mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,707
Duh siyajui vizuri haya ya sheria,ila swali langu hii imekaaje ki diplomasia?Juzi juzi BASATA ilitangaza kumfungia Msanii Diamond Platinumz na mwenzake kwa muda usiojulikana kutokana na kukiukaa sheria kwa kuimba wimbo wenye matusi wimbo uliopigwa marufuku.
Kufungo hicho ni cha ndani ya nchi na nje ya nchi, pamoja na adhabu hiyo lakini Msanii huyo amekaidi amri hiyo na amesafiri kwenda Embu Kenya kufanya Tamasha. Kukiuka amri hiyo tayari kuna mvutano kati ya serikali BASATA na msanii huyo, hivyo tunasubiri mshindi wa mvutano huo.
Rai yangu kwa Wasanii wetu Waheshimu Sheria za Nchi.
Unafurahishwa na matusi ya Diamond? Huna aibu weweAcha upumbavu bas kwahiyo akichukuliwa hatua Kali wewe utafaidika na nini
Watu kama nyie unakuta mnaish kwa shemeji zenu kuanzia asubuh had jion miguu umemyosha kwenye sofa huku ukicheza na watoto Wa Dada yako
Duuuuh! Nimegundua ligi iliyopo sasa......twende kazi!Hapa kuna kupimana nguvu Kati ya Mwakyembe , Shonza na Makonda. Ngoja tuone nani ataibuka mshindi.
jamani mlivyomkomalia Dai??????
Kwanini ungoje wakati mshindi anajulikana? Tangu lini Bashite akashindwa na kiongozi yoyote yule nchii hii zaidi ya akiyemteua tup?Hapa kuna kupimana nguvu Kati ya Mwakyembe , Shonza na Makonda. Ngoja tuone nani ataibuka mshindi.
Nilichogundua mimi mkuu,shida sio kosa alilofanya huyu dogo,bali ni wivu tu kwa huyu mtu. Wabongo tuna nongwa za kipuuzi sana na ndio maana tupo hivi hivi tulivyo,hatusogei,tunapenda kuona mtu kadondoka ili tumseme.
Kosa alilofanya sio la kufungiwa kwa muda usiojulikana,ni mihemuko tu ya kuharibia watu maisha yao ndio iliyotumika hapa.