Tunaposema Sera za CCM zimeshindwa hatutanii, mfano hai huu..

Sera nzuri vitabuni siyo ishu kama uongozi ni wa ubabaishaji. CCM pamoja na ubovu wake sijaona mbadala wake kwa sasa! matukio ya ugawanaji holela wa madaraka kama vile viti maalum huko Chadema na kulalamikiwa na watu wengi inaonyesha ni jinsi gani ambavyo Chadema siyo mbadala wa CCM. Vyama vya upinzani vijiimarishe kimfumo, kiutendaji na kiuongozi ili hatimaye Watanzania wavipe dhamana ya uongozi huku wakiviamini. La sivyo vitaendelea kulalamika tu! Chama kuwa ni mali ya mtu mmoja na kuegemea ukanda mmoja wa Nchi kimaslahi si sawa kabisa! Labda kama itakuwa SACCOS!!
 

Mwanakiji samahani mkuu hapa hujaongea kitu labda mda mrefu hujajitokeza jamvini lete mada yenye busara na hoja maana umesema ubovu wa sera ilihali hujaelezea lolote la sera.hebu jenga hoja usilete chuki kwa herufi za ccm
 
Wengine wanafikiria tatizo ni mtu mmoja tu; matokeo yake tunafikiria tukibadili sura basi tunaweza kuwa tumebadili sera...
 
Watu waliposema ni tatizo ni mfumo mlishupaa, mkampigia debe jamaa, yeye ni tofauti, now unakuja tatizo ni sera, sasa huyo mtu wako hafuati sera wala katiba, yeye atavyoamka ndivyo gari atakavyoliendesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…