Usitarajie hilo kwa hii serikali iliyojikita kukamua wanyonge.....Wakati asilimia kubwa ya nchi inakaribia kuunganishwa umeme hasa maeneo ya vijijini ambapo palikua hapajafikiwa kwa asilimia kubwa.
Ikumbukwe kodi/tozo ya REA iliwekwa mahsusi kwa ajili ya kusaidia kupatikana kwa fedha za kusambaza umeme vijijini ambapo mpaka sasa zaidi ya 84% ya vijiji vyote Tz vimefikiwa na umeme.
Macho yetu tunasubiri kuondolewa kwa tozo ya REA kwenyebidhaa za nishati ili kupunguza mzigo kwenye garama za nishati hasa umeme na mafuta.