Tunapozidiwa hadi na nchi zenye watu laki 3 kwenye Olympics

Tunapozidiwa hadi na nchi zenye watu laki 3 kwenye Olympics

Uganda walikuwa lock down kipindi kirefu lakini waliwekeza kuandaa wana michezo wao sisi tumekalia bla bla tu,
Chaajabu tuna kaa kushangilia mchezaji wa Germany mwenye asili ya TZ kweli tumejichoka kabisaa.
 
Tuna tatizo kubwa la kimkakati linaloanzia kwenye Taifa mpaka hizi ngazi za chini kiuongozi, huwezi kuamini kuna watu ni viongozi miaka rudi nenda na bado ukifika uchaguzi wanachaguliwa tena ili hali hakuna walichofanya muda wao wa uongozi,.
Ili tuweze kusonga mbele tunatakiwa kuwa na shule za michezo kuanzia primary na kuendelea hapo tunaweza kupiga hatua. Yaani kwasasa viongozi wapo ofisini wakisubiri mtu ajitume mwenyewe afanye mazoezi aonekene na wadau kisha wao ndio wanaenda kumdandia na kumpeleka kwenye mashindano.
Nawanampeleka mmoja halafu viongozi wanakuwa 60 hapo ndipo kunamaajabu mengine tena.
 
Nawanampeleka mmoja halafu viongozi wanakuwa 60 hapo ndipo kunamaajabu mengine tena.
Ajabu sana Mkuu, fikiria eti wameenda wanariadha 3 na viongozi 4, tutatoka kweli kwenye hizi mambo? Viongozi wa michezo ni wale wale kila siku, huko riadha miaka na miaka ni wale wale, volleyball, basketball nk, Hivi Bayi bado ni kiongozi ama alishaacha?
 
Tatizo ni serikali kutojali michezo
 
Huwezi kuwa bora kwenye kila kitu, Marekani na umwamba wake wote ule lakini football team yao sio kali kivile

Mkuu unaelewa kuwa Marekani juzi wamebeba ubingwa wa Bara la America Kaskazini?
 
Wale wanaofatilia Olympics wataona kuna nchi kama Bahamas ina Wanamichezo wengi kwenye hii Olympics kuliko sisi. Cha ajabu idadi ya watu huko Bahamas ni laki tatu tu. Sisi wenye milioni 60 tunashindwaje?

Jamaica idadi ya watu milioni 3 tu kama nusu ya wakazi wa Dar. Ajabu wana wanamichezo wengi sana kutuzidi.

Hivi kweli Taifa la watu milioni 60 haya warussha tufe Tu hatuna?

Nchi kama Botswana..Qatar..zimetushinda?

Uganda , Namibia?..

Waziri wa michezo anafanya shughuli gani?
Yuko bize na mbowe na tozo
 
Viongozi riadha na olimpiki wapo kimaslahi zaidi kujifaidisha sio kukuza michezo

Wanamichezo wa Tanzania watabaki kuwa wasindikizaji na watalii
 
Ná sisi kama nchi tuna ubora kwenye mchezo gani kule kwenye Olympics Tokyo?
Huwezi kuwa bora kwenye kila kitu, Marekani na umwamba wake wote ule lakini football team yao sio kali kivile
 
Sio kweli...sisi ni fungu la kukosa tu..
Fungu lakukosa linatokana na aina ya viongozi tulionao.Na viongozi tulionao wanatokana na siasa,kwahiyo utaona tu kua ukishakua na siasa mbovu lazima uwe na viongozi wabovu.na viongozi wabovu wanatoa matokeo mabovu.
 
Muda mwingi tunautumia kwenye siasa
Fikiria saa hii watu wako Space, kesho wako hoi unategemea nini, tunaishi kwa ujanja ujanja tu, kuiba zilizopo bila kuzizalisha
Hiyo wewe unaiona haina faida?.mbona watu wanaongea mambo ya msingi sana.au unataka watu wasichokoze fikra hili tuendelee kua wajinga zaidi.
 
Hiyo wewe unaiona haina faida?.mbona watu wanaongea mambo ya msingi sana.au unataka watu wasichokoze fikra hili tuendelee kua wajinga zaidi.
Usinifanyie udikteta nikose uhuru wa kutoa mawazo. Hayo ni mawazo yangu
 
Tanzania vitu vingi tunafanya kwa kujuana sio kwa uwezo wa mtu we kama huamini fuatilia hizi timu za vijana za Tanzania utasikia abasi kapombe Joseph boco ayubu ninja Alex Maxime nenda kwenye siasa hivyo hvyo kiufupi hautangalii uwezo tunaangalia kujuana ndo maana tunafeli sana katika kila idara.
 
Kilichobaki sasa hivi ni kufurahia medali ya Malaika Mihambo kuwa ni mbongo wakati ni Mjerumani 😂😂😂
Wenzetu Kenya na Uganda wanajiokotea tu medali huko Nipon (Japan)
Serikali ikae ikijua hakuna njia ya mkato Kwa wanamichezo kuleta medali ktk Taifa hili bila kuwekeza kwenye michezo.
Nalog off
 
Nimemwona mu ukraine mweusi amechukua medali ya dhahabu kwenye mieleka.
Hivi Urusi na Croatia wana raia weusi?
Nalog off
 
Huyu Waziri Issue Ya Simba vs Yanga Ilitosha Kumfuta Kazi
Ile Ambayo Haikuchezwa Kama Ilivyopangwa 😂😁🤣😃😄😀
 
Wale wanaofatilia Olympics wataona kuna nchi kama Bahamas ina Wanamichezo wengi kwenye hii Olympics kuliko sisi. Cha ajabu idadi ya watu huko Bahamas ni laki tatu tu. Sisi wenye milioni 60 tunashindwaje?

Jamaica idadi ya watu milioni 3 tu kama nusu ya wakazi wa Dar. Ajabu wana wanamichezo wengi sana kutuzidi.

Hivi kweli Taifa la watu milioni 60 haya warussha tufe Tu hatuna?

Nchi kama Botswana..Qatar..zimetushinda?

Uganda , Namibia?..

Waziri wa michezo anafanya shughuli gani?
Olympic committee yetu ni ya wala rushwa na watu wasiofaa kokote
Wachunguze na uangalie mafaili yao
 
Back
Top Bottom