Hallelujah hallelujah!
Ombi langu kwa serekali yetu tukufu,sioni umaana wa kubadilisha katiba yote kwa maana ya kuanza upya,je haiwezekani jambo hili likafanywa kwa kugeuza baadhi ya vipengele ambavyo vimeshindwa kuendana na wakati wa sasa?
*Kwa imani yangu vipengele vinavuopigiwa sana kelele ni haswa kuhusu uchaguzi huru na mfumo wake!
*Kuhusu serekali na rais kuweza kushtakiwa
*Matokeo ya uchaguzi yawezekane kupingwa mahakamani
====================
Haya ndiyo yamekuwa kilio kikubwa sana kwa upinzani,je hayawezi kurekebishwa bila kutumia mabilioni yasiyo na msingi wowote?
***Mnaweza kuongeza vipengele ili tu serekali isibebe mzigo na wapigaji wakaingiza mikono hapo!
Katiba mpya sio kwamba inafuta vyote vya zamani.
Bali inaboresha na kuongeza baadh ya vipengele.
Wapinzan ni kweli wanataka Tume huru ya Uchaguzi iwe huru. Na wanaochaguliwa wasiwe na Chama cha siasa.
Ila Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, na Wilaya (DEDs) walikuwa ndio wasimamizi wa uchaguzi wa moja kwa moja kwenye maeneo yao kwa mujibu wa nafasi zao za kazi.
Na hawa wote wanachaguliwa na Raisi.
Haya ni ya kisiasa ila yako meng yanamhusu hata asiye na chama.
Mfano sasahiv tuna uhuru wa kuongea ila Rasim ya katiba hii inampa mwananchi yoyote uhuru wa kwenda mahakaman kumshtak kuongoz flan kuwa amefanga hivi au vile kinyume na Haki.
Yaan Kiongozi akikuzingua na ww unaenda mahakaman kumzingua πππ
Akiwa na Mali nying una haki ya kuuliza kapataje. Maana Katiba inasema akiingia madarakan aseme mali zake na akimaliza aseme pia.
Ni meng rasim inaongea kuhusu Haki na wajibu wa Wananchi.
Pia Raisi amepunguziwa madaraka.
Pia kuna muundo wa serikal 3.