UTAKUJA UJE
Member
- Aug 4, 2020
- 34
- 78
Nimeshangaa kumsikia mgombea u Rais wa chama cha mapinduzi akitumia vibaya kauli ya Mh Lissu-Rais mtarajiwa wa awamu ya sita na kipenzi cha watu,aliyoitoa akiwa Mwanza kwamba yeye Lissu hayuko tayari kupewa kazi na Magufuli, badala yake akasema hiyo kazi akawape anaowaokota majalalani.
Hapa Lissu alikuwa sahihi kwani Magufuli akiwa Singida ni kama alimdhihaki Lissu kwamba aachane na kugombea badala yake asubiri atapewa kikazi kidogo ambacho ana uwezo nacho.Hii ni dharau kubwa kwa msomi huyu nguli wa sheria,na nataka nimkumbushe Magufuli,yeye hana hati milki ya taasisi ya urais kiasi cha kumtaka Lissu asubiri kupewa kikazi kidogo.Kwa nn yy Magufuli asiachie hiyo nafasi na asubiri Lissu ampe japo nafasi ya kuzibua mchanga kwenye madaraja makubwa?
Kauli ya Lissu ya kutaka Magufuli awape kazi anaowaokota jalalani imerejea alichowahi kusema Profesa Kabudi kwamba anamshukuru Magufuli kwa kumtoa jalalani na kumpa hiyo kazi ya kuteuliwa.Watanzania wote tulisikia na Magufuli anatakiwa kujua kwamba SISI WATANZANIA SIYO WAJINGA!
Nimemshangaa leo akiwa Mkoani mara anaitumia ndivyo sivyo kauli ya Lissu kwamba aliwaita watumishi wote ni majalala. Bila aibu akawataja wateule wake wengi, walimu, waganga, maaskari nk. Magufuli usitupotoshe, nadhani kwa matendo yako unatakiwa kupewa kauli kali zaidi ya hizo kwa maana umetutesa sana Watanzania tulio wengi.
Kituko kingine alichofanya mh Magu ni pale aliposema kwamba ataongeza mishahara ya watumishi kabla hajamaliza muda wake. Ni kichekesho kweli!We unajuaje utaendelea kuongoza? Na kama unajua utaendelea kuwa Rais,kampeni unafanya za kazi gani?Kipindi chako cha miaka mitano kimeisha na sasa wewe ni mgombea huna uhakika wa kushinda ndo maana unatafuta huruma tu!Nafikiri wapenda haki kote dunia wanapaswa kuungana kukukataa kwa nguvu zote!Miaka mitano kila mmoja analia,ukiongezewa miaka mitano si utaua Watanzania wote?Hapana,tumechoka,inatosha,kapumuzike ulikojijengea uwanja wa ndege,TUNASAFIRI NA ANTIPAS LISSU TUNDU,Chaguo la wengi,chaguo la Mungu.HATUDANGANYIKI,SASA,BAAAAAAAASI!