungu mwenyewe na sio akili zetu hizi alizotupa Mungu.Mzee Mwanakijiji napata mashaka na "hadhi" yako ya uzee. Anaingia adui ndani mwenu wakati wewe na "bibi" mnapigana. Je ni uamuzi upi sahihi utauchukua kati ya kuendelea na ugomvi wenu na "bibi" na kupambana mvamizi? Nakubaliana na ubovu wa sera sio tu za CCM bali sioni wa kuyabadilisha maswala kadhaa yanayohusu nchi hii kwa miongo kadhaa ijayo!