Kwa utaratibu wa rais kutoka kwenye cabinet, ( Mkapa, Kikwete,Magufuli, hata Mwinyi nadhani), walitokea ndani ya cabinet ya Rais anayetoka madarakani, hawakuachwa njiani kama Lowasa
Mgombea kuaminiwa na Rais aliye madarakani, Nyerere hakuna na shida/Mgogoro na Mwinyi, Mwinyi hakuna na shida/Mgogoro na Mkapa, Mkapa hakuna na shida/Mgogoro na Kikwete, as for so Kikwete hakuna na shida/Mgogoro na Magufuli so far Madelu ni kipenzi cha mama Bado na amemuamini kwenye wizara nyeti,
Marais kuanzia BM, JK,JPM walikua na background ya kudumu kwenye cabinet na kuhudumu at least zaidi ya wizara mbili, chini ya Marais wawili kwa ufanisi tofauti, so far kwa CCM huu ndio unaoitwa uzoefu, ingawa Kuna mawaziri wengine Wana hii Sifa kama Bashungwa,Lukuvi, Jafo, Simbachawene, Doto, etc ila Madelu amewazidi kwa kigezo cha Strong Political Mileage kwenye siasa za chama, amewahi kuwa Naibu katibu mkuu bara, alishagombea ujumbe wa NEC Taifa na kishika nafasi ya nne ( Si jambo la kupuuzwa)
Madelu anaweza kuuzika zaidi kuliko remaining candidates wengi ndani ya CCM kwa sababu ana uthubutu mwenyewe, ni mbunifu na ana (hata kwa tai zake za bendera ya Taifa tu😂) then ana political legitimacy ndani ya chama na serikali,
Kipindi CCM kinapitia upinzani mkali kutoka Chadema yenye nguvu enzi za JK ni Madelu pekee wakati akiwa mbunge aliyekua Frontline kupambania kwa kujibu mashambulizi kutoka kwa wapinzani kiasi cha kwamba JK ( M/kiti) aliguswa sana na kumtolea mfano wa kada imara kiasi cha kumvika cheo cha Naibu katibu mkuu
Kingine ana flexibility ya hatari anaziweza siasa za kiuanaharakati mpaka za kidiplomasia,
Hence,
Tulia anahitaji kuuzwa sana unlike Madelu ana asili ya kuuzika mwenyewe so political Profile ya Madelu ni asset kwa CCM zaidi ya Tulia.