Mkuu punguza jaziba, unatukana daktari mshono haujatolewa nyuzi!
.
Hivi Magu alivyo popular wa ukweli akashinda kihalali kwa kishindo, utasingizia tume imekwapua matokeo?
Ninakushauri safari hii jiandae kisaikolijia, maana dalili za ushindi mnono kwake zipo dhahiri.
Halafu hili la majalala pia nawe umelikuza mno ama umelitafsiri ndivyo sivyo.
Palamagamba mwenyewe aliwahi kulitolea ufafanuzi tamko lake hilo huku akinukuu vifungu vya biblia kwamba hakumaanisha jalala unalotafsiri wewe leo kwa kutokujua ama kwa makusudi.
Kila mwanasiasa ana staili yake ya uongozi hapa duniani na pia binadamu hatujaumbwa kwa ukamilifu.
Maana hata huyo unayempigia debe mheshimiwa Lisu akitawala hawezi kuridhisha kila mtu, naye atalaumiwa pia tena sana tu.
Nyerere mwenyewe muasisi, leo anasifiwa kwa utawala bora, lakini alitawala kwa fimbo ya chuma na yeye aliwahi kukiri wazi wazi, sembuse Munghwaye!
Kwa waAfrika tulivyo, siwezi kumsifia mtu kwa kubet nini atakacholifanyia taifa eti kwa tu kanadi propaganda hizi dhaifu.
Aheri huyu Magu tumemuona, Taifa analisongesha kwa kasi inayotarajiwa.
Wewe ulivyo mbinafsi unalalamikia mshahara, je sisi wakulima tumeongezewa bei ya mazao, na kwa thread yako hii sisi unatuweka kundi gani?
Kwa taarifa yako, huyu ndiyo rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na nchi nyingi barani Afrika kama mfano na dunia kwa ujumla wake, kila mahali wanamlilia kuwa aheri angelikuwa ni rais wao kwa jinsi anavyoliletea taifa la Tz maendeleo yenye kuonekana.
Mimi si mpiga kura mzuri, lakini kwa thread kama hizi, zitanifanya siku hiyo ya trh 28 potelea kwa mbali nami niende nikasongamane ili kuongeza nguvu, maana sasa ngebe zinataka kuzidi kudadadeki.
Sent using
Jamii Forums mobile app