Tunasubiria shauri lililopelekwa mahakamani kuhusu Michango ya Harusi

Tunasubiria shauri lililopelekwa mahakamani kuhusu Michango ya Harusi

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
7,743
Reaction score
13,657
Kwakuwa shauri lipo mahakamani ni vizuri tusubiri maamuzi ya mahakama.

Lakini michango ya Harusi ni mingi kuliko hata Tozo tunazozipigia kelele kila uchao. Na hili nalo mkaliangalie.

Na kesi ya msingi wakati inasikilizwa ni vizuri kusitisha michango ya harusi kwanza tupate muongozo wa kimahakama na kisheria.

IMG-20220929-WA0041.jpg
 
Ndio maana nasema wajinga na wapumbavu wamejaa humu jf . Mchango wa harusi ni hiari, unatoa Kama utataka kutoa. Na hata anayekupa kadi huwa anakuomba sio kukulazimisha
 
Si asitoe hela yeye,

Tena mtu mwenyewe bonge alafu anaendekeza njaa,

Ukiweza changa, huwezi tulia,
Wengi wanaokataa kuchangia huwa wana pepo la umaskini

Matajiri wengi wenyebroho ya utajiri watoaji sana iwe michango ya harusi,misiba ,sadaka kanisani au misikitini nk wako juu

Kumjua mtu mwenye pepo la umaskini mwangalie kwenye michango iwe ya harusi nk utamjua tu kuwa huyu si tu mapepo la umaskini la kibinafsi bali ana generational curse inayoenda beyond yeye na kizazi chake
 
Ndio maana nasema wajinga na wapumbavu wamejaa humu jf . Mchango wa harusi ni hiari, unatoa Kama utataka kutoa. Na hata anayekupa kadi huwa anakuomba sio kukulazimisha
Hiari!?
Hiari gani hiyo unafuatiliiiwa sio ofcn sio kijiweni mpaka Nyumbani
Message za kukumbusha 5 kwa siku na usipotoa unanuniwa, unaonekana mbaya sijui nini....
Wacha watu waendelee tu kuchangia lkn ukweli si hiari, ina kaulazima flani hv...
 
Hiari!?
Hiari gani hiyo unafuatiliiiwa sio ofcn sio kijiweni mpaka Nyumbani
Message za kukumbusha 5 kwa siku na usipotoa unanuniwa, unaonekana mbaya sijui nini....
Wacha watu waendelee tu kuchangia lkn ukweli si hiari, ina kaulazima flani hv...
Kama kosa kisheria mburuze huyo mfuatiliaji mahakamani kufuatilia.mchango ulioahidi wewe mwenyewe

Unaahidi wakati lofa hela huna wakikufuatilia utimize ahadi lofa mkubwa wewe unanuna.Ulilazimishwa kutamka hugo ahadi ? Ohh nitachingia milioniwakati hata chupi unayovaa inechakaa kwa ulofa huna hela hata ya kununua chupi ya mtumba
 
Si kejwli ila atakuwa mpare huyu. Ila michanho inaboa sana mwezi uliyopita nimemaliza 250k kwa harusi Tena mtu ankufuata inbox kabisa.
 
Hii habari haijakamilika
Ni kweli habari kamili hii hapa

Hai. Mfanyabiashara maarufu wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, James Mushi amefungua maombi madogo akiiomba Mahakama ya Wilaya hiyo itoe zuio la kusitisha usambazaji wa kadi na michango ya harusi ya mtu anayedaiwa kutumia jila lake na familia yake kuchangisha michango hiyo.

Akiwasilisha maombi hayo jana Jumatano Septemba 28, 2022, wakili wa mfanyabiashara huyo, Elia Kiwia, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Julieth Mawole alidai mteja wake huyo ameingia kwenye mgogoro mkubwa na familia yake na kutishia ndoa yake kuvunjika baada ya mke wake kumtuhumu mumewe kuwa ni mzinifu.

"Kati ya tarehe 16 na 20, mwaka 2022 mteja wangu alipata taarifa kuwa katika eneo la Boma ng'ombe, Machame na Arusha kuna mtu alitengeneza kadi kwa ajili ya michango ya harusi na kusambaza kadi hizo za mchango wa harusi kwa kutumia jina lake yeye na mke wake bila yeye kushirikishwa," alisema

"Mheshimiwa kitendo hicho cha mtu huyo kutumia jina la mlalamikaji yeye na familia yake imesababisha mgogoro mkubwa kwenye ndoa na kuhatarisha ndoa yake kuvunjika.

“Ambapo mke wake mlalamikaji amemchukulia mume wake kama mtu mzinifu mwenye watoto nje ya ndoa kwa kumuingiza kwenye michango bila ridhaa yake" alieleza wakili Kiwia

"Fedha hizo mlalamikaji hajui kama zinatumika kwa njia gani na kwamba hana uhakika kama fedha hizo zinazokusanywa kwa kutapeli au anadanganya kwa njia ya kujipatia fedha jambo ambalo aliona na yeye linaweza kumletea shida na familia yake".

"Huyu bwana James na familia yake wanashindwa kuelewa hizo fedha ni za nini na kwamba ni uwezekano wa matapeli wanakusanya fedha kwa kutumia jina lake ambao mwisho wa siku wanaweza kukamatwa yeye na mke wake kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na wanaweza kufungwa."

"Kwa hiyo tumekuja hapa kuomba kadi hizi zisiendelee kusambazwa na huyu anayelalamikiwa pamoja na watu wengine wanne ambao majina yao yako ndani ya kadi hii".

Hata hivyo, hakimu Mawole alitoa zuio usambazwaji wa kadi hizo pamoja na michango hiyo mpaka hapo kesi itakapotajwa Oktoba 19.

Akizungumza nje ya mahakama, mfanyabiashara huyo, Mushi alisema baada ya kupata taarifa zimechapishwa na kusambazwa mtaani alifanya jitihada za kupata kadi hizo katika meneo mbalimbali na kukuta zimeandikwa jina lake.

"Wakati kadi hizi zikiwa zinaendela kusambazwa maeneo mbalimbali iliniletea shida na familia yangu ambapo mke wangu aliniuliza inakuwaje natengeneza kadi za michango ya harusi bila kumshirikisha yeye ndipo akaanza kunituhumu nina watoto nje ya ndoa na hii imeleta shida kwenye ndoa yangu na jamii kwa watu ambao wananifahamu".

"Kwenye ile kadi kulikuwa na majina ya watu watano ambao mimi siwafahamu na wala sikuwahi kukaa kikao chochote na wao kupanga mchango au kitu chochote, kwa kuwa kitendo hiki niliona kinaniletea madhara katika familia ikabidi nimtafute wakili wangu ili tujue ni kwanini hawa watu wanafanya hivi."

Source:Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom